Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Dkt. Magufuli anaendelea na kampeni mkoa wa Songwe na sasa yuko Tunduma.
MAGUFULI: Ninafamu kuna kero moja kwa kinamama inaitwa kampeni ya mama kamandoo ambapo wamama wanapochelewa kwenda kliniki wanatozwa 50,000. Naifuta leo moja kwa moja hiyo tozo.
Kwa hiyo pasitokee mtu yoyote kutoka wizara ya afya au mahali popote anawatoza kina mama hawa wajawazito ati kwa sababu wamechelewa kliniki, kumtoza elfu hamsini ni kumuonea mwanamama huyu ambae anahangaika miezi tisa tumboni.
Kwa hio kina mama pateni mimba zenu, nendeni mkajifungue sawasawa. Wewe mama umemuona ni mjamzito, wewe unaenda kumtoza elfu hamsini, ulimpa wewe mimba?
Kamandoo aende shambani akalime au afanye biashara nyingine. Mtu unachelewa kwenda kliniki unatozwa elfu hamsini wakati mikoa mingine hawatozwi. Hili nasema hapana kwa hio marufuku kuanzia leo.
Nilileteeni Silinde, alikuwa CHADEMA kwenye jimbo la Momba, alipokuwa kule CHADEMA alijua uozo uliomo humo akawa kila mara anabembeleza, anasema baba nimechoka niko radhi nipoteze ubunge lakini nihamie CCM hata kama nitakuwa karani, nikamshangaa kijana huyu ambae alikuwa yuko radhi apoteze mishahara na fedha za ubunge kwa ajili ya maslahi ya watu.
Alichaguliwa na wabunge wa CCM kuwakilisha katika bunge la Afrika, kijana mdogo jasiri aliye na upendo wa kweli. Alikuwa agombee Momba, nikamwambia nenda kanisaidie Tunduma kwa sababu ndio pana changamoto nyingi kubwa.
Nileteeni Silinde alafu mje mniulize maji ya hapa na ukweli nimeshaanza kuipanga hiyo miradi, tunataka tuyatoe maji Ileje yateremke mpaka hapa Tunduma, mtakunywa mpaka mtachoka.
Lakini msinichanganyie, mkiniletea hao, nasema maji hamyapati. Lazima tuambizane ukweli na mimi nazungumzaga ukweli.