Songwe: Askari waliovuka mpaka kuingia Malawi kinyume cha sheria wafukuzwa kazi

Songwe: Askari waliovuka mpaka kuingia Malawi kinyume cha sheria wafukuzwa kazi

Septemba 15 askari Polisi wa Tanzania waliingia Malawi kinyume cha sheria wakimfukuza bodaboda waliyedhani amebeba biashara ya magendo ambapo walipoingia Malawi walipigwa mawe na wamalawi na kuokolewa na Polisi wa Malawi

Askari 7 wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ileje mkoani Songwe wamefukuzwa kazi kwa kosa la kuvuka mpaka na kuingia nchini Malawi wakiwa na mavazi ya kijeshi na silaha za moto kinyume na taratibu za kijeshi

Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe Janeth Magomi amethibitisha tukio hilo
Du!! Ajira zenyewe ngumu mura.

ANAEJUA MAANA YA ALAMA IYO YA KUSHOTO, SIMU IYO
Screenshot_2021-09-21-18-36-06-27.jpg
 
Ata katika biblia waliambiwa watosheke na mishahara yao, hawa jamaa wakiona pesa akili wanaweza kuziacha popote
CCM ndio imewafanya wawe watumwa maskini jamani na wanawatumia Kama makondom. Wakisikia kongamano la Chadema kudai KATIBA mpya mnakwenda kuwapiga ili Hali KATIBA mpya ingewasaidia kuboresha maslahi na utu wenu. Ona Sasa mmefukuzwa kazi na Mkoloni wenu mtajutaa.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
CCM ndio imewafanya wawe watumwa maskini jamani na wanawatumia Kama makondom. Wakisikia kongamano la Chadema kudai KATIBA mpya mnakwenda kuwapiga ili Hali KATIBA mpya ingewasaidia kuboresha maslahi na utu wenu. Ona Sasa mmefukuzwa kazi na Mkoloni wenu mtajutaa.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
Da kidogo tu umeingizia dukuduku lako mwanangu, si polisi wa Tanzania tu hata wakati wa Biblia walikuwa hivyo hiyo ndiyo hoja, maumivu yako hayaingii hapa ndiyo maana hata Bob aliimba bufaloo soja ni hicho hicho. Chadema inawatesa sana.
 
Ebwana eeh kama akifanya ujanja asiporudisha sare anahama nazo mkoa mwingine anakua anatapeli watu.

Anajua muundo wa jeshi la polisi na taratibu zake so inakua rahisi tu kukamata vinabo na kuvipiga.
 
Hii ndio taarifa mpya kutoka kwenye Jeshi la Polisi Tanzania , Idadi ya Polisi waliofutwa kazi ni 7

Siku chache zilizopita tuliripoti tukio la Polisi wa Ileje kushambuliwa nchini Malawi na magari yao kuharibiwa baada raia wa Malawi kupinga askari wageni kuvamia nchi yao


Hii ni wiki ngumu sana kwa Polisi , huku haya yakitokea kule kwingine kuna PGO !
Lakin pia pongez kwa wananch wa malawi sio mazombi. Kitendo cha kuwatwanga hao vilaza walioingia kwako ni cha kizalendo na kujielewa..

Njoo sasa huku kwetu kwa mazombi, kule Tarime one time police wakenya walivuka mpaka kuwakamata boda boda waliokuwa wanavuka mpaka kwenda Kenyaa..

Mazombi ya tz yakawa yanasema tu mbona wamevuka mpaka..mbona wanawashika..alaf yamekaa tu kutazama..
Vichwa wa wabongo vimejaa simba na yanga tu..shwaini
 
Back
Top Bottom