Songwe: Askari waliovuka mpaka kuingia Malawi kinyume cha sheria wafukuzwa kazi

Askari 7 wanamfukuza bodaboda mmoja, ila hawa ndugu sijui hata wanawaza nini

PGO ndio yanapoanzia matatizo yote, kama mimi Raia najua kuvuka mpaka wa nchi nyingine ukiwa na silaha za moto, mavazi au sare za kijeshi au kuvuka bila kutimiza vigezo ni kosa wao walishindwa nini kujua hilo
 
Eti waliona piki piki wakaikimbiza wakizani ina magendo.... ujinga mtupu yaani sijui wanakuwa trained vipi hawa jamaa. Hapo utakuta walikuwa wanakimbiza wapate rushwa.
 
Happy hakuna tofauti na wale wafanyakazi wa TRA waliopoteza maisha Kwa ajili kukimbiza magendo. Tofauti ni kwamba wale wamepoteza maisha, Hawa wamepoteza kazi Ila wote walikuwa wanakimbiza ili kupata Cha juuuu!!!!
 
RPC anasema waliwashtaki hao Polisi kwa kufuata Kanuni zao zinazowaongoza Jeshi la Polisi yaani PGO.

Kesi ya kina RPC Kiangi na wenzake ni ngumu sana, kama hawakufuata Sheria zilizopo kwenye PGO na wao watakuja kushtakiwa na kufukuzwa kazi.
 
RPC anasema waliwashtaki hao Polisi kwa kufuata Kanuni zao zinazowaongoza Jeshi la Polisi yaani PGO.

Kesi ya kina RPC Kiangi na wenzake ni ngumu sana, kama hawakufuata Sheria zilizopo kwenye PGO na wao watakuja kushtakiwa na kufukuzwa kazi.

Hii kitu kanuni za PGO inawasumbua sasa, wanatakiwa kuisoma, kuifahamu na kuitumia katika kazi zao

Tanzania Police Force in modernisation strides - Daily News

7 Aug 2020 — TANZANIA Police Force (TPF) is on the verge of reviewing its Police General Order (PGO) that would incorporate addressing administration
 
Uko sahihi.
 
Safi saaaan ukisikia polisi zero ndio hao hata km sijasoma sheria nisingekuwa na akil hizo za kuingia mpakan mwa watu bila kibal kwenda kuwakamata
 
askari wetu hamna kitu wanajua yani ni tatizo la mfumo kuingizana kwa baba kanituma wapo wapo tu haishangazi wakifanya makosa makubwa kama hayo.
hata movie hawaoni hahaha unaingiaje nchi nyingine kwa namna hiyo ndo mana risasi wanapiga 10 inafika mwilini 1
 
vipi bosi aliyewatuma mbona bado anaendelea kupokea mshahara?
 
PGO, PGO Kuhusu mtuhumiwa akikimbilia nchi jirani inasemaje?

Naomba kazi nikafundishe PGO kama building capacity kwa jeshi letu afadhali.
 
Hizi njaa zitawamaliza polisi. Wengine watwangwa risasi na Hamza wakitaka kumpora, wengine wamejisahau kama wamevuka mpaka wako nchi ya watu wakiwa mbioni kumpora mtu mali zake.
 
Bodaboda alistiriwa vizuri na Wamalawi, lakini wananzengo wakaambulia kipigo. Kwa nini Wamalawi hawakumkabidhi mhalifu wao wakaamua kuwashushia kipondo vijana wetu? Kwa nini isiwe vinginevyo? PGO haikusomwa? Hii inatafakarisha sana.
 
Pgo ni(police general orders)
Unapewa maagizo na mkubwa wako aliyekuzidi cheo ili ufate maagizo yake.
Huu ni muongozo wa utendaji kazi(code of conduct) au ni maagizo ya mkubwa wako wa kazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…