Umaarufu wa Edward Lowassa si wa leo wala jana, Edward Lowassa anafahamika vizuri si vijijini wala mjini, kutokana na jitihada zake pamoja na wazifa wake ndani ya chama alichokuwepo.
Magufuli ameibuka tu for a short time na kujikuta amefakamia/amefakamishwa sehemu ambayo hawezi kuimudu.
niwapongeze kamati ya mipango ndani ya Ccm kwa kulijua hili tangu mwanzo wa kampeni za mgombea huyu, kilichofanyika ni kuwa, kutokana na kutokujulikana/kuzidiwa umaarufu na Edward Lowassa, Ccm wameona ni heri wamkuze jina kidogo na wamemkuza kwa kutumia wasanii, watu ambao wamekuwa wakijaa kwenye majukwaa ni kwaajili ya kuwaangalia wasanii, na hapa ccm ndo wamekuwa wakitumia nafasi hii kumtangaza, vinginevyo wangekuwa wanatoka patupu.
Lakini ccm tusitegemee matunda yake tutayapata mwaka huu, unapopanda mti tarajia kupata matunda mwakani hivyo tumwandae MAGUFULI for the next time 2020 naamini atakuwa vizuri zaidi na atakuna na uwezekano mkubwa wa kushinda.
NAWASILISHA.