Songwe: Basi la Kampuni ya Kilimanjaro Express lapata ajali, watu wanne wafariki dunia

Songwe: Basi la Kampuni ya Kilimanjaro Express lapata ajali, watu wanne wafariki dunia

Acha mambo ya kuhisi hisi. Kampuni ina bus mengi tu ya kuagiza ambayo hata kampuni zingine zinaota kuyamiliki. View attachment 2149819
Mabasi original yatakuwa machache sio nahisi, mimi mwenyewe zama za kale in my early 20’s wakati naishi UK ndio nilikuwa nampeleka Sawaya kununua hizo 7.5 tonnes za mizigo anazogeuza mabasi, ma lorry yake ya masafa ya marefu, parts za magari yake hasa engines za Scania na tankers zake (ambazo nyingi wanazoleta huku, ulaya wanapotoa wanabebea maziwa, ndio maana zikianguka mafuta yanamwagika) tanker la mafuta lina bei na ngumu mafuta kumwagika ata likipinduka.

So naelewa ninachokisema
 
Magari yenyewe mengi ya Kilimanjaro yalianza maisha kama LGV trucks huko anaponunua Sawaya akishayaleta bongo anayabadili kuwa mabasi na body anaunga mwenyewe.

Sasa upande basi kama hilo ambalo lipo zaidi ya 10 barabarani na njia zetu hizi; si suicide mission hiyo. Huu utaratibu wa kununua LGV na kuyageuza mabasi na wenyewe ushapitwa na wakati, sidhani kama Kilimanjaro wana bus ambalo lilinuliwa original likiwa basi.
Marcopolo za kilimanjaro hazijawa modified. Unless unaongelea mawazo yako binafsi
 
Mkuu,
Alhamis wiki iliyopita nilipanda kimotco mida ya Saa nane kasoro mchana, (nadhani ile inayotoka arusha), kutoka Dodoma kuelekea Iringa, abiria wenzangu walikalia mabegi yao kwenye kile kikorido cha kupita, wengine walikalia zile "arm rest", na wengine kusimama kabisa, pia yule kondakta alikuwa anaenda siti za nyuma anawaomba wakae watu watatu katika siti zilizotengenezwa kwa ajili ya kukaa watu wawili tu(muundo wa siti za basi hilo ni 2 by 2(2*2)). Na Bado njiani waliendelea kuchukua raia/abiria.Wakati wa kukata tiketi ukiuliza siti zipo wanakwambia zipo za kutosha.

Katika "Traffic Stops" zote kutoka dodoma mpaka ninafika iringa hakuna polisi alieingia ndani ya basi. Mwana usalama pekee alieingia ndani ni afisa wa uhamiaji pale mtera basi.

Haya mambo yapo na yanaendelea.
Mjinga nani hapo Kati yako na konda?
 
Bus la kampuni ya Kilimanjaro limepinduka asububuhi hii mkoani Songwe likitokea Tunduma kuelekea Jijini Dar es salaam ambapo taarifa za awali zinaeleza ajali hiyo imesababisha watu kadhaa kufariki na uwepo wa majeruhi, taarifa kamili zitakujia hivi punde.

===================

Basi la Kampuni ya Kilimanjaro Express limepata ajali kwa kupinduka asubuhi ya leo Machi 14, 2022 Mkoani Songwe wakati likitokea Tunduma kuelekea Jijini Dar es Salaam.

Taarifa za awali za mashuhuda waliopo eneo la tukio zinaeleza ajali hiyo imesababisha watu kadhaa kufariki na uwepo wa majeruhi.

Ofisa Mmoja wa Kilimanjaro Express amekiri kutokea kwa ajali hiyo lakini hakuwa tayari kuelezea kiundani kwa madai siyo msemaji wa kampuni. Juhudi za kumpata RPC wa Songwe, Janeth Mgomi zinaendelea ili kupata ripoti kamili.

UPDATES;

Watu wanne wamefariki papo hapo huku wengine 26 wakijeruhiwa katika ajali ya basi la Kilimanjaro Express lililopindukia korongoni eneo la Senjele wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, Rashid Ngonyani amesema ajali hiyo imetokea saa moja asubuhi baada ya dereva wa basi la Kilimanjaro Express kuwa kwenye mwendokasi na kutaka kuyapita magari mengine yaliyokuwa mbele yake.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba amesema majeruhi wote 36 wanaendelea vizuri ambapo kati yao saba wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Mbeya na wengine 28 wakitibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe

View attachment 2149697
View attachment 2149696
View attachment 2149698

View attachment 2149968
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Maumba alimjulia hali miongoni kwa majeruhi wa ajali ya basi kampuni ya Kilimanjaro, Yusuph Ramadhan ambaye yeye na wenzake sita walikimbizwa katika Hospitali Teule ya Ifisi iliyoko mkoani Mbeya. PICHA: Grace Mwakalinga, SONGWE

View attachment 2149979
Hii gari ilikuwa na bima? Majeruhi wanatibiwa kwa Gharama ya bima au mwenye bus au Serikali?

Marehemu wanne nini kitaendelea kuhusu bima ?
Kuna tabia bus Linaua watu kila mtu anaondoka na mwili wa ndugu yake kwenda kijijini kuuzika hawarudi tena nyuma kuulizia au kuifuatilia bima.

Ninashauri TIRA itoe maelezo na maalekezo kwa abiri wanaotumia vyombo vya moto.
 
Ni kweli kabisa Aboud mabasi mabovu anayapeleka Mbeya na Tunduma!
Sasa nauli ikiwa kubwa hamtaki kulipa
Basi jipya huwezi peleka route ya wataka nauli ndogo hailipi

Basi la zamani linakuwa Walau pesa ilisharudi kupitia route fupi.Likichoka unapeleka route ndefu kwa wabahili waishie nalo

Mabasi mazuri route ndefu kubali kulipa nauli kubwa.Mbona yapo
 
Sasa nauli ikiwa kubwa hamtaki kulipa
Basi jipya huwezi peleka route ya wataka nauli ndogo hailipi

Basi la zamani linakuwa Walau pesa ilisharudi kupitia route fupi.Likichoka unapeleka route ndefu kwa wabahili waishie nalo

Mabasi mazuri route ndefu kubali kulipa nauli kubwa.Mbona yapo
Tunduma kuna visu vya uhakika.

Hiyo mbaula Kilimanjaro imepotea njia tu ilitakiwa iende Babati huko!
 
Siku hizi unakuta magari ya mikoani yamejaza hadi abiria wengine wamekalia vile vindoo vya dustbin na wala hawaogopi trafiki.

Sasa ikitokea ajali kama hii mtoa roho anaanza na wewe.
Yaani route kutoka sumbawanga to Tunduma Hadi dar mabasi hayana ustaarabu Hata kidogo hii tabia ya kupanga ndoo njiani kuanzia seat ya nyuma Hadi mbele nimeshangaa Sana aiseee.. gari linajaza Sana na trafik Hata wachukui hatua... Igeni mikoa ya Arusha na Moshi gari ikiwa level seat it's enough
 
Yaani route kutoka sumbawanga to Tunduma Hadi dar mabasi hayana ustaarabu Hata kidogo hii tabia ya kupanga ndoo njiani kuanzia seat ya nyuma Hadi mbele nimeshangaa Sana aiseee.. gari linajaza Sana na trafik Hata wachukui hatua... Igeni mikoa ya Arusha na Moshi gari ikiwa level seat it's enough
Mkuu.
Route ya DAR ARUSHA, ni habari nyingine. Hata DOM DAR DOM wanaionea wivu
 
Back
Top Bottom