kuna nati zimelegea katika medula oblongata yako.
HIVI KWA NINI MAGUFULI ASIAPISHWE TU:
"Tanzania ya magufuli,itakuwa ni ya viwaaaandaaa"(In Magufuli voice).Huyu jamaa ni noma,kwanini asiapishwe tu,kuna sababu kweli ya kusubiri na kupiga kura hiyo tar 25??kwa hali hii naona mpinzani wake ameshadodaa.Ebu cheki bukoba leo hii:-
Dr. John Pombe Magufuli kwa sasa njia ya Ikulu iko wazi. Hii ni kutokana na mbinu anayotumia ya kuhutubia mikutano rasmi na isiyo rasmi akiwa njiani kuelekea kwenye mikutano ya kampeni. Anaongea na wapiga kura ana kwa ana kuliko mwenzake anayetumia chopa na kukutana na watu wachache mijini. Kwa tathmini hii Dr. Atapata ushindi wa asilimia zisizopungua 75 kwani na wanaupinzani wa kweli sasa wameanza kumkubali baada ya kuwa na imani naye na kumuona kuwa ni mkweli na ana nguvu na nia ya dhati ya kuleta maendeleo. Magufuli si mtu wa blaa blaa ni mchapakazi na ni mzalendo. Unasubiri nini ndugu yangu kuachana na viroba na kuwa na akili timamu nawe umchague mtu makini wa kukuvusha. Kinachonifurahisha hata mgombea wa tiketi ya Ukawa anamkubali Magufuli ndo mana anafanya kila mbinu kupunguza kura zake huku akijua kuwa ndiye rais wake ajaye. Hongera Magufuli kwa kushinda alfajiri.
Wewe gazeti hunywi viroba na uko vizuri. Hapa naongelea wanofuata mkumbo na kufikia kusema kuwa hata wakiwekewa jiwe na chama wanchokichukia watapigia jiwe. Watu wanamna hii ndo wanaoonekana kuwa kama wanywa viroba. Wewe nakufahamu ni mtu makini kabisa na najua kura yako baada ya kutafakari utampa Magufuli lakini hapa unazuga tu ili kuonyesha kuwa unakubaliana na wenzako. Twendelee kujenga hoja.Tatizo umejiunga maalumu kwa ajili ya propaganda tu, mbaya
zaidi ukasahau kuwa JF ina watu wanaofikiri sana haiwezekani
kwa mwanaJF mzoefu akamshawishi mtu kwa kumwambia UWE NA
AKILI TIMAMU UACHANE NA VIROBA, unamwitaje mtu ambaye umeanza
kumtukana?
Bila shaka wewe ni mnywaji mzuri wa GONGO.
Watu kama hawa bado hawajitambui nini wajibu wao. Wewe unasikia habari ya mjini ni Magufuli , afu wewe bado upo kwenye matumaini.