Mgombea uraisi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dr John Pombe Magufuli amewataka watanzania kudumisha na kulinda amani kwa kuwa palipo na amani ndip[o palipo na maendeleo ya kweli.
Dr Magufuli aliyasema hayo mjini Mtwara wakati akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wake wa kampeni kuwania kiti cha uraisi uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara jioni hii.
Alisema maendeleo ya kweli ya nchi yanategemea sana uwepo wa amani na na mshikamano hivyo kusisitiza watanzania kuilinda amani iliyopo kwa nguvu zote kwani amani ikkiponyoka si rahisi kuirejesha tena.
Dr Magufuli alisisitiza kwa kutolea mfano nchi ya Libya ambayo wananchi wake walikuwa na amani na maendeleo,lakini wakaamua kuanza vurugu na kumuua kiongozi wa nchi hiyo Muhamar Gadaf na kusababisha nchi hiyo kuingia kwenye vurugu kubwa ambayo hadi sasa Libya hapakaliki.
Sasa hivi wananchi wa Libya wanakimbia nchi yao kwa kukimbilia Ulaya,na wako tayari kufia majini kuliko kukaa nchini mwao alisisitiza Dr magufuli.
Aidha Mgombea huyo wa uraisi kupitia CCM amewaomba watanzania kumpa kura aweze kuwa raisi wa awamu ya tano na kuahidi kwamba katika kipindi chake cha uraisi atawatumikia watanzania bila kujali itikadi za vyama,dini,kabila wala kabila la mtu kani watanzania wote ni sawa.
Serikali nitakayoiunda nikifanikiwa kuingia ikulu itamhudumia mtu yeyote bila kujali itikadi ya chama,wala dini,walakabila.Nitamhudumia mwana Chadema,nitamhudumia mwana ukawa,nitamhudumia mwana CCM na wale wote wasiokuwa na vyamaalisisitiza Dr Magufuli.
Aliongeza kuwa serikali atakayounda iwapo watanzania watampa ridhaa ya kuongoza nchi kuanzia mwakani atahakikisha wazee wanaanza kulipwa pesheni,sambamba na kuhakikisha kupunguzwa kwa bei ya vifaa vya ujenzi ili watanzania wawe na uwezo wa kujenga nyumba bora.
Dr Magufuli alienda mbali kwa kuahidi kuwa atakuwa rafiki wa wafanya kazi wanaotimiza wajibu wao na kuhakikisha wanalipwa vizuri ili waweze kutimiza wajibu wao na kwamba hatawavumilia wafanya kazi wazembe katika serikali atakayoiunda endapo atapewa ridhaa ya kuongoza Tanzania awamu ya tano.
Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mtwara kwenye uwanja wa Mashujaa ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa Mtwara utakuwa mji wa viwanda na wananchi wake watapewa kipaumbele katika ajira.
Mgombea Urais kupitia CCM, Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa Ubunge jimbo la Mtwara, Mhe.Husnein Murji kwenye mkutano wa kampeni za CCM kwenye uwanja wa Mashujaa.
Mhe.Husnein Murji akihutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni za CCM kwenye uwanja wa Mashujaa
Umati wa wakazi wa Mtwara waliojitokeza kwenye mkutano wakisikiliza hotuba za viongozi mbali mbali.