Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Malori makubwa makubwa yamehusika hapo
Lakini kuweni wapole tupo njiani Tutawarudisha wote.
 
Ma CCM bhana cjui yakoje!!
Halafu haya yanayojidai mtaisoma namba hayajui hata huwa magufuli anaongea nini, kitu gani kinafanyika! Wao ni kupenda umbea umbea tu..
"Ama kweli kuielimisha mi Tanzania, ni sawa na kuielimisha mi wenda wazimu" ccm ccm kibwege -----.. Sijui inafurahi kuendelea kukatiwa umeme! Kulipa kodi kubwa ya bidhaa, nauli kupanda na thamani ya pesa kushuka!!!!!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

Kwahiyo Lowasa jangwan ndo aliongea nn?... Hiv hujui kwamba Richmond ndo imetufikisha hapa kwenye suala la umeme..... Tulieni dawa iwaingie.... Hapa kazi tu.... Ufisadi peleka ukawa
 
Ilani mnazijua au hizo ahadi ndiyo ilani ,maana watu wengine hats majina yenu amyajui.
 
yale mashati ya mistari ya kijani kwa njano,natafuta sana..
 
Ilani ya UKAWA imeandikwa kwenye moyo wa watanzania..........mabadiliko,mabadiliko,mabadiliko.
 
[h=3]DK MAGUFULI AKISHINDA URAIS AAHIDI SERIKALI KUJENGA RELI KUTOKA MTWARA HADI MBAMBA BAY RUVUMA, KUPUNGUZA BEI YA VIFAA VYA UJENZI[/h]



Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM kumnadi mgombea urais Dk John Magufuli wilayani Masasi leo. Dk Magufuli amesema kuwa CCM ikishinda Serikali itajenga Reli kuanzia Mtwara hadi Mbamba Bay Ruvuma

Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi katika mkutano wa kampeni mjini Masasi, mkoani Mtwara leo.



Mfuasi wa CCM akiwa amejichora usoni huku kidevuni akiwa aqmeandika jina la Mgombea Urais wa Tanzania kuptia CCM, Dk Magufuli.

Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akitoa ahadi mbalimbali za maendeleo endaqpo akichaguliwa

Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika leo wilayani Namtumbo, Ruvuma. Dk Magufuli alitangaza kwamba akichaguliwa atahakikisha vifaa vya ujenzi bei yake inashuka kupunguza kodik.

Dk Magufuli akionesha Ilani ya Uchaguzi kabla ya kumkabidhi Mgombea ubunge jimbo la Namtumbo. Injinia Edwin Ngonyani

Mama mkazi wa Kijiji cha Chomolo, wilayani Namtumbo, mkoani, akishangilia baada ya Dk Magufuli kutangaza kwamba akishinda urais kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne hawatolipa ada

Dk Magufuli akihutubia baada ya kuzuiwa na wananchi katika Kijiji cha Kilimasela wilayani Namtumbo, alipokuwa akienda kufanya kampeni Masasi mkoani Mtwara

Dk Magufuli akihutubia baada ya kuzuiwa na wananchi katika Kijiji cha Kilimasela wilayani Namtumbo, alipokuwa akienda kufanya kampeni Masasi mkoani Mtwara

Dk Magufuli akihutubia baada ya kuzuiwa na wananchi katika Kijiji cha Nandembo wilayani Tunduru, alipokuwa akienda kufanya kampeni Masasi mkoani Mtwara

Dk Magufuli akihutubia baada ya kuzuiwa na wananchi katika Kijiji cha Matemanga wilayani Tunduru.

Akina mama wakiwa karibu na mti wenye picha ya Mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli

WAFUASI WA ccm wakishangilia wakati Dk Magufuli akijinadi


Ni furaha iliyoje kwa Bibi kizee huyu baada ya kumuona Dk Magufuli wakati wa mkutano wa hadhara mjini Tunduru leo

Dk Magufuli akijinadi katika mkutano wa kampeni mjini Tunduru
Mrembo akiwa amejiremba ki ccm katika mkutano huo wa kampeni mjini Tunduru

Baadhi ya wananchi wakiwa juu ya ukuta ili wapate kumuona Dk Magufuli akihutubia mjini Tunduru

Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ramo Makani

Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli

Dk Magufuli akiwapongeza wafuasi wa CUF waliokihama chama hicho na kujiunga na CCM KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA MJINI TUNDURU

Mambo ya warembo wa ccm

Msafara wa Dk Magufuli ukiwasili katika Kijiji cha Ligunga, wilayani Nanyumbu, Mkoa wa Mtwara




Mwanafunzi akiwa akiparamia mti ili aweze kumuona Dk Magufuli
​

Dk Magufuli akihutubia wananchi waliomzuia katika Kijiji cha Michiga, wilayani Nanyumbu alipokuwa akienda Masasi kuendelea na kampeni​
 
[h=3]WAZEE SONGEA WAMUANGUKIA RAIS AJAYE[/h]

01.JPG

WAZEE wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wamemtaka mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu ujao kuwa endapo atachaguliwa kuwa rais wa nchi kwa awamu ya tano wazee wa Tanzania wanamuomba aone umuhimu kwa kutambua mahitaji yao na kuwasaidia changamoto walizonazo.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa baraza huru la wazee wa halmashauri ya manispaa ya songea Salum Mwale wakati akichangia mada kuhusu mahitaji na matarajio ya wazee wa Tanzania iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali linalowahudumia wazee (PADI) lenye makao makuu mjini songea kwenye mkutano uliowakutanisha wazee na waandishi wa habari.


Mwale alisema kuwa wazee kwa muda mrefu wamelitumikia Taifa la Tanzania katika sekta mbalimbali zilizo rasmi na zisizo rasmi na wamekuwa chimbuko kubwa na mhimili wa taifa la Tanzania wamekuwa wakitoa jasho jingi katika kuhakikisha kuwa taifa linasonga mbele lakini bado wanaendelea kutoa mchango wao kwa kujinyima sana hasa ikizingatiwa hali zao za kiuchumi ni mbaya sana.


Alisema kuwa ili kuhakikisha vijana wanapata elimu na maisha bora kwa lengo la kuboresha uchumi wa nchi kwa kizazi kijacho bado wazee wanaendelea kuuumia na serikali haionyeshi kuwasaidia kwa kuwapa pensheni.


Hivyo amemuomba rais ajaye wa serikali ya awamu ya tano kazi kubwa ya kwanza atayoanza kuifaanya ni vyema aangalie namna ya kuwasaidia wazee kwa kuhakikisha kuwa wanapatiwa pensheni ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa baadhi ya changaamoto wanazokabiliana nazo.


Kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye kituo cha kulelea wazee kilichopo eneo la Unangwa nje kidogo ya manispaa ya songea Edita Nchimbi ambaye ni mjumbe wa babraza huru la wazee wa manispaa ya songea alisema kuwa pensheni kwa wazee ni muhimu sana hivyo ni vyema serikali ijayo ikachukua jukumu la kuwatambua wazee wote hapa nchini kwa kuwapa huduma mbalimbali zikiwemo za matibabu kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali za serikali.


Kwa upande wake Daud Mpangala ambaye pia ni mjumbe wa baraza la wazee ameiomba serikali ya wamu ya tano itakapoanza kufanya kazi isikilize kilio cha wazee wanaohitaji kusaidiwa kupatiwa pensheni na huduma zingine tofauti na ilivyo sasa wazee wamekuwa wakikabiliana na changamoto nyingi kwa vile hawana uwezo kiuchumi.​
 
Back
Top Bottom