Soon nakuwa mama wa kambo. Nahitaji maombi yenu na ushauri wa maisha haya mapya

Ohoo! ni wa kike! kwahiyo ndio kusema hatanipenda! hahahhaa. Ukweli mume wangu ananipenda na anijali. Mtoto nampokea kwa roho nyeupe tu haina shida. Nilitaka kujifunza zaidi ili itakapofika muda niwe nimeshajifunza kama yapo ya kujifunza na ya kufanyia kazi
 
Kama unaroho mbaya basi utakuwa na wasiwasi kwani si anakuja kukaa kama wengine wanavokaa mbona unaanalyse vitu ambavyo havina umuhimu,nadhani utakuwa mbaguzi tuu
Sio mbaguzi ila maandalizi lazima yawepo. Unaweza kuchukulia kitu easy kumbe sio unavyofikiria. Ndio maana nikashea wajameni.
 
Asante sana kwa ushauri. Nimekuelewa vilivyo
 
Ushauri nimechukua. Amejibu kwa ufasaha na kistarabu sana. Kuna wengine wanakazana mimi sijui mchoyo, mbinafsi, sijui ndezi jamani Khaaa!
 
Bond watu wanatemgeneza tu, huwa hakuna wakati ambao mtu hudhamiria kufanya hivyo...

Mbona sisi tusiojuana hata kwa sura let say mi na Joanah , tumekutana tu kijiwe cha JF na unapata tume bond vizuri wakati hata sijui ako anafanana aje...

Wanadamu huwa tuna sifa moja, tumeumbwa/undwa kukutana na vitu vipya na kuvi own...

Ukiona li mtu lina mihasira hasira ujue kachagua kuwa hivyo, ukiona mtu mwenye roho nzuri naye halikadhalika kachagua kuwa hivyo...
 
Mtoto ni wake yet mimi tena nimsisitizie aje likizo! naamini ilikuwa ni jukumu lake na hakuwahi kufanya hivyo. Yaan yeye alitakiwa awe mstari wa mbele. Mtoto sio wangu halafu ningeanzaje kusisitiza? Alitakiwa ajiongeze kwahiyo sidhani kama ilikuwa kosa langu. Mwanzoni kabisa baada ya kuniambia kuna mtoto niliimwambia amlete but akasema hataishi na sisi. Sikuona sababu ya kumlazimisha. Sasa baada ya miaka 10+ ndio anataka amlete na mimi sina shida na hilo. Nilitaka tu kupata mawili matatu kutoka hapa jamvini. Si unajua penye wengi pana mengi. Maisha ni funzo na kujifunza ni kitu endelevu
 
Ondoa hio negativity ya u mama wakambo kwanza! Pia utajaribu kuwa nae karibu kumjali kama mwanao wakumzaa japo kuna watoto wengine humezeshwa sumu na mamazao hata uwapende vipi! Mungu akusaidie mpatane
 
Ni kwa "NEEMA" tu [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Sema wanawake saa zngne mnaakili ndogo sana mm nililelewa Na mama wa kambo wawili tofauti huyo wa kwanza alinilea kama mwanae baadae akaachana na mzee akaja huyu funga kazi roho mbaya chuki na alipandikiza sumu hadi mshua akawa hanipendi kabsa kabsa lakini sikuhizi japokua sina maisha mazuri kvle naona anajifanya kunipenda kumbe unafki tu shenz kabsa.
 
Unataka amtupe? Je angekuwa wako ungetaka amuweke wapi? Ni suala la busara na kutokuwa mbinafsi na mjinga kumkataa mtoto wa mwenzio.
 
Pole sana! maana kulelewa na mama wa kambo wawili hiyo nayo kali. Well mimi akili yangu sio ndogo lakini hahaha! Ila mimi naamini kukaa na mtoto akiwa mdogo inakuwa rahisi. Wengine wakishakuwa wakubwa nao wanaweza kuwa na perception zao kwamba mama wa kambo labda ni hivi na hivi anajikoki kabisa maana jamii nayo haichukulii mama wa kambo kama mtu poa. Wameshaweka ni wabaya tu wengi wanavyofikiria. Mimi niko poa tu sina shida. Inategemea sasa na mtoto mwenyewe atakavyonichukulia
 
Unataka amtupe? Je angekuwa wako ungetaka amuweke wapi? Ni suala la busara na kutokuwa mbinafsi na mjinga kumkataa mtoto wa mwenzio.
Hamna sehemu nimesema nimekataa mtoto wala kusema amtupe. Soma vizuri jamani.
 
Maneno yamekua meeeng...inshort ni hiv..maisha yako wont be the same no more...hvyo yan.....man rule the world remember
 
Maneno yamekua meeeng...inshort ni hiv..maisha yako wont be the same no more...hvyo yan.....man rule the world remember
Sijaelewa vizuri mkuu. Sasa hapo man rule the world na nini inakujaje tena wakati mambo ni maelewano. Manake ni suala la mahusiano hapa na sio siasa or anything
 
Walikuwa wanapima tabia yako wamejiridhisha hawana shaka nayo thus walichelewa.Mpokee mwa moyo mweupe show love usimbague hakuna ajuae kesho yake nani atakulea
 
Mtendee wema kesho yako uijui hata watoto wako wanaweza kuja lelewa na mama wa kambo ya kesho atuyyajui kama ambavyo Sabaya na bashite awakutegemea kuwa raia wa kawaida leo.
 
Mtoto hakuletwa mapema kutokana na reaction yako siku umeambiwa mmeo ana mtoto. Mmeo alifanya hivyo kuinisuru ndoa yenu.
Sasa amejua una uwezo wa kuishi nae ndiyo maana anamleta.
Wewe cha kufanya acha kujipa umama wa kambo ule wa kiibilisi bali jipe umama. Hujui ya baadae kwani hata watoto wako wanaweza kuja lelewa na mama wa kambo.
Hivyo mtendee huyo mtoto vile ambavyo ungependa mama wa kambo wa wanao aje watendea watoto wako.[emoji120]
 
Sasa upendo haulazimishwi, hiyo inategemeana na roho yako ilivyoumbwa. Huwezi chagua umpende nani na nani usimpende. Ila kumpa mtu haki yake hilo ni suala la uchaguzi na usipochagua kutoa haki ni kinyume cha maadili na sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…