KERO Responded Songea: Hali ya Soko la Bombambili si salama, wakati wa mvua hali ni mbaya

KERO Responded Songea: Hali ya Soko la Bombambili si salama, wakati wa mvua hali ni mbaya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

NBica

Member
Joined
Sep 13, 2010
Posts
44
Reaction score
41
Hali ya Soko letu la Bombambili hapa Mkoani kwetu Songea Mjini sio nzuri hasa inapotokea mvua imenyesha, miundombinu yake inakuwa siyo rafiki.

Wafanyabiashara na wateja wote wanapata wakati mgumu kupita na kufanya shughuli zao nyingine kutokana na matope, uchafu na mvurugano uliopo

Kinachotusikitisha ni kuwa kila mwaka Serikali imekuwa ikisema itarekebisha na sasa miaka inakata lakini hali bado ni ileile.
WhatsApp Image 2025-03-28 at 12.21.43.jpeg
Ikumbukwe kuwa soko hili lilipokea pia Wafanyabiashara kutoka Manzese ambao soko lao lilivunjwa, so wingi wa watu wote hao unafanya mazingira kutokuwa rafiki kabisa na hata afya zetu kuwa hatarini.


Pia soma:
~
Mkurugenzi Manispaa ya Songea akabidhi eneo la Mradi wa Ujenzi wa Soko la Sh Bilioni 22.9 - Manzese A na B

~ Songea: Baada ya malalamiko ya Wananchi, RC wa Ruvuma afanya ziara kukagua Soko la Bombambili na masoko ya Manzese A
 
Ila soko la bm2 liko hovyo mno toka kimuundo na hata mazingira yake, hali ni mbaya tena kule chini kwa wakulima ndo hatari kabisaa.

Ndo maana mie naendaga soko kuu town kuchukua mahitaji.

Viongozi wako bize kula hela na kutanua Lol.
😢😢😢😢
 
Daah Usimamizi wa soko uliangalie hili kwa makini, wasifanye masihara kwenye afya za Watanzania
 
Back
Top Bottom