Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Nilifikiri niko mwenyewe... Kiukweli Joti nilikuwa nampenda sana na vitangazo vyake ila kwa sasa namchukia kupita maelezo..

Watu wa Marketing wa Tigo kaeni macho na hili..

Huko 0713 nako huenda yako majingajinga unadhani hayaoni? Kama hayaoni hayajasikia? Afya ya mtu na siasa wapi na wapi!
 
Mimi sinunui bando siku hizi. Napokea tu. Juzi wamenikopesha kinguvu nikalaani sana.
 
Huyu kijana anatumika pasipo kujua kwamba tuna msubiri akiugua. Wenzake wana kwenda kutumika kama kifaa cha majaribio ya dawa mpya India yeye tuna msubiri Muhimbili. Kila jambo lina wakati wake..Hatuwezi kuvumilia tabia za kipuuzi namna hii hapa nchini.
Msisababishe akajinyea!
 
Watu wakisema huenda tanzania imelaaniwa nahisi wana factual grounds kwa kutumia reference ya joti! hajui afanyalo!
 
Nimeona video nyingi sana za Orijino comedy kwenye msafara wa #HapaNiKaziTu wakidhihaki hali ya Lowassa.

Mwanzoni nilikuwa namsapoti Magufuli, lakini hawa kina Joti pamoja na maneno ya kina Nape ya kukejeli afya ya Lowassa yalinifanya kuwachukia CCM na kumwonea huruma Lowassa na kumfuata Ukawa.

Kwa jinsi muda unavyoenda nimejikuta na vutiwa sana na sera za Ukawa.

Zina malengo ya kuleta maendeleo na kujali utu wa watanzania wote, sio kama sera za CCM ambazo ni za maslahi ya wachahche.

Ndio maana hata Magufuli anaruhusu upuuzi kama wa Orijino comedy kwenye msafara wake.

Jinsi ninavyoona vituko na kejeli za kina Joti napata hasira sana. Hasira hii inatokea pia pale nionapo bango la Joti na Tigo barabarani, hata tangazo likitokea kwenye TV nabadilisha chanel.

Sinunui tena bundle za Tigo sababu wanasupport kina Joti
Tigo potezeeni endorsement ya kina Joti kabla hawajawaharibia image yenu kwa vijana wapenda Mabadiliko.
Nilidhani ni mimi tu kumbe tuko wengi !!
 
[h=3][/h] Aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la Sikonge, lakini akaanguka katika kura za maoni, Said Nkumba, akimnadi akimnadi Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo aliyeshinda, George Kagunda, wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgomba Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Tabora
​
Aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la Sikonge, lakini akaanguka katika kura za maoni, Said Nkumba, akimnadi akimnadi Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo aliyeshinda, George Kagunda, wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgomba Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Tabora

​
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavica) wilaya ya Igunga, Anuari Kashaga akiisasambua Chadema, wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgomba Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Tabora
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Tabora
​
Mdau akiperuzi mtandao katika simu yake
​
Daudi Nteminyanda, aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la Tabora Kaskazini- Uyui, kwa tiketi ya Chadema, lakini baadaye Chama hicho kikamuengua na kumuweka Joseph Kidaha aliyehamia Chadema baadaya kushindwa katika kura za maoni, akiichana Chadema, na kudai ni wanafiki katika kila jambo, alipohutubia mkutano wa kampeni wa Mgomba Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika leo katika jimbo la Tabora Kaskazini mkoaniTabora
​
Mgombea Ubunge jimbo la Manonga, wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Seifu Gulamali, akisalimia wananchi akati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Tabora Kaskazini-Uyui mkoani Tabora.
​
Mgombea Ubunge jimbo la Urambo Magharibi, Margaret Sitta akiomba kura wakati wa mkutano wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika leo eneo la Usoke, katika jimbo hilo mkoani Tabora.
​
Aliyekuwa Katibu wa Chadema wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Obeid Balola akiichana Chadema wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Usoke jimbo la Urambo Magharibi mkoani Tabora
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihtubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo eneo la Usoke, katika jimbo la Urambo Magharibi mkoani Tabora
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Urambo Magharibi, Margaret Sitta katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo mkoani Tabora
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimkabidhi kitabu cha Ilani ya CCM, Mgombea Ubunge jimbo la Urambo Magharibi, Margaret Sitta katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo mkoani Tabora
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akikumbatiana na Mgombea Ubunge jimbo la Urambo Magharibi, Margaret Sitta baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo mkoani Tabora. PICHA NA BASHIR NKOROMO

 
Hawa watu wanajiita wachekeshaji ni majanga. Ivi mlishajiuliza kama kusingekuwa na wanawake wavaa madela na mawigi na kujipodoa sana hawa comedian wangekuwa wanachekeshaga kitu gani??

Ningekuwa mimi ndio ndio original comedy nisingejihusisha na siasa chafu kwa kiwango kile maana wanunuzi na wafuatiliaji wa kazi zao ni watu wa vyama vyote na wengine hawana vyama.
 
Wamesahau vengu hata hawez kusimama,alafu wanadhihaki kisa pesa itawatafuna.
 
Mbona Vengu wao ni mgonjwa na hakuna aliyewahi kuwadhihaki wala kuwakejel yani binadamu sisi ni wasahaulifu kweli....sawa asanten orijino komedi nyie ni wazima milele.
 
Thread nyingine bwana, nawewe unajisifia kwenu kwamba ni great thinker?
 
Mbona Vengu wao ni mgonjwa na hakuna aliyewahi kuwadhihaki wala kuwakejel yani binadamu sisi ni wasahaulifu kweli....sawa asanten orijino komedi nyie ni wazima milele.

Hawajifunzi kutoka kwa mwenzao Vengu maana alikua bingwa wa kumwigiza A.Mlema now ye ndo yupo kitandani.
 
Hawa watu wanajiita wachekeshaji ni majanga. Ivi mlishajiuliza kama kusingekuwa na wanawake wavaa madela na mawigi na kujipodoa sana hawa comedian wangekuwa wanachekeshaga kitu gani??

Ningekuwa mimi ndio ndio original comedy nisingejihusisha na siasa chafu kwa kiwango kile maana wanunuzi na wafuatiliaji wa kazi zao ni watu wa vyama vyote na wengine hawana vyama.

Hawajaenda skuli walee hawajui
 
Back
Top Bottom