Songwe: Askari waliovuka mpaka kuingia Malawi kinyume cha sheria wafukuzwa kazi

Songwe: Askari waliovuka mpaka kuingia Malawi kinyume cha sheria wafukuzwa kazi

Hii ndio taarifa mpya kutoka kwenye Jeshi la Polisi Tanzania , Idadi ya Polisi waliofutwa kazi ni 7

Siku chache zilizopita tuliripoti tukio la Polisi wa Ileje kushambuliwa nchini Malawi na magari yao kuharibiwa baada raia wa Malawi kupinga askari wageni kuvamia nchi yao.

Hii ni wiki ngumu sana kwa Polisi, huku haya yakitokea kule kwingine kuna PGO!
PGO ni kielelezo (mfano) mmoja tu wa uozo ulioenea kila sehemu serikalini!
 
Mkuu hawa ni wale waliofeli O level hawajui hata PGOs wanayotakiwa kufanya kazi nazo kila siku sembuse mipaka ya nchi yetu.

kila kitu itaonekana chanzo ni elimu zao,mpaka tuje kushtuka kuna maprof wametukwamisha vya kutosha,tayari tuko shimoni.

na hii huwa ni mbinu ya haraka kujaribu kukwepa tatizo,yaani unalipa sababu ya haraka.
 
Lakin pia pongez kwa wananch wa malawi sio mazombi. Kitendo cha kuwatwanga hao vilaza walioingia kwako ni cha kizalendo na kujielewa..

Njoo sasa huku kwetu kwa mazombi, kule Tarime one time police wakenya walivuka mpaka kuwakamata boda boda waliokuwa wanavuka mpaka kwenda Kenyaa..

Mazombi ya tz yakawa yanasema tu mbona wamevuka mpaka..mbona wanawashika..alaf yamekaa tu kutazama..
Vichwa wa wabongo vimejaa simba na yanga tu..shwaini
Kwanini usingeenda kupambania nchi over hao polisi?!
 
Hv hao jamaa hawasomagi hilo dubwasha linaitwa PGO!!??
Au limeandikwa kwa kithungu, jana kuna mtu nafanya nipo nae ofisini akawa ananiambia anahangaikia mdogo wake alikuwa jkt ili aingie polisi lakini wamemkataa eti ana dibision 3 wanataka 4 ya 28,nikasema kweli PGO itaendelea kuwa msamiati
 
Hii ndio taarifa mpya kutoka kwenye Jeshi la Polisi Tanzania , Idadi ya Polisi waliofutwa kazi ni 7

Siku chache zilizopita tuliripoti tukio la Polisi wa Ileje kushambuliwa nchini Malawi na magari yao kuharibiwa baada raia wa Malawi kupinga askari wageni kuvamia nchi yao.

Hii ni wiki ngumu sana kwa Polisi, huku haya yakitokea kule kwingine kuna PGO!
Yaani SIRO ameharibu jeshi la polisi hadi ina fika mahali hata RPC hajui PGO ina mtaka askari kufanya kitu gani na ni kitu gani hstahili kufanya. Bado Mama Samia haoni huo uozo
 
Back
Top Bottom