Uchaguzi 2020 Songwe: Dkt. Magufuli afanya kampeni Tunduma, afuta tozo ya mama kamandoo

Jamani hivi hizi ahadi na maamuzi ndani ya kipindi cha kampeni sio rushwa??NEC Njooni msikilize mzee baba mmemkaza Lissu lakini huyu bado hana namna anaona asipofanya hivyo maji yamezidi unga 😀😀

Kila mwasiasa unaemjua ni MSANII.

kuhusu rushwa ni bahati mbaya kiswahili kina upungufu sana wa neno sahihi. kwa kiingereza kwa kuwa yeye ni incumbent President na maamuzi yake ni ya mwisho, anakuwa akitoa inaitwa sleaze.

Sababu yeye kama head of state anaitwa Conforter in chief. na ndio severeignty. ( kwa mkuu wa Nchi ni sio kwa Mkuu wa serikali)

Anatakiwa ku confort raia wake, kwa kipindi hichi sio hairuhusiwe kupenda watu wake, hali hii haipendezi, sasa inapunguzwa makali wanaiita sleaze.
 
Dkt. Magufuli anaendelea na kampeni mkoa wa Songwe na sasa yuko Tunduma.

MAGUFULI: Ninafamu kuna kero moja kwa kinamama inaitwa kampeni ya mama kamandoo ambapo wamama wanapochelewa kwenda kliniki wanatozwa 50,000. Naifuta leo moja kwa moja hiyo tozo.

Kwa hiyo pasitokee mtu yoyote kutoka wizara ya afya au mahali popote anawatoza kina mama hawa wajawazito ati kwa sababu wamechelewa kliniki, kumtoza elfu hamsini ni kumuonea mwanamama huyu ambae anahangaika miezi tisa tumboni.

Kwa hio kina mama pateni mimba zenu, nendeni mkajifungue sawasawa. Wewe mama umemuona ni mjamzito, wewe unaenda kumtoza elfu hamsini, ulimpa wewe mimba?

Kamandoo aende shambani akalime au afanye biashara nyingine. Mtu unachelewa kwenda kliniki unatozwa elfu hamsini wakati mikoa mingine hawatozwi. Hili nasema hapana kwa hio marufuku kuanzia leo.

Nilileteeni Silinde, alikuwa CHADEMA kwenye jimbo la Momba, alipokuwa kule CHADEMA alijua uozo uliomo humo akawa kila mara anabembeleza, anasema baba nimechoka niko radhi nipoteze ubunge lakini nihamie CCM hata kama nitakuwa karani, nikamshangaa kijana huyu ambae alikuwa yuko radhi apoteze mishahara na fedha za ubunge kwa ajili ya maslahi ya watu.

Alichaguliwa na wabunge wa CCM kuwakilisha katika bunge la Afrika, kijana mdogo jasiri aliye na upendo wa kweli. Alikuwa agombee Momba, nikamwambia nenda kanisaidie Tunduma kwa sababu ndio pana changamoto nyingi kubwa.

Nileteeni Silinde alafu mje mniulize maji ya hapa na ukweli nimeshaanza kuipanga hiyo miradi, tunataka tuyatoe maji Ileje yateremke mpaka hapa Tunduma, mtakunywa mpaka mtachoka.

Lakini msinichanganyie, mkiniletea hao, nasema maji hamyapati. Lazima tuambizane ukweli na mimi nazungumzaga ukweli.

Kutisha wananchi kwamba hutawapelekea maendeleo kisa wamechagua wapinzani ni kiburi na dhihaka kwa wananchi. Wananchi tunalipa kodi na kama anataka hivyo na kodi zetu asichukue, atumie michango na mapato ya CCM..
 
Hivi huyu mzee yupo timamu kweli? Yani anasemaje????? Au kachanganyikiwa huyu, yani kuwa na Magorofa aneishajiona kuwa anaweza piga watu Kwa kuwa wamemnyima kura? Khaaaa amedalilika Sana tumuombeee hayuko sawa kichwani
 
Kaongea haya akiwa kama MGOMBEA ama RAIS there should be a line
Katiba mbovu mru anaingia kwenye kampen akiwa bdo ni rais nch za wenzetu chaguz zikifika rais na mawazir wanapunguzwa madaraka na hawaruhusiw kwenda kwenye kampen na vyeo vyao
 
Dr Magufuli amesema mara ya mwisho alipokuja Tunduma wafuasi wa Chadema walimshangilia sana na hiyo inamaanisha kuwa maendeleo hayana vyama.

Magufuli amesema Silinde alikuwa anambembeleza toka akiwa Chadema kwamba anaomba ahamie CCM hata kama atapoteza ubunge.

Silinde alikuwa agombee Momba lakini nikamwelekeza agombee Tunduma kwa sababu kuna changamoto nyingi amesema Dr Magufuli.

Maendeleo hayana vyama!
Uongo...mchana kweupe.
 
Kutisha wananchi kwamba hutawapelekea maendeleo kisa wamechagua wapinzani ni kiburi na dhihaka kwa wananchi. Wananchi tunalipa kodi na kama anataka hivyo na kodi zetu asichukue, atumie michango na mapato ya CCM..
Electoral politics/voting meaning: is a set of activities that are associated with making decision for distribution of resources and status.
 
Dkt. Magufuli anaendelea na kampeni mkoa wa Songwe na sasa yuko Tunduma.

MAGUFULI: Ninafamu kuna kero moja kwa kinamama inaitwa kampeni ya mama kamandoo ambapo wamama wanapochelewa kwenda kliniki wanatozwa 50,000. Naifuta leo moja kwa moja hiyo tozo.

Kwa hiyo pasitokee mtu yoyote kutoka wizara ya afya au mahali popote anawatoza kina mama hawa wajawazito ati kwa sababu wamechelewa kliniki, kumtoza elfu hamsini ni kumuonea mwanamama huyu ambae anahangaika miezi tisa tumboni.

Kwa hio kina mama pateni mimba zenu, nendeni mkajifungue sawasawa. Wewe mama umemuona ni mjamzito, wewe unaenda kumtoza elfu hamsini, ulimpa wewe mimba?

Kamandoo aende shambani akalime au afanye biashara nyingine. Mtu unachelewa kwenda kliniki unatozwa elfu hamsini wakati mikoa mingine hawatozwi. Hili nasema hapana kwa hio marufuku kuanzia leo.

Nilileteeni Silinde, alikuwa CHADEMA kwenye jimbo la Momba, alipokuwa kule CHADEMA alijua uozo uliomo humo akawa kila mara anabembeleza, anasema baba nimechoka niko radhi nipoteze ubunge lakini nihamie CCM hata kama nitakuwa karani, nikamshangaa kijana huyu ambae alikuwa yuko radhi apoteze mishahara na fedha za ubunge kwa ajili ya maslahi ya watu.

Alichaguliwa na wabunge wa CCM kuwakilisha katika bunge la Afrika, kijana mdogo jasiri aliye na upendo wa kweli. Alikuwa agombee Momba, nikamwambia nenda kanisaidie Tunduma kwa sababu ndio pana changamoto nyingi kubwa.

Nileteeni Silinde alafu mje mniulize maji ya hapa na ukweli nimeshaanza kuipanga hiyo miradi, tunataka tuyatoe maji Ileje yateremke mpaka hapa Tunduma, mtakunywa mpaka mtachoka.

Lakini msinichanganyie, mkiniletea hao, nasema maji hamyapati. Lazima tuambizane ukweli na mimi nazungumzaga ukweli.

Alikuwa agombee Momba, nikamwambia nenda kanisaidie Tunduma kwa sababu ndio pana changamoto nyingi kubwa!

Si alisema hajamtuma mtu!
 
JPM wakati anapambana na Lowassa alipiga push-ups nyingi mara kadhaa, ulifahamu maana yake? Dhihaka kwa Lowassa kuhusu afya yake. Rhetorical language.

Wakati huu anapambana na amepigishwa magoti mara mbili akiomba kura, unajua maana yake??

Mataga Tafuta thamani ya X......
Maana yake ni nini...?
 
nasubiria lissu atoneshe kidonda cha mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

magufuli: mimi bado ni raisi na kuanzia leo wanafunzi wote hawatalipia mikopo yao.

kutekenywa ukatekenyeka
Hahahaaaa ngoja wamguse kunako
 
Rais Magufuli amesema hivi ''Najua viongozi wa Serikali mnanisikia, Wizara ya Afya mnanisikia na mimi mpaka leo bado ni Rais. Kampeni ya Mama Kamandoo ni marufuku kuanzia leo, kwa hiyo wakina mama bebeni mimba zenu vizuri tuongeze idadi ya Watanzania''

Dkt. Magufuli ameongeza kuwa ''Kuna malalamiko dhidi ya kampeni ya Mama Kamandoo kuwatoza wanawake wajawazito wanaochelewa kujiandikisha kliniki Tsh. 50,00. Hii kampeni naifuta leo, kwahiyo Mama Kamandoo aende shambani akalime Mahindi aachane na tabia ya kutoza kinamama''
Siku zote alikuwa hajui amesubiri lisu aseme ndio afute amechelewa sana
 
Dr Magufuli amesema mara ya mwisho alipokuja Tunduma wafuasi wa Chadema walimshangilia sana na hiyo inamaanisha kuwa maendeleo hayana vyama.

Magufuli amesema Silinde alikuwa anambembeleza toka akiwa Chadema kwamba anaomba ahamie CCM hata kama atapoteza ubunge.

Silinde alikuwa agombee Momba lakini nikamwelekeza agombee Tunduma kwa sababu kuna changamoto nyingi amesema Dr Magufuli.

Maendeleo hayana vyama!

..anaanza hotuba zake kwa kusema maendeleo hayana vyama.

..halafu anamaliza kwa kusema wananchi wakichagua mpinzani atawanyima miradi ya maendeleo.
 
Dkt. Magufuli anaendelea na kampeni mkoa wa Songwe na sasa yuko Tunduma.

MAGUFULI: Ninafamu kuna kero moja kwa kinamama inaitwa kampeni ya mama kamandoo ambapo wamama wanapochelewa kwenda kliniki wanatozwa 50,000. Naifuta leo moja kwa moja hiyo tozo.

Kwa hiyo pasitokee mtu yoyote kutoka wizara ya afya au mahali popote anawatoza kina mama hawa wajawazito ati kwa sababu wamechelewa kliniki, kumtoza elfu hamsini ni kumuonea mwanamama huyu ambae anahangaika miezi tisa tumboni.

Kwa hio kina mama pateni mimba zenu, nendeni mkajifungue sawasawa. Wewe mama umemuona ni mjamzito, wewe unaenda kumtoza elfu hamsini, ulimpa wewe mimba?

Kamandoo aende shambani akalime au afanye biashara nyingine. Mtu unachelewa kwenda kliniki unatozwa elfu hamsini wakati mikoa mingine hawatozwi. Hili nasema hapana kwa hio marufuku kuanzia leo.

Nilileteeni Silinde, alikuwa CHADEMA kwenye jimbo la Momba, alipokuwa kule CHADEMA alijua uozo uliomo humo akawa kila mara anabembeleza, anasema baba nimechoka niko radhi nipoteze ubunge lakini nihamie CCM hata kama nitakuwa karani, nikamshangaa kijana huyu ambae alikuwa yuko radhi apoteze mishahara na fedha za ubunge kwa ajili ya maslahi ya watu.

Alichaguliwa na wabunge wa CCM kuwakilisha katika bunge la Afrika, kijana mdogo jasiri aliye na upendo wa kweli. Alikuwa agombee Momba, nikamwambia nenda kanisaidie Tunduma kwa sababu ndio pana changamoto nyingi kubwa.

Nileteeni Silinde alafu mje mniulize maji ya hapa na ukweli nimeshaanza kuipanga hiyo miradi, tunataka tuyatoe maji Ileje yateremke mpaka hapa Tunduma, mtakunywa mpaka mtachoka.

Lakini msinichanganyie, mkiniletea hao, nasema maji hamyapati. Lazima tuambizane ukweli na mimi nazungumzaga ukweli.

Watanzania msiwe wajinga.
Miaka mitano aliyokaa madarakani hakujua kwamba kuna hiyo tozo?
Hapo ninapo waona Watanzania wenzangu hatujitambui. Hiyo ni hongo kama ya t shirt na. Kofia.. Halafu akipata kura ina rudi kishkaji
 
Back
Top Bottom