Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu


..ni kweli ukawa wamepigwa ganzi kuzungumzia ufisadi.

..lakini sasa wameibuka na hoja ya MABADILIKO.

..naona kama vile CCM wana-struggle jinsi ya kuwashawishi wananchi wenye kiu ya mabadiliko.

..sasa hivi ndiyo unaona wamebaki na hoja za kutisha wananchi kuwa wakifanya mabadiliko watakuwa kama LIBYA.
 
Jenga hoja ili nijue kweli hapa ni kazi au ujambaz!!! Km cc tunafisad 1 nyie mnao 11 sa wa wap ndo hawasafishiki?
 
Idawa umemjibu vyema huyu jamaaaa, msema kwel n kura, wengi wenu humu mmekula pesa za lowasa ndo maana mwashindana weka post humu ili muonekane mwafanya kaz bt mwsho wa siku kura zenu kwa Magufuli tuu

kweli wewe ni kiboko.
Asante kwa kuwapatia wanafiki ukweli.
 
Subirini tarehe 8/09/2015 Pale Mji wa ifakara utakaposimama EL Atakapokuja kuwajambisha MAFISADI na huyo makufuli
 

Mpigie Kura kiongozi mwenye sifa ya kuchukia Rushwa, Ufisadi na asiye na kigeugeu​
 
acheni sired za hawa wafu...hazina mzuka kokote kule...iwe baani...ndani ya bus...facebook...whatsaap nk
 
Tar 25 ncha ya kidole cha mwisho cha mkono itakua na wino..ukiona hvyo ujue kura yangu kwa magufuli. Otherwise kadi ya kura itabaki kwenye wallet until further notice
 

CCM haina haja ya ku-struggle kuhusu mabadiliko kwa vile wanachotakiwa ni kuonyesha tu kuwa wako serious kuleta mabadiliko ndiyo maana wakawatosa viongozi wake waandamizi. Wakumbushe kuwa mabadiliko siyo kubadilisha na majina ya vyama bali ni kubadilisha viongozi; huwezi kupata mabadiliko kwa kuondoa chama cha CCM na kuleta chama cha CHADEMA kinachoongozwa na wale wale waliokuwa CCM.
 

..kwa mtu wa nje kueleza ni rahisi.

..lakini mtu wa ndani ya ccm ni vigumu kwasababu ccm walishapewa nafasi ya kuleta mabadiliko lakini hawakuyaleta.

..hata Magufuli anapata taabu sana na hii hoja ya mabadiliko na ndiyo maana anajaribu kutisha wananchi na habari za Libya. Pia kuna wakati alikuwa anawatisha wananchi kuwa Tz itakuwa kama Iraq, au Zaire.

..Ukishaona mgombea anadanganya waziwazi ujue kuna tatizo.

NB:

..hata ukawa nao wana-struggle haswa na kuibuka kwa Dr.Slaa. inasemekana Dr atakwenda mikoani " kuwaaga" wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…