Soseji zapigwa marufuku nchini Korea Kaskazini!

Soseji zapigwa marufuku nchini Korea Kaskazini!

Hivi hakuna raia anaweza akajitoa ufahamu akamla kichwa?
Ujamaa ni mfumo wa utawala unaomfanya kiongozi wa juu aonekane mkubwa kupita kiasi.

Nchi za kijamaa Serikali ina fedha ila raia ni makapuku.


Wananchi wa kawaida wanatabika mno huku watawala wakiwatenda watakavyo bila kuhojiwa.
Mwl. Nyerere katika kuunda Mfumo wa Utawala wa CCM pamoja na Mfumo wa Utawala wa Serikali katika nchi hii ya Tanzania aliiga Mifumo ya Utawala kutoka Korea ya Kaskazini, China na Urusi (USSR).

Watanzania na raia wa China, Urusi au Korea ya Kaskazini kamwe hatuwezi kuchekana, Wananchi wote katika nchi hizi ni MATEKA WA WATAWALA.
 
Si waliue, kuna watu wanafanya wenzao waishi kwa tabu sana hapa duniani
Mpangilio wa ulinzi binafsi unamfanya awe salama.

Analindwa na watu waliochujwa kwa vetting kali na maisha ya walinzi hao ni ya upendeleo, ni ngumu kumgeuka.

Askari kanzu kila kona, ukimsema vibaya leo, kesho unatafutwa na usijue nani aliyekuchoma!

Watawala wa taifa hilo ni wafalme madikteta wanaoishi kama marais kwa maisha ya anasa.
 
Unaponunua nyama safarini huwa unajuaje ni ya mbuzi kweli na sio mbwa, ni ng'ombe sio panda au ni kuku sio kunguru??
Mambo ya vyakula ni magumu sana sahivi kila chakula kikiwa shambani ni genetic modified na vinapigwa madawa sana
 
Tuliza akili na kuwa makini, feinberg ndyo alifanya mahojiano na rabbi, kisha akawasilisha hiyo taarifa
Leta hapa link ya YouTube ya mahojiano, leta hapa picha ya huyo rabi wako.
 
Huwa sina utaratibu wa kula vyakula vigumu nikiwa safarini
Wenye utaratibu wa kula vyakula vigumu wakiwa safarini wafanye nini kujiridhisha nyama wanazokula sio za punda, mbwa au kunguru??
 
Mwl. Nyerere katika kuunda Mfumo wa Utawala wa CCM pamoja na Mfumo wa Utawala wa Serikali katika nchi hii ya Tanzania aliiga Mifumo ya Utawala kutoka Korea ya Kaskazini, China na Urusi (USSR).

Watanzania na raia wa China, Urusi au Korea ya Kaskazini hatuwezi kuchekana, Wananchi wote katika nchi hizi ni MATEKA WA WATAWALA.
Ila Tanganyika tuna ahueni kidogo baada ya USA kuingiza Ubepari kidogo kwenye mfumo wetu.

Ila Nyerere alitujengea misingi ya kuwa kondoo, tusihoji wala kuuliza chochote.
 
Unaponunua nyama safarini huwa unajuaje ni ya mbuzi kweli na sio mbwa, ni ng'ombe sio panda au ni kuku sio kunguru??
Vyakula haramu ni vya kufikirika zaidi kuliko uhalisia.

Kwa mfano hoteli za njiani tunamopita kusimama kula, tuwe tunalishwa vyakula haramu na asipatikane mtu hata mmoja wa kushitukia?

Je mifugo mingi namna hiyo ya kuchinja kila siku kama ni mbwa na paka, ni wapi huko inafugwa kutosha kukidhi soko?

Kama kuku tunaokula wawe ni kunguru na mwewe, ni wapi huko wanakokusanywa kila siku kwa kiwango hicho, waijua kazi ya kuwinda ilivyo ngumu na ya kubahatisha?

Viungo vya ndege wa pori na kuku vinafanana?

Mkuu, cha kujadili hapa ni namna ya uandaaji wake na ubora wa vyakula ndiyo waweza kuwa na kasoro, maana vyakula hivyo huwa lazima viuzwe na kwisha bila kujali vinakaa siku ngapi kabla ya kuuzwa na huwa havimwagwi.
 
Back
Top Bottom