Somo la mali kwa wanandoa kwa kilichotokea kwa Achraf Hakimi na mkewe

Somo la mali kwa wanandoa kwa kilichotokea kwa Achraf Hakimi na mkewe

Dunia haitomsahau Gabriel Villa, mwanasheria kwa taaluma aliyefanya pia kazi ya uwakala wa usafirishaji.

Bwana huyu mwaka 1994 alikutana na mwanadada mrembo Christina Carta kwenye sherehe

Wawili hawa wakapendana na hatimaye kufunga ndoa licha ya kuwa Gabriel alimzidi mrembo huyo miaka 30.

Tajiri huyo mara tu baada ya kufunga ndoa alimpeleka mkewe nchini Jamhuri ya Dominica kwenye visiwa vya nchi hiyo kula maisha kwa miezi minne.

Na waliporudi waliishi pamoja kwenye ndoa ya furaha kubwa kwa miaka 20.

Baada ya miaka hiyo ishirini ya kuishi pamoja hatimaye wawili hawa waligombana na Mwanamke akaenda kudai talaka kisheria ili wagawane mali.

Lakini baada ya kufuatilia taratibu hizo za kisheria, Wanasheria wa Mwanamke huyo walimjulisha kuwa bwana Gabriel alimtaliki mke wake huyo miaka 20 iliyopita bila yeye kujua hivyo kwa miaka yote hiyo hawakuwa wanaishi kwenye ndoa.

Kumbe bwana, ile fungate bwana Gabriel aliyompeleka mkewe nchini Jamhuri ya Dominican alitumia pia mwanya huo kuandikisha talaka kabisa kwa mkewe bila mwenyewe kujua kwani kwa wakati huo ni nchi ya Jamhuri ya Dominican pekee ndiyo iliyokuwa inaruhusu kisheria talaka kutolewa bila mmoja wapo kujua.

Mwamba huyu alipoulizwa alisema alijua kuwa siku moja Mwanamke huyo angetumia mbinu ya kudai talaka ili kuchukua mali zake hivyo alijiandaa mapema😀

NDUGU YETU HUYU ANAPASWA KUPEWA CHEO GANI😀😅?

👇👇👇View attachment 2592307
Haki Ya Mungu huyu Jamaa Apewe Cheo cha Uwanamume Uliotukuka au Nadanganya Wakuu dronedrake adriz Liverpool VPN
 
Sheria ya Uislmau kwenye Ndoa linabaki kuwa ndio Sheria Sahihi na Salama kabisa.
 
PILI, mnaweza kuwa na makubaliano kuhusu kila mali,kuanzia zile ambazo mlikuwa nazo kabla hamjaoana, mpaka zile mtakazopata wakati wa ndoa. Mtakubaliana ipi iwe ya pamoja na ipi iwe ya mmoja.

Japo hili ni gumu kwa maisha yetu sababu ukilianzisha hili utaambiwa HUNA MAPENZI YA KWELI.
Hii si ndio wanaita prenup? Sikua najua kama bongo inatambulika kisheria
 
Back
Top Bottom