Songwe: Askari waliovuka mpaka kuingia Malawi kinyume cha sheria wafukuzwa kazi

Songwe: Askari waliovuka mpaka kuingia Malawi kinyume cha sheria wafukuzwa kazi

Hapo order ilitoka kwa bosi wao. Afande akisema tuvuke hamuwezi kumbishia.

Wakufukuzwa hapo alikuwa ni mmoja tu, kiongozi wao.
 
Septemba 15 askari Polisi wa Tanzania waliingia Malawi kinyume cha sheria wakimfukuza bodaboda waliyedhani amebeba biashara ya magendo ambapo walipoingia Malawi walipigwa mawe na wamalawi na kuokolewa na Polisi wa Malawi

Askari 7 wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ileje mkoani Songwe wamefukuzwa kazi kwa kosa la kuvuka mpaka na kuingia nchini Malawi wakiwa na mavazi ya kijeshi na silaha za moto kinyume na taratibu za kijeshi

Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe Janeth Magomi amethibitisha tukio hilo

Pia soma: Polisi wa Tanzania wanasa Malawi wakifuatilia wahalifu
Wamewaonea. Wa kufukuzwa ni Siro. Kwa nini Polisi wake hawajui taratibu za kipolisi (PGO) wanapotimiza wajibu wao? Je, wanafumdishwa na kuoimwa kuona kama wameelewa? Au polisi hawafundishiki, ikiashiria hawana akili ya kuelewa hata wakifundishwa?
 
Polisi wenyewe ni form 4 wenye dvn 4 wanajua nini kuhusu sheria?
Bora wanajeshi kuliko hawa polisi, polisi elimu inatakiwa wachukuliwe watu wenye diploma, degree na masters.
Labda walikua doria
 
Hawa jamaa wangewakuta wa Malawi wana akili kama zao sahizi tungekua tunaongea story nyingine.
Polisi wetu wafundishwe misingi ya kazi zao.
 
Askari 7 wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ileje mkoani Songwe wamefukuzwa kazi kwa kosa la kuvuka mpaka na kuingia nchini Malawi wakiwa na mavazi ya kijeshi na silaha za moto kinyume na taratibu za kijeshi
Tukisema mafunzo wanayopitia yana mapungufu wanajigamba ati mtaala wa Polisi Tanzania hakupo mahali pengine duniani kila nchi inaushangaa ulivyo mzuri!!!🤣🤣
 
Back
Top Bottom