China imeweka wazi kuwa haitahudhuria mkutano wa Ukraine Peace Conference utakaofanywa nchini Switzerland June 15-16, 2024

Wajumbe 160 wamealikwa kwenye mkutano huo kutoka nchi za G7, G20 na BRICS. Lakini Russia haikualikwa.

Sababu ya China kukataa kuhudhuria mkutano huo ni kutoalikwa kwa Russia.

Wanadiplomasia wa China wanasema ikiwa Russia wangealikwa kwenye mkutano huo basi kungekuwa na ushiriki sawa wa pande zote na majadiliano ya haki.
 
Maandamano ya amani huko Budapest, Hungary makumi ya maelfu wakiandamana kupinga ushiriki wa NATO katika vita hivyo.

Harakati za amani zinazokataa kuwa "silaha ni njia ya amani" na badala yake zinataka kurejea kwa diplomasia na mazungumzo.

 
Alichosema Zelensky kwenye Shangri-La Dialogue nchini Singapore

Zelensky: "Xi Jinping aliniahidi China itasimama kando na haitaiunga mkono Urusi kwa silaha. Lakini, leo dalili kutoka kwa huduma za kijasusi, zikiwemo zetu kwamba kuna silaha zinaenda nchini Urusi kutoka China. Baadhi ya silaha zinatoka China."

Zelensky:
"Kwa sababu ya uungaji mkono wa China kwa Urusi, vita vitadumu kwa muda mrefu zaidi. Hii ni mbaya kwa ulimwengu wote."
 
Vipande vya kombora la Kimarekani la GMLRS lililorushwa na Jeshi la Ukraine vilivyopatikana katika eneo la Belgorod nchini Urusi baada ya kupokea kibali kutoka kwa Biden kutumia aina hizi za silaha kwenye maeneo ya Urusi.

Kwa sasa, Marekani bado haijaruhusu matumizi ya makombora ya masafa marefu ya ATACMS.

 
Time will tell
 
KABLA ya vita ilitakiwa Mr Zerensiky aingie google kutazama nafasi ya Urusi Kijeshi.
 
Umefika wakati inatakiwa hivi vita vya kijinga vimalizike sasa na dunia isonge mbele.
 
Huyu nae kunya anye Bata akinya kuku kahara yy mbna anaomba wazwaz anategemea nini?..kila mtu na washirika wake other wise wakae chini wayamalize kwa sababu n ndg.
 
NATO wslizingua kitambo kwa kumfunga mikono Ukraine. Tangu mwanzo walitakiwa kumpa silaha na kumuacha azitumie kwa uhuru.
 
Binafsi napenda sana vita,VITA INALETA HESHIMA NA AMANI YA KUDUMU, nilikuja gundua Demokrasia iliishashindwa. Ili kuweka mambo sawa inabidi wapigane kwanza, kisha tutafanya tathmini baadaye. Kwasasa kuzungumza kutafuta suluhu ni uongo, vita hiyo hai epukiki.

Cha msingi tujuzwe wanaanza lini kutwangana, tutapata shida lakini ikiisha tutatulia muda mrefu sana bila vita. Na ikiwa huu utakuwa mwanzo wa vita kubwa, basi na iwe, maana imeshaonekana hakuna suluhu, bora kuanza mapema tufahamu kuna vita.

Akishinda Russia, hakutatulia duniani itabidi tuhamishiwe Mars kwa muda mpaka hali itakapo kuwa shwari.
 
Kwanza Nashangaa Hivi Urusi inashindwa nini kumalizana na huyu Msanii halafu itulie kwanza mana yuko tu anajificha poland pale KGB imalizane nae kwanza
malengo ya SMO yalikua ni denazification na demilitarization,

ili ufikie malengo hayo unatakiwa kuwaondoa wanajeshi, sasa utawapunguzaje ukiamua kupiga vita vya kimaangamizi kama anavyofanya US?

mpk leo jeshi la ukraine lipo kwenye breaking point, wamekufa wanajeshi wengi mnoo kiasi saizi wanahangaika na kukamata wanaume wote waende jeshini, hii maana yake russia anafanikiwa ktk lengo lake la kuwamaliza wanajeshi wa ukraine (wear them down),

kwa sasa ni mercenaries wa nato ndio wapo kwa % kubwa,
 
Wao wa Rusia hawafi?

Ni kwamba West wanaenda kwa mahesabu katika hii vita. Kubwa zaidi ni kumdumaza Putin kiuchumi na hilo haliwezi kutokea kwa ghafla.
Subiri miaka 5 ijayo uone vilio kutoka kwa Putin.
a
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…