Kuna mgombea anaongea mpaka sauti ina mkauka mishipa imemtoka lakini kazi ni kukariri yale yale kila anapoongea na wananchi bila kuangalia mahitaji ya eneo husika na uelewa wa anao ongea nao. Hii ni kama mtu aliye zaliwa kipofu bahati nzuri macho yakafunguka kwa sekunde moja akawa kamwona punda mbele yake kisha macho kufunga tena. Kuanzia siku hiyo ikawa kila unacho sema yeye anasema ni kama punda. Ukisema fulani kajenga nyumba nzuri anasema kama punda? Ukisema fulani kanunua gari zuri yeye anasema kama punda? Ukisema dada fulani ni mzuri anasema kama punda?
Sasa huyu mgombea naye kakariri hata kabla hajaanza kuongea unajua kabisa atakariri mabilioni wizara ya afya, ndege, sgr, stigula, urefu wa barabara, bure elimu. Wakati mwingine hata anao ongea nao hawajui bilioni ina elfu moja ngapi kwakuwa maisha yao ni ya chini sana yanaishia kwenye elfu lakini yeye amekazana kutaja mabilioni. Mara ndege wakati wananchi anao ongea nao maisha yao ni baiskeli wana hitaji maji. Wengine wame dhurumiwa korosho zao. Hayupo contextual wala contemporary kabisa. Akienda kanisani ni hivyo hivyo. Bora wangekuwa wanaweka CD au flash ya hotuba yake inapofika zamu ya kuhutubia kwani wana mchosha wakati hana muktadha kabisa.