Kama wamejiandaa inakuaje maambukizi yafikie 40+ rwanda?
ww ungesema wanatumia nguvu kubwa mno kujihami mpka polisi wanapiga watu risasi ,inatisha na kuogopesha
Waafrika hatuamini kuwa huo ugonjwa unaweza kuwa ni tatizo kwetu na huu ni mtazamo wa raia wenyewe hadi viongozi,hizi jitihada ni tunazoziona ni za kuondoa lawama tu.
Mkuu hapo Rwanda watu wamekula shaba,Kenya wanatandikwa bakora na India polisi wanakula kichapo kutoka kwa raia.Ukisema waafrika si sawa. Rwanda, South Africa, Uganda, Kenya na nchi nyingi tu wanapambana na huu ugonjwa. Nadhani tatizo ni Tanzania peke yake.
India zaidi ya bilioni 1 wapo lockdown na wanasema hamna kuiondoa:
Why India cannot afford to lift its lockdown
Nadhani tuna matatizo ya elimu zaidi kama anavyotambua TWAWEZA.
Mkuu hapo Rwanda watu wamekula shaba,Kenya wanatandikwa bakora na India polisi wanakula kichapo kutoka kwa raia.
Suala la dini limeingiaje tena hapa?Huko ndiyo kudhamiria kumalizana na Corona. Hili suala tunalifanyia sana lelemama.
Tumesahau kuwa taifa halina dini bali wenye dini zao ni wananchi.
Tafadhalini jamani dini bakini nazo kibinafsi mnatukera wengine ambao hatukubaliani na misimamo ya dini zenu.
Suala la dini limeingiaje tena hapa?
Hata hivyo mkuu hilo jambo mmelichukulia tofauti sana ila hikuwa na maana ya kwamba watu wasifanye kitu bali wategemee Mungu,mbona mashule yamefungwa na hatua mbalimbali zimechukuliwa kwa kiasi chake katika kuonesha nasi tunapambana na corona.Mkuu pale ilikuwa katika kudadavua zaidi.
Tofauti yetu na wote waliodhamiria kupambana na sisi iko kwenye wenzetu kutumia raslimali zao na sisi ati kumkabidhi Mungu.
Ilikuwa katika kudadavua zaidi tu.
Tuko pamoja mkuu.
Hata hivyo mkuu hilo jambo mmelichukulia tofauti sana ila hikuwa na maana ya kwamba watu wasifanye kitu bali wategemee Mungu,mbona mashule yamefungwa na hatua mbalimbali zimechukuliwa kwa kiasi chake katika kuonesha nasi tunapambana na corona.
Ndiyo maana nikasema viongozi na raia kwa afrika wanaamini huu ugonjwa ni wa watu weupe na hizi juhudi tunazoona ni kwa ajiri ya kuonekana tu nasi tunaunga mkono hii vita ya corona.Mkuu huu ugonjwa hautaki nusu. You do or you die.
Shule zimefungwa hatua njema. Masoko wazi, ibada wazi, usafiri wa umma wazi, maisha mengine yanaendelea. Pana Tina hapo?
Wanaita kisebu sebu na kiroho papo.