Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Utamkumbuka wewe na familia yako, uwanja wa ndege Chato unakusaidia nini?
 
Wananchi hatukuelewi hata unasema nini.
 
Anashabikia ujinga huku amejaa shida mpk sehemu za siri
Mwenye kujibu uwepo wa maji Safi na salama mji wa katoro na buseresere mkoa wa Geita ,miji iliyopo Jimbo alilizaliwa magufuli ajibu na amehudumia Jimbo hilo kwa miaka 20 akiwa mbunge na waziri. Hakuna maji na Kuna wakazi mamilioni
 
Mwenye kujibu uwepo wa maji Safi na salama mji wa katoro na buseresere mkoa wa Geita ,miji iliyopo Jimbo alilizaliwa magufuli ajibu na amehudumia Jimbo hilo kwa miaka 20 akiwa mbunge na waziri. Hakuna maji na Kuna wakazi mamilioni
Huo uwanja mbona umepelekwa baada ya yeye kuwa Rais?
 
Na: Giantist McWenceslaus
Dodoma
14/09/2020.

www.ccmmpya.org

Habari za muda ndugu wanabodi wenzangu... Nakumbuka kuwa nilikwishapata nafasi ya kuwajuza mafanikio mbalimbali yaliyopatikana ndani kwa miaka minne na miezi kadha chini ya uongozi makini wa Dkt. John P. Magufuli kupitia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020. Niligusia mafanikio hayo kwa upana zaidi na kwa maandishi mengi kweli katika sekta ya Elimu na sekta ya Afya. Basi kwa heshima na taadhima leo napenda niwashirikishe katika kuwaonesha mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya uchukuzi, ujenzi na mawasiliano kwa maendeleo ya nchi.

Kwa kuzingatia muda na ushauri ambao nimeweza kuupijea kutoka kwa wadau wengi, nitajitahidi kuyasema kwa maneno machache sana. Nitahakikisha nazingatia maeneo ya msingi kwa uchache.

Hata hivyo, umuhimu wa sekta hii kwa wananchi umepata kujidhihirisha kwa uwazi na hasa ukizingatia ni maeneo ambayo yanawajibika moja kwa moja katika kuwaunganisha watu na kuifanya nchi kuwa moja. Na kwa hakika ni sekta ambayo ina mahusiano ya moja katika kuimarisha uchumi wa watu na taifa kwa jumla, na hasa katika karne ya sayansi na teknolojia ambapo suala la muda ndio mtaji wa msingi katika kufanikisha jambo liwalo lote lile.

Hivyo basi, leo tutaitazama sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Tutakumbuka kuwa maadui wa maendeleo wale watatu: Ujinga, umasikini na maradhi. Na kwamba ujinga na maradhi wameweza kusambaratishwa kutika na kuimarika kwa sekta ya Elimu na sekta ya Afya. Kwa hiyo ili kuweza kumfarakanisha adui umasikini, serikali chini ya ilani ya CCM iliweka nguvu katika kuimarisha sekta hii ya uchukuzi, ujenzi na mawasiliano. Na kwa kiasi kikubwa hilo limewezekana chini ya uongozi imara wa Rais Dkt. John P. Magufuli kwa miaka Mitano ya mwanzo 2015 - 2020.

Mhe. Rais Dkt. JPM kupitia maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi, ameweza kuimarisha njia za uchukuzi na ujenzi wa miundombinu muhimu pamoja na mawasiliano kwa madhumuni ya kuchochea kasi ya kuongezeka kwa wawekezaji nchini, kurahisisha shughuli za kibiashara katika maeneo yote muhimu na hasa kilimo, na kurahisisha muda kukaa muda mwingi njiani na kuingeza muda mwingi wa kufanya kazi ili kuongeza uzalishaji. Na kwa kufanikisha mambo hayo, leo watanzania ni mashahidi wa faida ambazo zimeweza kupatikana kutokana kupitia sekta hizo, ukiachia mbali uhakika wa ajira ambao vijana wengi ndio wanufaika, watanzania wameweza kuona faida ya kuimarika kwa sekta hizo na hasa katika kuzisaidia kukua na kuimarika kwa sekta ya Afya kwa kurahisisha uharaka wa upatikanaji wa huduma ya afya kwa watu ambao hutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kupata huduma bora zaidi ya afya.

Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa miaka mitano ya kwanza alifanya mambo kadha yenye tija kwa maendeleo ya nchi katika sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kama yafuatayo:

Mosi, amejenga barabara na amepanua barabara. Miaka ya nyuma gharama ya bidhaa nyingi zilikuwa kubwa kutokana na ufinyu uliopo katika usafirishaji (miundombinu ya barabara) ambapo mfanyabiashara ilimpasa atumie gharama kubwa kusafirisha bidhaa zake na hivyo kufanya mlaji wa mwisho kupata huduma ya bidhaa hiyo kwa bei ya juu zaidi. Lakini pia, tumeshuhudia zaidi ya tani milioni tano ambazo zimesafirishwa kutokea bandari ya Dar es Salaam na kuelekea nchi za jirani kwa kupitia barabara, na hivyo kupelekea makusanyo makubwa ya fedha katika serikali, na hivyo kuongeza mapato ya nchi. Etoshe kusema kuwa zaidi ya asilimia 98 ya maeneo ya Tanzania na nchi jirani zimeunganishwa kwa pamoja kutokana na kuwepo kwa barabara za kiwango na za uhakika.

Kupitia sekta hii Rais Dkt. JPM amefanikiwa kupunguza kero ya msongamano wa magari katika mkoa wa Dar es Salaam na kupelekea watumishi wengi kuchelewa kufika kazini au kukosa kabisa muda wa kumpumzika kutokana na kuwahi kuamka ili kukwepa msongamano wa magari, na hivyo kupunguza weredi wa kufanya kazi na kupunguza tija ya kazi kwa mtumishi. Na hiyo imewezekana kutokana na ujenzi wa Daraja la Mfugule TAZARA, pamoja na ujenzi wa Ubungo Flyover, ambayo ipo katika hatua za mwisho mwa ukamilifu wake. Dar es Salaam Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! Watumishi Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! Huyo ndiye Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na hiyo ndiyo CCM yenyewe, hakuna chama kingine chenye mikakati madhubuti ya kuondoa umasikini nchini.

Pili, amejenga vivuko vipya na ameboresha vivuko vya zamani. Upo usemi mashuhuri wa wazee wetu, usemao "Siri ya mtungi aijuaye kata!" Adha ya uhaba wa usafiri wa kuvukia maeneo ya maziwa, mito na Pwani za bahari, wanazifahamu wananchi wakazi wa maeneo hayo. CCM na Dkt. John Magufuli hakika walikuwa ni sehemu ya kata hizo hivyo ilikuwa rahisi kuweza kutambua siri za mitungi ya wananchi. Serikali kwa miaka mitano imeweza kuhakikisha inaziondoa adha na tabu za vivuko kwa wakazi wa maeneo ya ng'ambo ikiwa ni sehemu ya kuwarahisishia usafiri, na kuwaletea nafuu ya maisha kwa kuweza kufanya biashara zao kwa urahisi kutokana uhakika wa kuwepo kwa vivuko. Maeneo ni mengi sana kwa mfano, ilani ya CCM 2015/2020 iliielekeza serikali kukarabati vivuko vitatu maeneo ya Pangani, Busisi na Kigamboni, na kujenga vivuko vipya vinne maeneo ya Nkome, Nyamisati, kayenze na ukara. Vivuko ni moja ya njia za mawasiliano, ambayo huunganisha watu na kuwarahisishia katika kufanya kazi za uzalishaji katika kuimarisha uchumi wa watu na wa nchi.

Tatu, ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR na kufufua reli za zamani, ikiwa ni ile ya Tanga - Moshi na Moshi - Arusha .Ukweli usipongika ni kuwa Shirika la Reli la Tanzania ni shirika ambalo lilikuwa likichechemea katika kujiendesha yenyewe. Na hiyo ilipelekea kukosekanika kwa miundombinu imara ya reli ambayo ilipelekea kukosa wateja na hatimaye kushindwa kujiendesha! Ndio kusema shirika hili lilidhoofika lenyewe. Hata hivyo, kwa muda wa miaka mitano Mhe. Dkt. John P. Magufuli ameweza kulifufua na kulisimamisha imara shirika letu la Reli... kwa kurudisha huduma za Reli kutokea Tanga kupitia Moshi na kueleke Arusha. Ni ukweli wa shahiri kuwa uasfiri wa Reli ni dawa kwa watanzania wa kiapato cha chini, ambao kwa shirika kuweza kurudisha usafiri wa treni itawasaidia kupunguza gharama za usafiri wao pamoja na mizigo yao. Ambapo kabla, walikuwa wakiitumia gharama kubwa za kusafirisha mizigo yao mwa njia ya basi.

Kwa sasa serikali chini ya ilani ya CCM na usimamizi wa Mhe. Rais Dkt. John P. Magufuli, inaendelea na ujenzi wa Reli ya kisasa ya SGR ambayo itawezesha shughuli za kiuchumi kuongezeka kwa kasi kubwa sana. Kwani watu watakuwa wanaishi mkoa mmoja na kwenda kufanya kazi mkoa mwingine, haitoshi hiyo pekee lakini pia haitachukua zaidi ya siku kwa mfanyabiashara kuweza kuutoa mzigo wake bandarini na kuuleta kwenye eneo lake la biashara hivyo itasaidia upatikanaji wa bidhaa nyingi kwa urahisi na uharaka. Mradi huo wa ujenzi utatoa fursa nyingi sanaata baada ya kukamilika kwake, achana hii faida ya sasa ya kutoa ajira za kutosha kwa vijana wengi wa kitanzania, na kina mama.

Nne, kuimarisha shirika la usafiri wa anga ATCL kwa kununua ndege nane, na kuboresha viwanja vya ndege ikiwemo cha Dodoma, Julius Nyerer International Airport (JNIA) na ujenzi aa kiwanja cha ndege wa mkoani Geita. Pamoja kuimarisha ulinzi wa anga kwa kununua rada kubwa na za kisasa, kazi hiyo ni ndani ya miaka minne na miezi kadhaa. Ukweli ni kwamba faida zitokanazo na kuimarika kwa shirika la Ndege la Taifa ni nyingi sana sana katika kukuza uchumi wa nchi. Katika karne ya sasa Dunia ni Kijiji, na kama ambavyo barabara imekuwa ikiunganisha mkoa na mikoa mengine mengi, na nchi za jirani kwetu, vivyo kwa ndege ambazo zenyewe inaiunganisha nchi yetu na Dunia. Na kwa hakika zipo fursa nyingi zaidi na hasa nchi inapokuwa imejiunganisha vema na Dunia!

Tano, ujenzi wa Meli za Kisasa. Mpaka nayaandika haya leo ni dhahiri shahiri kuwa serikali imeendelea na kukarabati meli pia, ikiwa ni sehemu moja ya kuweka mazingira mazuri ya usafirishaji pamoja na ya kibiashara. Mhe. Rais Dkt. John P. Magufuli, katika utekelezaji wa ilani ya CCM ya 2015/2020 amefanikiwa kukarabati MV Clarias, MT Sangara na ML Wimbi, MV Viktoria na MV Butiama. Kama hiyi haitoshi mpaka wakati huu serikali ipo mbioni kukamilisha ujenzi wa Meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu. Na kwa hakika mambo ni mengi hasa ambayo yametekelezwa na ilani ya CCM kwa miaka mitano ya mwanzo chini ya Mhe. Rais Dkt. JPM. Itoshe kusema mapambano dhidi ya adui umasikini yanaendelea vizuri na kwamba kama nchi Mhe. Rais Dkt. JPM amefanikiwa kuiweka nchi yetu Tanzania katika uelekeo sahihi wa kupata ushindi huo, na hiyo itafanikiwa kwa haraka kama watanzania tutampatia kura na ridhaa nyingine ya kuongoza nchi kwa miaka mitano mengine chini ya ilani ya CCM ya 2020/2025.

Hii ndio CCM Chama Kubwa. Na huyu ndiye Dkt. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, ifikapo Oktoba 28, 2020. Nenda kamchague Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ili akaongoze kwa miaka mitano mengine 2020 - 2025.

#MchagueDkt.JPM
#TumeahidiTumetekelezakwaKishindo
#Tunasongambelepamoja
#ChaguaWabungewaCCM
#ChaguaMadiwaniwaCCM

Sauti ya Mdodomia
 
Umeandika mengi ila sijayasoma nataka niijibu title yako halafu nikasome

Jibu ni
Ujinga- wananchi hatuelewi hasa yapi majukumu na wajibu wa raisi
Uoga- kuna watu wanatishiwa na jiwe eg Bariadi
Tutaibiwa- kuibiwa kwa kura ni lazima kuwepo
 
Umeandika mengi ila sijayasoma nataka niijibu title yako halafu nikasome

Jibu ni
Ujinga- wananchi hatuelewi hasa yapi majukumu na wajibu wa raisi
Uoga- kuna watu wanatishiwa na jiwe eg Bariadi
Tutaibiwa- kuibiwa kwa kura ni lazima kuwepo
Ujinga wa wananchi ndiyo mtaji wa CCM
 
Mwenyekiti na mgombea wa CCM amekubali kuegemea Kamba,anajibu hoja za Lissu na Kutekeleza ahadi za Lissu na Chadema . Kwa staili hii ya kukubali kukaa kambani Lissu anachagua pa kupiga .

Wananchi waliokuwa wanapuuza hoja za mishahara, ajira mpya na bima ya afya kwa wote wamemwamini Lissu na wanasikilza kwa makini kujua atamwagiza nini mgombea wa CCM. Yupo mmoja kamwom a Lissuaagize mifuko ya ensheni ilipe watumishi.
 
Usitupoze wewe majibu bado hapa

  1. Ni faida kiasi gani ndege hizo zinaleta kwa taifa?
  2. Kwanini amehamishia ndege kwenye kasma namba 20 ambayo haikaguliwi na CAG kama ambayo mashirika mengine ya umma yanakaguliwa?....
Good questions. Maswali haya yakijibiwa Kwa ufasaha yanaweza saidia zaidi CCM kuliko yakipuuzwa mana ndio hayahaya wapinzani wanatumia kuchanja mbuga. Kwa bahati mbaya, sioni mtu wa Chama akiattempt kuyajibu Kwa ufasaha. Majibu mengi yanayotolewa yanakaribisha Maswali zaidi badala ya kupunguza Maswali.
 
Na kauli za Polepole kuwa Chadema haina hospitali haiwezi kutoa bima ya afya kwa watu wote ni kauli chakavu sana. Kwani hospitali ni za CCM?
Nadhani Boss kupoteana mana kama Chadema wakishinda maana yake hizo Hospital si zitakuwa zinasimamiwa na Serikali yao? Au anadhan bado CCM itakuwa na Sauti?
 
Mwenye kujibu uwepo wa maji Safi na salama mji wa katoro na buseresere mkoa wa Geita ,miji iliyopo Jimbo alilizaliwa magufuli ajibu na amehudumia Jimbo hilo kwa miaka 20 akiwa mbunge na waziri. Hakuna maji na Kuna wakazi mamilioni
Akikujibu nakufa
 
Toka Lissu aombe mdahalo na Magufuli sijasikia chochote kutoka kwake. Nilichokiona ni wana CCM kumkingia kifua mgombea wao kwa kutafuta visingizio
 
Tanzania hatuna Sana ada na midahalo.

Slaa Aliutaka Mdahalo, hatukutokea na TULISHINDA.

CHADEMA Ukawa nayo haikutaka Mdahalo. Wakaweka Mpira Kwapani. MAGUFULI akashinda!
 
Ushamba tu..hapo Kenya tu kila chaguzi kuna presidential debate..Magu hawezi battle na
Lissu" kidude" kitazima
 
Ile kampeni ya mgombea Urais wa JMT kupitia CCM ndugu John Magufuli haitokuwepo leo.

Inasemekana kesho ndiyo ataelekea huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…