Najiuliza sipati jibu hivi inakuwaje Great Thinker anaweza kuhusisha Elimu na Dini ya mtu.
Uzi huu toka ulipoletwa na mleta mada in a smart way alionyesha dalili ambazo kwa tafsiri yangu ni aina fulani ya mchezo [game] ambao unazaa question mark pale alipo mcc faizafoxy.
Tafsiri yangu binafsi ambayo kwa waerevu wanaunga dot.
Kitendo cha mleta mada kumcc Faizafoxy kwa jambo linalo husiana na mtoto wa marehem Malima ni ishara ya mambo makuu mawili.
1: Faizafoxy ni shabiki sana wa mijadala ya udini ambayo inashabiana na siasa za Taifa.
2: Ni mnazi wa kujadili ushindani wa taaluma unaoangalia sana mwenye taaluma husika ni muumini wa dini ipi.
Kijana Malima ni Mtanzania kama watanzania wengine,kitendo cha mafanikio yake kujadiliwa na kuyapa sura za kiushabiki wa udini badala ya mjadala kuangalia changamato za mafanikio yake na kuona mtanzania mwingine atapataje fursa kama aliyopata Asanterabi.
Majadliano ya mafanikio au upeo aliofika Asante yanaweza kwenda mbali kwa kuangalia historia yake, wazazi wake, shule alizosoma, marafiki zake waliomzunguka na mengineyo, lakini pale watu wanapovuka mipaka na kuangalia angle ya dini ni UFANATICISM.
Malima Yes na ndio alikuwa Muumini wa dini ya Kiislam, kama imani yake ya kumcha Mungu wake hapa duniani. Elimu na dini ya mtu vinauhusiano gani kiasi cha kusema dini yake ndio msingi wa mafanikio yake na kuwa kwa mafaniko hayo basi ubora wa dini ndio shina la kujadiliwa kweli na great thinkers hapa jukwaani.
Ukweli wwa wengine tunaumia sana kunapoibuka mijadala ya dini isiyokuwa na A wala BE. Sie wengine tumezaliwa unakuta Baba yako mdogo ni Sheikh wakati Shangazi yako ni Sister na Mjomba wako ni Pastor na wote mnakula na kulala pamoja kama familia moja, tena familia yenye mshikamano wa ajabu.
Mimi kama ni mjadala ajadiliwe kijana Malima kwa angle zenye mashiko ,nani asiyejua kuwa Marehem Malima alikuwa bright na kama alikuwa bright kizazi chake kama ni matokeo ya vipimo vya kisayansi basi hata Asanterabi anauwezo mkubwa tu kuwa bright hata zaidi ya Baba yake [Wanasayansi wanasema 80% ya akili ya mtoto ni ya Kurithi wakati 20% ni akili ya anayopata kutokana na mazingira yanayomzunguka.].Sasa udini hapa na akili ya Asanterabi vinatoka wapi hasa wale wachangiaji wahusudisha udini?
OMBI KWA MODERATORS NA THINKERS WA JF.
Tufike sehemu moderators na Great Thinkers wote kwa umoja wetu tuwe SENSITIVE na swala la UDINI kwenye mada za SIASA, SCIENCE au mada toka angle yoyote isiyoshabiana na kutokana na mjadala DINI kama Mada kwa uzito wa hoja anzishwa.
Mode ni vyema ukaibuka utamaduni wa kupigaban na mpigwaji akionekana kudumu kwenye tabia hiyo basi apigwe TOTAL BAN aludi kwa ID nyingine, na kwa kuwa jasili aachi asili atajitokeza tu ale TENA BAN.Kuna wengine humu wameshakuwa na majina makubwa kula TOTAL BAN na kuja kwa jina jipya UKWELI ITAWACOST MNO hivyo watajiheshimu na kubehave kama GREAT THINKERS.
Jukwaa linawakilishwa kada fulani kubwa ya mchanganyiko wa Watanzania wengi, wenye umri mkubwa, umri mdogo, wanawake, wanaume, vijana, wazee, walioa, ambao awajaoa, Wakristu, Waislam, Hindu, Dini za jadi, na wengineo wengi wakiwemo wasio na dini.
Sasa kuendelea kuendekeza tabia ya kuruhusu majadiliano ya UDINI kwa sura za namna hii, TUNATENGENEZA CHACHU ambayo POLEPOLE inazaa ISHARA MBAYA!!!
Nisivyo na ITIKADI ya vyama vya siasa, ndivyo vivyo vivyo mimi nisivyo penda UTUMIAJI HOJA ZA DINI. Binafsi nina IMANI ya DINI yangu, ambayo kwa malezi nimelelewa na kuzungukwa na dini zingine nikiona ni sehemu ya MAISHA yangu.Ukifika wakati wa kumsujudia MUNGU kila mmoja anamsujudia kwa IMANI YA DINI YAKE , kwenye dhehebu lake, bila bughudha wala kero toka kwa Mwanafamilia, tena wanafamilia wanatoa msaada kuona azima yake ya kumtumikia MUUMBA wake kwa IMANI yake INATIMIA kupitia mikono ya na maombi ya wanafamilia.
Siku moja nilikwenda kwenye nyumba moja ya ibada nikakuta familia moja maalufu kwenye Biashara na Medani ya Soka na Michezo ambayo kiimani ni waumini wa Dini tofauti na eneo husika lakini kwa utamduni wa malezi yao, wako pale kama wanafamilia kujumuika na MDOGO WAO ambae ni muumini wa dhehebu tofauti na wao tena akiwa ni KIONGOZI ambae alikua amekuja toka MKOANI kwa ajili ya SEMINA YA KIDINI kwenye dhehebu moja kubwa Tanzania.
Familia ile iliudhuria IBADA ile aliyokuwa anaendesha MDOGO wao na mwisho wa IBADA familia ile ya WANAMICHEZO NA WAFANYABIASHARA WAKUBWA walipewa nafasi ya kujitambulisha na kusema machache na moja kubwa ni kuwa KIONGOZI huyo wa KIIMANI wa madhehebu hayo ya Kikiristo amefika pale kwa support ya wanandugu hao ambao binafsi wana DINI na wana sali dhehebu tofauti mdogo wao huyo ambae walikuja kumsupport kiimani wakati huo.
Picha ile ya Familia ya Wanamichezo hao ni Picha ya Familia nyingi sana za Kitanzania ikiwemo yangu pia.Tukikutana kama familia uwezi tambua kuwa yupi ni muumini wa dini au dhehebu fulani.
MODE, SWALA LA UDINI LIWE NA UKOMO TAFUTA JIBU.
Tusitambuane kwa UDINI humu.....