Songwe: Askari waliovuka mpaka kuingia Malawi kinyume cha sheria wafukuzwa kazi

Songwe: Askari waliovuka mpaka kuingia Malawi kinyume cha sheria wafukuzwa kazi

PGO hata Mimi inanichanganya sijui hata hao police wataweza kuilewa!
 
Hii adhabu ni kubwa sana , ni Bora wasingelipa mshahara hata mwaka mzima, huku wakiendelea na majukumu yao
 
Hii adhabu ni kubwa sana , ni Bora wasingelipa mshahara hata mwaka mzima, huku wakiendelea na majukumu yao
Hujui kwa askari kuvuka mpaka ukiwa umevaa uniform na silaha juu bila taarifa yoyote inatafsiriwa kama uvamizi kwenye nchi ya watu?hiyo adhabu ni stahiki kwao kabisa.
 
Hujui kwa askari kuvuka mpaka ukiwa umevaa uniform na silaha juu bila taarifa yoyote inatafsiriwa kama uvamizi kwenye nchi ya watu?hiyo adhabu ni stahiki kwao kabisa.
[emoji3166][emoji3166][emoji3166] tungewasamehe sababu ni policcm
 
21 SEPTEMBER 2021
ILEJE, SONGWE
TANZANIA

ASKARI WA POLISI WATANZANIA WALIOINGIA MALAWI WAFUTWA KAZI, PIA WALIKIMBIA NA KUTEKELEZA SILAHA ZAO

WALIKUWA KATIKA OPERESHENI AMBAYO HAIKUFUATA KANUNI ZA GPO

Askari 7 wa kituo cha Polisi cha Ileje bila kutoa taarifa kokote wala kibali cha IGP wa Tanzania waliingia katika nchi ya Malawi wilaya Chitipa wakidai kufukuzia magendo wakiwa na silaha 2 za SMG kila mmoja ikiwa na risasi 30 na gari moja la jeshi la Polisi la Tanzania.

Kufuatia kitendo hicho walikumbana na wananchi wa wenye hasira kali Malawi kupelekea askari polisi 4 kukamatwa pamoja na silaha mbili, risasi 60 na gari la polisi lenye usajili PT kushikiliwa nchini Malawi.

Askari hawa kwa kushindwa kufuata sheria ya utekelezaji kazi, kupata ruhusa, kutumwa / kupewa idhini halali toka ofisa wa Cheo cha juu kama zilizoainishwa na kanuni za GPO (general police orders), jeshi la Polisi kupitia mkuu wa Polisi mkoa wa Songwe amewafukuza kazi askari kwa kudhalilisha Jeshi la Polisi na pia kuifedhehesha nchi kwa vitendo vyao kufanya kazi bila kufuata GPO zinavyotaka.

Source : MATUKIO DAIMA TV
Ni kutelekeza na wala si kutekeleza... halafu mbona mnatuchanganya mara kule wanatuambia AK47 huku wewe watuambia SMG, which is which?
 
Bado madogo wale,tamaa ya hela imewaponza,lakini warudi uraiani wajipange upya,wanaweza wakaja wakatusua kinoma kwa miaka ijayo.
Kila la kheri,na pole kwao.
Wale wa sayansi wakasomee hata udaktari na kazi nyingine,wale waliojua ujasiriamali,wakomae,watatusua,hiyo ni ajali kazini.Ila GPO ni kisanga kwa hawa ndugu.
Hiyo GPO ndi and kitu gani boss
 
Tatizo la Askari wengi wa Tanzania ni njaa.
Njaa hadi inawatoa utu wao.

Yohana Mbatizaji alionya hili zamani sana ila hawa wenzetu hawasikii kabisa.

Luka 3:14
Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu.
 
Nahitaji mlinzi nafasi wazi tuma maombi vigezo na mashariti kuzingatiwa
 
Neno "FUKUZWA KAZI" ni mara chache sana nimelisikia(tena sikumbuki mara ya mwisho ni lini na ilikuwaje?) Mara nyingi tunasikia "SIMAMISHWA KAZI" Ambapo tafsiri yake yawezekana baadae aliyefukuzwa akarudi kazini...

Lakini awamu hii hawakutaka kulembe,
 
Mwenda zake ndo chanzo cha haya aliwapa nguvu sana sasa vichwa vilivimba wameamua waingie malawi kusaka hela za kiwi kama ulivyo sema mwendazake
 
PGO hawasomi iwaelekeze namna ya kuvuka mipaka ya Nchi.....Polisi pia mjulize kwanini mkipata shida Wananchi wengi hawasikitiki??
 
Back
Top Bottom