Mkuu hii ni hatari sijui nchi hii inaelekea wapi. Nimeona mwenyekiti wa CCM wakati anafungua mkutano wa leo amesema maneno ambayo yanaonyesha kuwahukumu baadhi ya wanachama kabla hata mkutano haujaanza. Kwa hiyo kama (Mh. Humphrey Harakaharaka) anasema "Kikao kwa sauti moja............kimeamua" sijua inakuwaje. Wakati inaonyesha mwenyekiti alikuwa ameshaelekeza hukumu. Hivyo inaonyesha wajumbe walifata amri tu. Na hivi wanaogopa kupunguzwa kesho hiyo ndiyo kabisa. Sasa kuna chama gani kinafaa mkuu? Chadema kuna wababe pia Zitto alitimuliwa, na CUF ndiyo balaa kabisa bora hata hao waliofukuzwa CCM nafikiri watakubali kwa shingo upande. Lakini walifukuzwa CUF wamekataa kuondoka, wameng'ang'ana na mpaka sasa wanaendesha chama kibabe. Na mpaka ruzuku wanaendelea kuchukua. Duh siyo mchezo!