Songwe: Basi la Kampuni ya Kilimanjaro Express lapata ajali, watu wanne wafariki dunia

Songwe: Basi la Kampuni ya Kilimanjaro Express lapata ajali, watu wanne wafariki dunia

Basi la mkoa gani bwashee wanakalia hadi vindoo.

Nijuavyo hayo mambo ilikuwa zamani sana!
Bwashehe nilipanda basi maarufu kutoka Songea, kufika Njombe kuna abiria wawili walikalia vindoo, mwingine alikalia begi lake. Kufika Iringa wakapata siti wote, ila akaingia mwingine yeye aliamua kulala kabisa katikati pale.

Sasa abiria kama huyu hata ikitokea ajali ndogo si atakufa tu huyu!
Kibaya zaidi kutoka mwanzo wa safari hadi mwisho hakuna trafiki aliyeingia ndani kukagua.
 
Dreva wa leo sijui alikua waziri na konda wake enjo au ni nani
 
Basi la mkoa gani bwashee wanakalia hadi vindoo.

Nijuavyo hayo mambo ilikuwa zamani sana!
Mkuu,
Alhamis wiki iliyopita nilipanda kimotco mida ya Saa nane kasoro mchana, (nadhani ile inayotoka arusha), kutoka Dodoma kuelekea Iringa, abiria wenzangu walikalia mabegi yao kwenye kile kikorido cha kupita, wengine walikalia zile "arm rest", na wengine kusimama kabisa, pia yule kondakta alikuwa anaenda siti za nyuma anawaomba wakae watu watatu katika siti zilizotengenezwa kwa ajili ya kukaa watu wawili tu(muundo wa siti za basi hilo ni 2 by 2(2*2)).

Na Bado njiani waliendelea kuchukua raia/abiria.Wakati wa kukata tiketi ukiuliza siti zipo wanakwambia zipo za kutosha.

Katika "Traffic Stops" zote kutoka dodoma mpaka ninafika iringa hakuna polisi alieingia ndani ya basi. Mwana usalama pekee alieingia ndani ni afisa wa uhamiaji pale mtera basi.

Haya mambo yapo na yanaendelea.
 
Back
Top Bottom