Songwe: Basi la Kampuni ya Kilimanjaro Express lapata ajali, watu wanne wafariki dunia

Hiyo njia imejaa madereva na mawakala wapumbavu kuliko njia zote. Kutwa kushindanisha gari gani inawasili stand mapema. Kilimanjaro nao wameingia kwenye huo mchezo. Kuna dereva wa hovyo sana. Waajiri watu wazima na wazoefu. Vijana ni chinjachinja.
Bus la kampuni ya Kilimanjaro limepinduka asububuhi hii mkoani Songwe likitokea Tunduma kuelekea Jijini Dar es salaam ambapo taarifa za awali zinaeleza ajali hiyo imesababisha watu kadhaa kufariki na uwepo wa majeruhi, taarifa kamili zitakujia hivi punde.

===================

Basi la Kampuni ya Kilimanjaro Express limepata ajali kwa kupinduka asubuhi ya leo Machi 14, 2022 Mkoani Songwe wakati likitokea Tunduma kuelekea Jijini Dar es Salaam.

Taarifa za awali za mashuhuda waliopo eneo la tukio zinaeleza ajali hiyo imesababisha watu kadhaa kufariki na uwepo wa majeruhi.

Ofisa Mmoja wa Kilimanjaro Express amekiri kutokea kwa ajali hiyo lakini hakuwa tayari kuelezea kiundani kwa madai siyo msemaji wa kampuni. Juhudi za kumpata RPC wa Songwe, Janeth Mgomi zinaendelea ili kupata ripoti kamili.

Ripoti kamili ya tukio hilo itafuata muda si mrefu...

View attachment 2149697
View attachment 2149696
View attachment 2149698
 
Wapumzike kwa amani waliotutoka na nawaombea uzima na nafuu majeruhi wote [emoji120]
 
Mbona picha inaonyesha gari limeanguka 2kms kutokea main road. Ni nini kimetokea?
RPC Songwe amefunga simu.
 
Newforce mchina na ndagu zenu za kibongo , wapi na wapi ?
Maana ndo anapelekea mabus meeengi sana maeneo hayo labda nae anatumia ndagu kama mnavyoamini wabongo wengi mambo ya ndagu. Kuna jamaa kasema mabus yanayoenda maeneo hayo wanatumia ndagu ndo nikamtajia Newforce maana ndo anapeleke gari nyingi uko.
 
Kuna mtu kasema humu chanzo cha ajali ni over take.na inaonekana sehemu aliyochagua dereva kuovertake sio nzuri.
 
Bus ya abiria, differential mbili za kazi gani hasa?

Tunduma-dar ni kama 935km! Hebu nitajie bus yenye diff zaidi ya moja inayoanzia dar kwenda bukoba 1400+ km!
Nyanda za juu kusini kuna mizigo mingi sana kuja Dar.... ukipeleka single diff kila siku utagombana na abiria au utapigwa faini mizani. Ndio maana wanaepeleka double diff. Wengi waliojaribu na single waliishia kuchemka. Kila abiria na kiroba cha mchele na cha ndizi.
 
Unamaanisha terias?
 
Unatakiwa ujue sio kila ekseli ya nyuma ni diff!
 
Magari yenyewe mengi ya Kilimanjaro yalianza maisha kama LGV trucks huko anaponunua Sawaya akishayaleta bongo anayabadili kuwa mabasi na body anaunga mwenyewe.

Sasa upande basi kama hilo ambalo lipo zaidi ya 10 barabarani na njia zetu hizi; si suicide mission hiyo. Huu utaratibu wa kununua LGV na kuyageuza mabasi na wenyewe ushapitwa na wakati, sidhani kama Kilimanjaro wana bus ambalo lilinuliwa original likiwa basi.
 
Mabasi yana namba ABX bado yanapiga long safari sio sawa! Hata Abood ana kamchezo hako; yale ya zamani ndio yanapigishwa long safari; mapya yanaishia hapo Morogoro. Huwa siwaelewi.
Hayo mascania ni imara Sana Mchina route ndefu linakufa ndani ya muda mfupi, Scania ina roho ngumu na mizigo yanabeba na mizani hayasumbui!
Pole SANA kwa wahusika! Daah
 
Magari yenyewe mengi ya Kilimanjaro yalianza maisha kama LGV trucks huko anaponunua Sawaya akishayaleta bongo anayabadili kuwa mabasi na body anaunga mwenyewe.

Sasa upande basi kama hilo ambalo lipo zaidi ya 10 barabarani na njia zetu hizi; si suicide mission hiyo. Huu utaratibu wa kununua LGV na kuyageuza mabasi na wenyewe ushapitwa na wakati, sidhani kama Kilimanjaro wana bus ambalo lilinuliwa original likiwa basi.
Acha mambo ya kuhisi hisi. Kampuni ina bus mengi tu ya kuagiza ambayo hata kampuni zingine zinaota kuyamiliki.
Screenshot_20220314-110543.jpg
 
Magari yenyewe mengi ya Kilimanjaro yalianza maisha kama LGV trucks huko anaponunua Sawaya akishayaleta bongo anayabadili kuwa mabasi na body anaunga mwenyewe.

Sasa upande basi kama hilo ambalo lipo zaidi ya 10 barabarani na njia zetu hizi; si suicide mission hiyo. Huu utaratibu wa kununua LGV na kuyageuza mabasi na wenyewe ushapitwa na wakati, sidhani kama Kilimanjaro wana bus ambalo lilinuliwa original likiwa basi.
Nimesema hapa hayo mabasi mabovu mabovu sana lakini mshana jr anabisha!
 
Hayo mascania ni imara Sana Mchina route ndefu linakufa ndani ya muda mfupi, Scania ina roho ngumu na mizigo yanabeba na mizani hayasumbui!
Pole SANA kwa wahusika! Daah
Hawa watu hawapo kwenye hii kitu ya usafirishaji na hawaelewi chichote kuhusu magari. Ndiyo sababu walio wengi hununua magari kwa namba za usajiri. Gari ikishakuwa namba D hana tena uelewa wa kuchunguza mambo mengine.
 
Back
Top Bottom