Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu


Kigoma ni ya wana Kigoma, wale watu hawana tofauti kabisa na Wapemba wa kule visiwani kwani unaongea nao na kukupigia makofi lakini moyoni wana chaguo lao

Na safari hii ndio kabisaa kwani pamoja na kutokuungana kwa Chadema na ACT kisheria lakini ni wazi Zitto ni rafiki binafsi wa Lissu mpaka aliweza kwenda kumsalimia Nairobi na Belgium? sasa hapo sioni kwamba Lissu atakuwa hayawani kuingia kwenye ngome yake na kumsambaratisha bali leo Lissu atapigilia msumari wa mwisho kama alivyofanya Zanzibar
 
Mkoa ulikua haujaunganishwa na Barabara, Grid ya taifa leo vinafanyika wapinzani wanasema havina maana, kwa nini wasikataliwe!

Huijui kigoma ungefunga bakuli lako.ni kikwete peke yake ndo alkuwa na mapenz na kigoma.miaka5 sasa toka Jamaa aingie barabara ni zilezile aloziacha kikwete umeme bado niwa generator una ongea nini wewe? Uwe unaenda ubungo kuangalia mabasi yanayotoka kigoma uone yalivyojaa vumbi.abiria utafkiri wafanyakazi wa mashineni kwa namna wanavyolipiga hilo vumbi humo njiani.
 
Kwa hiyo mmefanya tamasha la wasii mkaona haitoshi ikabidi muongeze nguvu kutoka Burundi lengo ni kumuangusha Zitto!!

Sasa Magufuli amekaa siku mbili tu akiondoka tu Zitto anakuja kufuta nyoyo zake zote,na Kabla ya Zitto kuja anapita Lissu anamtandika Màgufuli spanner za speed ya 5G
 
Unawajua watu wa Kigoma mbele ya burudani ya mziki??? Unakumbuka walivyojaa kwenye tamasha la diamond????

Umewapelekea Ali kiba, Harmonize, Linex , wanamuziki wa singeli alafu wasijae???
 
Kuna mgombea anaongea mpaka sauti ina mkauka mishipa imemtoka lakini kazi ni kukariri yale yale kila anapoongea na wananchi bila kuangalia mahitaji ya eneo husika na uelewa wa anao ongea nao. Hii ni kama mtu aliye zaliwa kipofu bahati nzuri macho yakafunguka kwa sekunde moja akawa kamwona punda mbele yake kisha macho kufunga tena. Kuanzia siku hiyo ikawa kila unacho sema yeye anasema ni kama punda. Ukisema fulani kajenga nyumba nzuri anasema kama punda? Ukisema fulani kanunua gari zuri yeye anasema kama punda? Ukisema dada fulani ni mzuri anasema kama punda?

Sasa huyu mgombea naye kakariri hata kabla hajaanza kuongea unajua kabisa atakariri mabilioni wizara ya afya, ndege, sgr, stigula, urefu wa barabara, bure elimu. Wakati mwingine hata anao ongea nao hawajui bilioni ina elfu moja ngapi kwakuwa maisha yao ni ya chini sana yanaishia kwenye elfu lakini yeye amekazana kutaja mabilioni. Mara ndege wakati wananchi anao ongea nao maisha yao ni baiskeli wana hitaji maji. Wengine wame dhurumiwa korosho zao. Hayupo contextual wala contemporary kabisa. Akienda kanisani ni hivyo hivyo. Bora wangekuwa wanaweka CD au flash ya hotuba yake inapofika zamu ya kuhutubia kwani wana mchosha wakati hana muktadha kabisa.
 
Kipindi kile cha dark ages akiwa ana recite idadi ya samaki ziwani basi mazuzu walikuwa wanamuona jamaa kama bonge la genius kumbe mbugira tu.
Jamaa hadi alishiba sifa akaanza kuita watu wengine vilaza.

Mamaaaaa🙆🙆🙆🙆 miaka 5 imekuwa kama upepo, imetosha kuonesha nyeti za kuku hakuna kitu pale. Ni fuvu la kubebea macho, masikio na nywele.

Mungu ingilia kati.
 
Jamaa hadi alishiba sifa akaanza kuita watu vilaza.

Mamaaaaa miaka 5 imekuwa kama upepo, imetosha kuonesha nyeti za kuku hakuna kitu pale. Ni fuvu la kubebea macho, masikio na nywele.

Mungu ingilia kati.
Ila Dr Slaa alimuonea sana kumuita Kikwete Dr nini sijuiiiii, walati wenye phd feki tumejionea wenyewe jinsi walivyo.
 
Wakati mwingine hata anao ongea nao hawajui bilioni ina elfu moja ngapi kwakuwa maisha yao ni ya chini sana yanaishia kwenye elfu lakini yeye amekazana kutaja mabilioni.

Mara ndege wakati wananchi anao ongea nao maisha yao ni baiskeli wana hitaji maji.

Wengine wame dhurumiwa korosho zao. Hayupo contextual wala contemporary kabisa.

Akienda kanisani ni hivyo hivyo.

Bora wangekuwa wanaweka CD au flash ya hotuba yake inapofika zamu ya kuhutubia kwani wana mchosha wakati hana muktadha kabisa.
 
Tuwaombeeni viongozi wetu, mmoja wa wagombea alidondoka jukwaani mchana kweupe,
Sasa wewe umekalia majungu tu Wakati mgombea kupitia Chama chako anadondoka jukwaani
 
Tuwaombeeni viongozi wetu, mmoja wa wagombea alidondoka jukwaani mchana kweupe,
Sasa wewe umekalia majungu tu Wakati mgombea kupitia Chama chako anadondoka jukwaani
Sababu mlimpiga risasi ili afe. Hajafa sasa. Na wewe utakufa kabla yake ili alione kaburi lako. Kama alivyokufa yule aliyetuita Malofa. Sema Ameen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…