Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Pesa uchaguzi huu kwa upande wa CDM hakuna. Ndio inaombwa hiyo michango.
Nyomi mara nyingi inadanganya watu. Wengi hawaendi kupiga kura hata kama wanacho kitambulisho.
Pesa uchaguzi huu kwa upande wa CDM hakuna. Ndio inaombwa hiyo michango.
Nyomi mara nyingi inadanganya watu. Wengi hawaendi kupiga kura hata kama wanacho kitambulisho.

Kwa hiyo mkuu tusiwe na wasiwasi. Nyomi za CHADEMA kura hawapigi Ila za CCM.

Au vp mkuu?
 
alafu hakunaga kitu kama uchumi in real, mtu kua maskini ama tajiri that all depends kwa mtu mwenyewe! wanaoendesha uchumi wa hii nchi ni wafanya biashara! izo kelele zingine ni upuuzi mtupu, mnakua kama hamjasoma bwana
Sio kweli, nitakupa mfano mdogo tu, angalia vijana wa bodaboda, wakati wanazuiwa kuendesha pikipiki unadhani uchumi wa familia zao ulikuwa umesinyaa kiasi gani na ninani alikuwa anawazuia wasifanye hizo kazi ? jibu unalo, unapomfukuza mtu kazi aliyekaribia kustaafu unadhani umedumaza watu wangapi walionyuma yake? unapombomolea mtu nyumba ya ndoto yake na usimpe fidia unadhani umedumaza wangapi, unapokataa bima ya afya isitumike kwa yeyote yule lkn wabafamilia unadhani umedumaza wangapi, ndugu orodha ni ndefu, jitambue.
 
Ni kweli kabisa Rais Magufuli amefanya mengi ambayo mazuri kwa ("baadhi ya") Watanzania. Lakini mimi nina maswali kadhaa ambayo napenda nyie mlio serious katika kuchambua kampeni zinavyoenda mjiulize:-

1. SGR inatoka Dar kwenda mikoani. Wanaofaidi ni watu wa Dar, sio wa Kigoma, wala Moshi wala Songea n.k. Vivyo hivyo flyovers na interchange na barabara nzuri zimejengwa zoooote Dar. Sasa hebu jiulize:- Unadhani ukimwambia Mtanzania aliye mkoani umemletea maendeleo atakuelewa akupigie kura wakati yeye hajaona hayo maendeleo mkoani kwake?

2. Ununuzi wa ndege ni jambo zuri. Lakini Watanzania wengi sasa ni waelewa. Wanajua kwamba kuendesha shirika la ndege ni kazi ngumu sana na ndio maana mashirika kadhaa ya ndege duniani yamefunga shughuli au kuuza ndege zake kwa kupata hasara. Zaidi ya hapo, Mtanzania wa kawaida ni lini atakaa apande ndege maishani mwake? Unadhani ukimwambia umenunua ndege atakuona umefanya jambo la maana? Lazima atajiuliza kama kweli ulikuwa unataka kuboresha maisha ya Watanzania kwa nini usingeongeza idadi ya mabasi ya mwendo kasi Dar ili kuondoa adha ya usafiri na kupunguza muda wa kazi unaopotea?

Tena atajiuliza kama umenunua hizo ndege kwa ajili ya kuleta watalii, mbona anga za Tanzania zilipofunguliwa hatukuona ndege zetu zikileta watalii bali walikuja na Ethiopian na Emirates?

3. Miaka yote tangu enzi za Nyerere, kila sikukuu ya Mei Mosi, rais aliyekuwa madarakani alikuwa anatangaza ongezeko la mshahara (hata kama ni kiasi kidogo). Kwa miaka mitano ya Rais Magufuli hakuna nyongeza na yeye ametamka wazi kwamba hataongeza mpaka amalize huo ujenzi wa mioundombinu anaoufanya. Unadhani kama wewe ni mfanyakazi unaweza kumshabikia rais ambaye hayuko tayari kukuongezea mshahara japo anajua kwamba hali ya maisha ni ngumu (kiasi cha kukataza watu wasiseme vyuma vimekaza)? Sio rahisi sana.

4. Nashindwa kuelewa ni kwa nini kabla ya kampeni kuanza, serikali haikuhakikisha kwamba wakulima wote ambao hawajalipwa kwa mazao waliyouza wanalipwa. Wengi ambao walikuwa ni wapenzi wa CCM hawaifurahii tena kwa sababu wamekopwa mazao yao japo Rais anasema anatetea wanyonge. Sio rahisi waipigie CCM kura safari hii.

Kwa kutafakari haya mambo niliyosema hapa juu, utaelewa kwamba uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu kwa CCM. Ipo sababu ingine ya kuufanya uwe mgumu. Wapenzi wakubwa wa CCM ambao walikuwa wanaipigania miaka mingi wameumia sana rohoni walipoona wahamiaji kutoka vyama vya upinzani wamepitishwa na chama chao kugombea wakaachwa wala waliohenyeka miaka nenda miaka rudi.

Asijali, atapumzika mazima tutapompa nchi Tundu Lissu. Aje atimize tu wajibu, nchi anakabidhiwa mwenye unyenyekevu wa kweli kweli mbele za Mungu; TUNDU A LISSU.
 
Mkuu alishasema lakini kachoka ila ni ULAFI wa madaraka tu. Madaraka YAMEMLEVYA.

Katika hali inayoashiri mikikimiki ya Campaign, Mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi amepumzika kufanya kampeni.

Wachambuzi wa mambo wanatafsiri kuwa kampeni za Mwaka huu zimekuwa siyo nyepesi kama zilivyodhaniwa.

Magufuli ambaye mwaka 2015 alizunguuka kwa barabara nchi nzima, inaonekana dhahiri kuwa safari hii hawezi kuifikia rekodi ya mwaka huo. Safari hii inaonekana ameweka nguvu zaidi katika mikoa ya ukanda wa ziwa huku Wapiga kampeni wengine wakienda kanda nyingine.

Hata hivyo wapiga kampeni wake yaani Mama Samia na Kassim Majaliwa hawana mvuto mkubwa wa kisiasa wa kuweza kuchangia kura za maana kwa Magufuli.

Wakati huohuo mgombea wa Chadema Tundu Lissu ambaye ana faida ya kujinadi mapema makhsusi kwa ajili ya uchaguzi huu kwa kisingizio cha "kutafuta wadhamini" ameendelea kuchanja mbuga kwenye ngazi ya jimbo kwa jimbo baada ya kumaliza kupiga show kwenye ngazi ya kanda kwa kanda.

Sambamba na ngazi ya Jimbo kwa jimbo, Chadema watafanya mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha wanamng'oa Magufuli madarakani.

Bado haijajulikana kama kupumzika huku kwa mgombea wa CCM ni routine ya kawaida tu au uchovu au afya, tunangoja chama cha mapinduzi kitujuze zaidi.

View attachment 1567050
 
Kuna tafsiri nyingi hapa
1. Keshajihakikishia ushindi kwa njia zisizojulikana
2. Amekata tamaa
3. Uchovu na afya
4. Mbinu ya kumpumbaza adui
5.UKATA
Kengine yote nakuunga mkono mkuu, Ila hapo 🖕 kwenye ukata😳,mmh napata kigugumizi kuamini.
 
Lazima atembelee gamboshi kama kawaida yake la sivyo mambo yake hayaendi vizuri.
Tunajua wewe Ni mke wake, hivyo Ni halali kabisa wewe kujua, anakotembelea mmeo.
Usiache kutujulisha kitakacho endelea huko gamboshi.
 
Mwingine anaweza kusema mwaka 2015 alitumia nguvu kubwa na akapita maeneo mengi kwa sababu kazi ilikuwa ngumu hata matokeo ya Uraia yalisadifu hilo.

Mwaka huu kazi ni nyepesi mno, kila mtu anaona kinachotokea, mwitikio wa Raia kwake na kwa wapinzani wake. ACT wameshanyosha mikono, CDM ndiyo Kama hivo, Juzi uliona Raia wa pwani Kama vile hawamjui, Jana Morogoro mjini umeona hali mwenyewe, kule Mheza ilikuwa aibu. Hata Makamanda tangu Mlivyoposti picha za Mbeya, hamjaposti tena, utafikiri Mgombea wenu yupo likizo naye.

Sasa kwa namna hiyo kwanini asipumzike Budha. Game imekuwa nyepesi mno.
Kama umegundua, wanachokifanya CCM baada ya uhakika wa Kushinda, ni kuhakikisha mtu anapata kipigo cha mbwa koko, hicho ndicho kinachofanyika kwa Sasa.
nyie ndiyo mliye mdanganya kuwa uchaguzi utakuwa bwerere
 
Katika hali inayoashiri mikikimiki ya Campaign, Mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi amepumzika kufanya kampeni.

Wachambuzi wa mambo wanatafsiri kuwa kampeni za Mwaka huu zimekuwa siyo nyepesi kama zilivyodhaniwa.

Magufuli ambaye mwaka 2015 alizunguuka kwa barabara nchi nzima, inaonekana dhahiri kuwa safari hii hawezi kuifikia rekodi ya mwaka huo. Safari hii inaonekana ameweka nguvu zaidi katika mikoa ya ukanda wa ziwa huku Wapiga kampeni wengine wakienda kanda nyingine.

Hata hivyo wapiga kampeni wake yaani Mama Samia na Kassim Majaliwa hawana mvuto mkubwa wa kisiasa wa kuweza kuchangia kura za maana kwa Magufuli.

Wakati huohuo mgombea wa Chadema Tundu Lissu ambaye ana faida ya kujinadi mapema makhsusi kwa ajili ya uchaguzi huu kwa kisingizio cha "kutafuta wadhamini" ameendelea kuchanja mbuga kwenye ngazi ya jimbo kwa jimbo baada ya kumaliza kupiga show kwenye ngazi ya kanda kwa kanda.

Sambamba na ngazi ya Jimbo kwa jimbo, Chadema watafanya mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha wanamng'oa Magufuli madarakani.

Bado haijajulikana kama kupumzika huku kwa mgombea wa CCM ni routine ya kawaida tu au uchovu au afya, tunangoja chama cha mapinduzi kitujuze zaidi.

View attachment 1567050
Kati ya ujinga wa waTanzania wengi ni kutokujua hesabu kubwa ya CCM inavyopigwa kwa akili na wao kutokua na wasi wasi wowote wa kushinda,watu wengi wanaendeshwa na mihemko tu ya vyama na hawajui kabisa pumzi kubwa na hesabu kubwa za CCM.
 
Sio kweli, nitakupa mfano mdogo tu, angalia vijana wa bodaboda, wakati wanazuiwa kuendesha pikipiki unadhani uchumi wa familia zao ulikuwa umesinyaa kiasi gani na ninani alikuwa anawazuia wasifanye hizo kazi ? jibu unalo, unapomfukuza mtu kazi aliyekaribia kustaafu unadhani umedumaza watu wangapi walionyuma yake? unapombomolea mtu nyumba ya ndoto yake na usimpe fidia unadhani umedumaza wangapi, unapokataa bima ya afya isitumike kwa yeyote yule lkn wabafamilia unadhani umedumaza wangapi, ndugu orodha ni ndefu, jitambue.

na pia ni very stupid mtu unakua na one source of income, mfnao uliotoa ni sawa sawa tu na mtu alieajiriwa vizuri lakini ghafla kampuni haijaenda vizuri inabidi atafute sehem ingine, tafaut ya hawa wtu wawili ni ndogo sana! wote upnde mmoja ukikata basi maisha yao yanayumba, lakini chukulia wafanya biashara wakubwa wakubwa, unadhan hwarecord losses kwenye financial statements zao? but there comes a rescue from another source of income, ndo maaana nkasema before uchumi ni nadharia! it depends with how you handle it, mtu kufa ama kupoteza ajira ama chochote ni swala la kawaida na sio kitu cha kutisha because ndo uchumi unavotakiwa urun, at the end of the day its still down to yourself
 
Kusema kampeni za CCM ni ngumu ni vichekesho. Rais Magufuli hata asipopiga kampeni kuanzia leo ushindi ni 90%

Rafiki zetu wa CHADEMA mtaula wa chuya huu mwaka hampati hata mbunge.
Natamani siku MOJA kibao kikugeukie uyapate maswaibu ya huu utawala....sisi waislamu tunasemaga inshallah....
 
Back
Top Bottom