Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Kinana na Sumaye wote wako ulingoni Kinana alianzia Chalinze akaenda Arusha, Sumaye alikuwa Singida Lowassa pekee ndio sijamsikia
 
Wamekusikia, swali fikirishi je wanaweza? maana kampeni za mwaka huu nizakupinga kwa hoja na sio kwa vioja
Wanaweza hasa ukiangalia influence walionayo kweny jamii na utashi wao kisiasa na uzoefu wa kutosha.
Niwatu wanaoweza kukinadi chama na kikapata uwingi wa kura kwa kiasi Fulani.

Lowasa alikua na influence kubwa 2015 ukiacha katikati kulikua na wafuasi wa CDM, bado kuna watu huwaelezi kitu kuhusu Sumaye na mwenzake Lws, hivyo uwezo wa kufanya kampeni anao kwa namna zote wanayo.
 
Yuko vizuri, Sera zake zinaeleweka kamanda, sio lazima kila mgombea aongee kama Lissu. CCM mbele kwa mbele, CCM tano tena.
expand...Kuna tofauti kati ya fasihi Andishi na Simulizi. Sera za vyama zimeandikwa na kuchambuliwa kwenye vitabu. Ukiachilia mbali kwamba sio wote wanaweza kupata vitabu hivyo lakini pia sio wote wanaoweza kusoma wakaelewa.

Tundu LISU anatumia muda wake mwingi wa kampeni kunadi sera zake kwa njia ya UHALISIA " Realities " .Jambo hili linawakera sana CCM kwa sababu anachofanya ni kama mwalimu anavyofundisha darasani.

Anaanza kueleza tatizo kwa kulitaja ..Kwa mfano ugomvi wa wakulima na wafugaji. Baada ya hapo anaeleza chanzo cha tatizo hilo..Mfano" Ardhi kubwa kumilikiwa na viongozi wakubwa au kampuni kadhaa na hapa anawataja kwa majina.

Baada ya hapo anaeleza jinsi walivyopata ardhi hiyo,kama ni kwa minajili ya vyeo vyao au kuuziwa isivyo halali au halali. Pia hueleza faida au hasara ya watu hao kujimilikisha ardhi hiyo.

Mwisho anarudi kwenye suluhisho kwa mujibu wa SERA za Chadema au kwa mujibu wa sheria za nchi ili kuonyesha UDHAIFU na kutowajibika kwa viongozi waliopo.

Huu ni uwasilishaji BORA kabisa wa SERA mpya na ambazo wananchi hawajazizoea au kuzielewa vizuri.

CCM na Tume (CCM) hawakutegemea kuona uwasilishaji huu. Walitamani awe anasoma kama ilivyoandikwa kwenye kitabu. Lakini pia walipenda waone uwasilishaji huo uwe kama alivyofanya Lowasa(2015) ,Dr Slaa(2010) au Freeman Mbowe (2005) ambao walikua wanazisema juu juu bila mifano hai inayowagusa wananchi wa eneo husika.

Hongera Tundu Lissu! shikilia hapohapo watu wanakuelewa sana na pia unawavuruga watu wa Lumumba. Hawana uwezo wa kujibu hoja zako,wanaishia kuandika "Magufuli 5 Tena
 
Watanzania gani wanaotaka kuongozwa na Magufuli?
Zamani kura za wadada na wamama ndizo ziliibeba CCM ila sasa wadada wote na baadhi ya wamama hawampendi huyu Mzee.
 
expand...Kuna tofauti kati ya fasihi Andishi na Simulizi. Sera za vyama zimeandikwa na kuchambuliwa kwenye vitabu. Ukiachilia mbali kwamba sio wote wanaweza kupata vitabu hivyo lakini pia sio wote wanaoweza kusoma wakaelewa..

Hana lolote la maana linaloishitua CCM.
CCM imeshayabaini mambo makubwa ( great things) , imeshatambua na inazo rasilimali ( resources ) na CCM inaendelea kufanya hayo mambo yatokee.

Na hata huyo tundu anayashuhudia hayo mambo makubwa na yanamuwezesha yeye kufika kwa baadhi ya watu na kuwaenezea chuki na kuwahadaa.

Great things never happens over a sudden, ni lazima ifanyike kama nilieleza hapo juu na inavyofanywa na CCM chini ya usimamizi imara wa Jemedari Dkt ( pHD ) JOHN Pombe Magufuli.

Yeye tundu anadhani akisema yanatokea kama alivyofanya Mungu alipouumba ulimwengu. Mwambieni aache theory za darasani. Tunataka kazi ambayo inaendelea kuchapwa na CCM.

Nawashauri anzeni na kujenga chama chenu kwanza. Mnashindwa hata kujenga Ofisi kwenye hizo kanda zenu , hamna uongozi kwenye ngazi za chini . Mtaongoza mkiwa kileleni?

Uongozi wa hivyo haupo. Yapo mnayoiga CCM basi igeni na system za uongozi halafu ndio mje mtafute mambo makubwa.
 
Nimepita sehemu kadhaa ambapo kuna TV na mikutano ya Magufuli ikirushwa Live.

Kitu nilichonotice ni kwamba wananchi wameshakuwa saturated na kumuona Magufuli, yaani wamemuona sana yeye peke yake mpaka sasa hawana shauku ya kumuona wala kumsikiiza sana.

Nimeona watu wakila chakula migahawani huku TV ikirusha mikutano ya Magufuli lakini wananchi wakiwa hawana time nayo.

Sababu kuu huenda ni kuona mtu yuleyule akiwaambia mambo yaleyale tangu kipindi cha kampeni iliyopita ya mwaka 2015.

Ukichukua kameni za Magufuli za mwaka 2015, ukalinganisha na za sasa anaongea almost yaleyale.

Kitu kingine ni wananchi kukata tamaa na utendaji wa Magufuli.

1. Magufuli aliingia madarakani kwa hoja kuu ya kupambana na ufisadi, lakini leo hii tunaona badala ya kukamata mafisadi halisi wale walioingia mikataba ya kifisadi ya madini, tunana akikibizana na wafanyabiashara na kuwaoa kesi za uhujumu uchumi, lakini wakita hela anawaachia.

2. Magufuli alitwambia akina Deo Mwanyika wanashirikiana na Mabeberu wa ACACIA kutuibia kwenye madini, akamfungulia kesi, baada ya miaka mitatu akamfungua na kumpitisha kugombea ubunge jimbo la Mbeya Mjini. Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM iweje awapelekee mgombea fisadi wananchi wa njombe mjini?

3. Kuna matukio chungu nzima ya wagombea wa CCM waliotoa rushwa ili kupata nafasi ya kushika tiketi ya kugombea ubunge kwa chama hicho, TAKUKURU inajua na Magufuli anajua lakini kawapitisha

4. Kuna siasa za biashara ya kisiasa zilifanyika ndani ya miaka hii mitano ya utawala wa Magufuli

5. Magufuli alitutangazia kuwa Andengenye na Lugoa wameinhia mkataba wa kifisadi wa shilingi Trilion 1, baadae akasema amemsamehe Andengenye na akamteua kuwa mkuu wa mkoa.

Kwa hiyo wananchi wakikumbuka yote hayo, wanaona kuwa Hoja ya kupambana na ufisadi ni usanii mtupu

Pia kuna ahadi ambazo Magufuli na CCM mwaka 2015 waliahidi kwa wananchi baadae wakaziruka kimanga

1. Waliahidi milion 50 kila kijiji, hawakutimiza.

2. Wakiahidi kukamilisha katiba mpya, leo hii wanaikama katiba mpya kuwa siyo kipaumbele

Lakini ia kuna kukata taamaa kwa wananchi kwenye masuala ya ukosegu wa ajira, maslahi ya wafanyakazi kutozingatiwa, kuongezeka kwa makato bodi ya mikopo ya elimu ya juu, kusuasua kwa sekta binafsi ambayo ndo inaajiri watu wengi zaidi

Wananchi wakiangalia yote hayo, wanaona kama kampeni za Magufuli kama mchezo wa kisiasa tu, hawaziamini sana

wakati huohuo, Tundu Lissu anaendelea kuchanja mbuga, japo anafanyiwa kila figisu ili taarifa zake zisisambae, lakini ukweli ni kwamba taarifa zake zinasambaa mdomo kwa mdomo, watu wanatafuta clip zake, wanazichambua, wanahadithiana na kwa namna hii umma unashirikishwa, unajishirikisha kampeni ya Chadema.

Watu wana kiu ya kumsikiliza Lissu, Clip yake moja ya wiki iliyopita inaendelea kuwa chemchem ya taarifa kwa wiki nyingi zijazo, views za clip hiyo zinaongezeka kila siku na watu kuielewa zaidi.

Kiukweli kabisa kama uchaguzi utakuwa fair, Magufuli byebye!
 
Wao wanatasisi kubwa za kiserikali nyuma yao analijua hili nasikia wanajadili kufanya uchaguzi kwa portion portion wanatuogopa kujitumbukiza wazimawazima jumla
 
Huwa kila siku nasema chadema sio wananchi/watanzania mnalalamika. Sasa wewe unayefatilia sio mwananchi uliyehamasika?
 
Mleta mada na mada yake ya kutunga,

"Nimepita maeneo kadhaa yenye TV"...

Kwa hii kauli anataka tumuamini.
 
Nipo naangalia TV ya chadema hapa "youtube" hahahah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…