Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Katika hali isiyo ya kawaida mhombea wa CCM John Magufuli akiwa njiani Nguruka kuelekea Urambo Tabora amampa nafasi Husna Mwilima aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini kumwombea kura mgombea wa CCM bwana Nashon, wakati Mwilima akiomba kura akamkumbisha Magufuli changamoto ambazo mgombea Nashoni amesahau kumweleza Magufuli, ndipo Magufuli bila ajizi akamwambia umekuwa mbunge hapa kwa miaka mitano ulishindwa nini kutatua shida hii ndogo ya shule.

Hapa ndipo huwa namwelewa sana Magufuli huwa hamezi maneno sehemu ambayo hajaridhika.

Maendeleo hayana chama
 
Na hapo ndipo ccm wanawachota wananchi akili, sio kazi ya mbunge kutatua kero kwa namna hiyo. Kazi ya mbunge ni kuzungumza badala ya wananchi, yaani badala ya sisi site kwenda Dodoma tunamtuma MTU akatusemee Yale tuliyokubaliana nae akatusemee. Kujenga shule, zahanati Barbara ,reli etc ni Kazi ya anaekusanya kodi.
Shida tunadanganywa wabunge kazi yao ni kutuletea maendeleo.
Wabunge kazi yao ni kuyawasilisha mawazo yetu tu, natunatakiwa tuwahukumu kwa namna wanavyotuwakilisha na sio wanavyotuletea vitu.
Huyo mama alikuwa sawa, president is wrong!!!!!!
 

Kama ni tabia ambayo nimefanana nae Rais Dkt. Magufuli basi ni ya kutokuwa 'Mnafiki' kisha 'Kutokuogopa' na kumpa Mtu 'Makavu' mubashara tu.
 
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu!
 
Hiyo kazi ya Serikali ndiyo wanakusanya kodi,tangu tupate uhuru bado tunawaza sijui Shule ,barabara nk alafu ndiyo zinakuwa agenda kwenye uchaguzi.

Kuna mahali ccm mshakwama , Mjitathimini kama bado mna uwezo wa kuongoza nchii hii.
 
Mimi nina Hasira na huyo Husna
Ndugu yetu alipata Ajira ATCL yeye akawatukana bungeni kuwa wana sura mbaya hawafai kufanya kazi ATCL sababu sio warembo

Ndugu yangu alilia sana akasema ina maana kazi ya u air hostess ni kwenda kujiuza sio kazi kama zingine?

Yeye alitakiwa tu kumnadi mgombea halafu akakae chini

Ashukuru Mimi na mihasira yangu sikuwepo hali ya hewa ingechafuka uvumilivu ungenishinda ashukuru Dk Magufuli ana huruma hadi kampa maiki Mimi ningempora na kumlamba makofi Yaliyobaki ningemwachia Magufuli aamue nini kifuate baada ya hali ya hewa kuchafuka
 
Nashoni huyu hyu tuliekuwane pale sua? mke wake alikuwa mwalimu Lupanga sc?
 
Hiyo kazi ya Serikali ndiyo wanakusanya kodi,tangu tupate uhuru bado tunawaza sijui Shule ,barabara nk alafu ndiyo zinakuwa agenda kwenye uchaguzi.

Kuna mahali ccm mshakwama , Mjitathimini kama bado mna uwezo wa kuongoza nchii hii.
A retarded economic growth due to selfishness of CCM.
 
kule uvinza alishaahidiwa cheo,angejikita tu katika kutafuta kura,kazi ya kusemea kero ni ya mgombea
 
kule uvinza alishaahidiwa cheo,angejikita tu katika kutafuta kura,kazi ya kusemea kero ni ya mgombea
Wewe akili yako yawaza cheo tuu,na si kutatua kero za wananchi!?
Pole sana mchumia tumbo wa mbogamboga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…