Hali ya Soko letu la Bombambili hapa Mkoani kwetu Songea Mjini sio nzuri hasa inapotokea mvua imenyesha, miundombinu yake inakuwa siyo rafiki.
Wafanyabiashara na wateja wote wanapata wakati mgumu kupita na kufanya shughuli zao nyingine kutokana na matope, uchafu na mvurugano uliopo
Kinachotusikitisha ni kuwa kila mwaka Serikali imekuwa ikisema itarekebisha na sasa miaka inakata lakini hali bado ni ileile.
Ikumbukwe kuwa soko hili lilipokea pia Wafanyabiashara kutoka Manzese ambao soko lao lilivunjwa, so wingi wa watu wote hao unafanya mazingira kutokuwa rafiki kabisa na hata afya zetu kuwa hatarini.