NANI ATAKUJA BAADA YA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI ITAKAPOTIMU MWAKA 2025?
Leo 13:15hrs 27/09/2020
Ni nani atakuja 2025 ili aweze kutupatia tokeo chanya la mradi wa ujenzi wa treni ya Umeme,reli ya kisasa SGR? Kwa sasa tunahitaji kuinua Uchumi wa Morogoro,Uchumi wa Tabora,Uchumi wa Kigoma,Uchumi wa Singida,Uchumi wa Shinyanga kwa kuwa na Uchumi unganishi toka Dar es Salaam kwenda Morogoro,kwenda Dodoma,kwenda Tabora,kwenda Kigoma,kwenda Singida,kwenda Shinyanga,katika hili tunahitaji kuwa na usafiri rahisi,salama,Uhakika,na wa haraka,hivyo basi bila kuwa na reli bora na ya kisasa hilo dhumuni halitafikiwa,sasa nani atakuja 2025 kutupatia tokeo chanya la treni ya Umeme kwa kutuletea Uchumi unganishi?
Nani atakuja Mwaka 2025 kutupatia tokeo chanya la Ujenzi wa meli kubwa tano katika ziwa Nyasa,Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika? Ujenzi wa meli hizo na upanuzi wa Bandari zetu,Bandari ya Dar es Salaam,Bandari ya Mtwara,Bandari ya Tanga,Bandari ya Kigoma,Uwepo wa Bandari hizi kubwa unavutia mizigo mingi itayokwenda katika nchi ya Malawi,Zambia,Zimbabwe,Rwanda,Burundi na Congo.Uwezo huu wa Bandari zetu kupokea mizigo mingi mikubwa inayokwenda katika nchi jirani isingekuwa rahisi kubaki tukitumia reli ya mkoloni kwa karne hii,Tunahitaji uharaka wa kufanya biashara na Uhakika wa usafiri kwa ajili ya kusafirisha mizigo ya wateja wetu toka bandarini hadi kwenye maeneo yao ya biashara.
Nani atakuja 2025 kutupatia tokeo chanya la Ujenzi wa bwawa kubwa la Umeme la mto Rufiji? Nani atakuja kutupatia tokeo chanya la Umeme wa uhakika utakaozalishwa na Bwawa la Julius Nyerere,Wilayani Rufiji? Uwepo wa Umeme wa uhakika na wa bei nafuu ni wazi kabisa utachochea kasi ya uwekezaji na ujenzi wa Viwanda,Umeme wa uhakika na wa bei nafuu ndio kichocheo kikuu cha Ujenzi wa Viwanda,Bwawa la Umeme la Julius Nyerere ,wilayani Rufiji litazalisha megawatt 2115, ni Mara mbili ya Umeme tunaotumia hivi sasa,Ni dhahiri kwa Umeme huu mwingi bei itapungua kwa maana Umeme wa ziada tutauuza nje ya nchi,Nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli atupe tokeo chanya la Ujenzi wa bwawa la Julius Nyerere?
Uwepo wa Umeme mwingi utafungua fursa kubwa ya uwekezaji ndani ya nchi yetu ya Tanzania,Ajira zitafunguka, Viwanda vitatengeneza ajira nyingi,watu wengi watakuwa kwenye nafasi ya kuajiriwa,ni muda sasa kila Mtanzania kufikiria wazo la kuanzisha kiwanda,watu wenye mashamba ya machungwa,machenza,korosho,matikitiki Maji,ni muda sasa kuanzisha Viwanda vya juice,watu wenye mashamba ya mahindi na mpunga ni muda sasa kuanzisha Viwanda vya unga na mchele na kuuza ndani na nje ya Tanzania,Umeme ni kila kitu katika uwekezaji,gharama za uwekezaji wa kitu chochote zinapungua kama Umeme ni wa uhakika na wa bei nafuu,
Watu wenye biashara za samaki,vinywaji baridi na moto,salooni,Viwanda vya magari,kuchomelea na kupaka rangi,Viwanda vya mbao,wote watanufaika sana na Umeme wa uhakika na bei nafuu, Morogoro kuna Mbuga ya Mikumi,Dar es Salaam hakuna Mbuga na Mbuga nzuri kwao na ya karibu ni Mikumi National Park iliyopo Morogoro,kwa hiyo fursa kwa wanamorogoro kupokea wageni pale Kihonda,wanaokuja na treni ya Umeme SGR na kuwapeleka Mikumi National Park, wanamorogoro mambo ya kuchukua mbwa wako kumpeleka Mikumi kumpandisha kwa cheetah au mbwa mwitu yaishe,ni muda wa kufanya biashara,anzisheni Tours,nunue Coaster chukueni watalii Morogoro Mjini,wapelekeni Mikumi National Park.
Nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli atujengee Viwanda baada ya Rais Magufuli kujenga bwawa la Umeme? Uwepo wa Viwanda vikubwa na vidogo kadhalika vitatoa fursa kwa Watanzania kuuza bidhaa zao na hasa malighafi kama nyanya,mahindi,viazi,mihogo,korosho,mananasi,machungwa,machenza,malimao,maaple,madaransi nk. Hii itasaidia kuinua Uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,tunatakiwa tuzalishe,tutengeneze na kula sisi wenyewe,kilimo kinatakiwa kitupatie ajira za aina tatu,kwanza kilimo kitupatie ajira ya kulima,zao la kilimo litupatie ajira viwandani, tutengeneze,juice,chakula,sukari na bidhaa hizo zitupe ajira nyingine ya biashara ndani na nje ya nchi,
Bila kusahau hata sasa miradi hii mikubwa inavyoendelea wapo watu wengi wameajiriwa, kuajiriwa kwao katika mradi wa treni ya Umeme na mradi wa Bwawa la Umeme unafanya pesa kuzunguka toka kwa mfanyakazi hadi kwa Mama ntilie anapokwenda kula hadi kwa mwenye duka anapokwenda kununua mchele na mwisho wa siku mwenye duka analipa kodi,kwa hiyo pesa ya mradi inarudi hata katika kipindi hiki wakati Ujenzi wa mradi ukiendelea kwa kukusanya kodi,kiuhasibu itaonekana tunatumia fedha nyingi kujenga miradi lakini kiuchumi tunapata faida kubwa kutokana na miradi hiyo,kwa maana miradi itatengeneza ajira,watu watalipwa watazungusha hela waliyolipwa katika mzunguko wa fedha na Serikali itapata kodi,
Nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli kulisimamia shirika letu la ndege la Atcl?Tangu mwaka 1977 baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki,nchi yetu ilikuwa na shirika la ndege linalosua sua na linalojiendesha kihasara kubwa,Mara baada ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kuingia, imefanikiwa kununua ndege mpya 11, Boeing,Airbus, Bomberdier,kufufuliwa kwa shirika letu la ndege kumetupatia heshima kama Taifa,tumewahi kukodi ndege mbovu,tumewahi kukodi ndege huku zikionekana zipo nchi nyingine zinapakwa rangi nyingine na kutumiwa na mtu mwingine,tumewahi kukatwa kodi na nchi tulizokodisha ndege badala ya kodi kuingia Tanzania,zilikwenda kwenye nchi hizo nyingine,
Wale baadhi wanaosema ndege si kipaumbele wala muhimu kwa Watanzania inabidi watambue Leo hii makusanyo ya mapato ndani ya Shirika la ndege ATCL ni zaidi ya sh Bilioni 4.5. na watalii wanaokuja na ndege hizo wameongeza mapato Tanapa na Mwaka uliopita Tanapa wametoa gawio la tsh Bilioni 650,ikiwa ni ongezeko la Watalii baada ya kununuliwa ndege kwa shirika letu la ndege la Atcl, kwa hiyo hii ndio faida ambayo watanzania tumeipata kwa Uwepo wa Rais John Pombe Magufuli,Je nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli ili aendeleze shirika hili la ndege la Atcl?
Nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli kutupatia tokeo chanya la Ujenzi wa bomba la Mafuta,Rais John Pombe Magufuli amefanikisha vilivyo kushirikiana na nchi ya Uganda kujenga Bomba la Mafuta linalotoka Hoima, nchini Uganda mpaka Chongoleani,mkoani Tanga nchini Tanzania, Ujenzi huo wa bomba la mafuta utazalisha ajira nchini na utaongeza pato la Taifa,Hayo yote yamefanikiwa kutokana na Serikali ya Rais John Pombe Magufuli kuzidi kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na nchi nyinginezo,miaka ya nyuma tulikuwa na shirika la Mafuta la tiper likafa lakini Rais John Pombe Magufuli ametuletea Mafuta kwenye bomba toka Uganda,Malori toka Rwanda,Burundi,Congo,Malawi,Zambia na Zimbabwe yatafunga safari kwenda Tanga kununua Mafuta,Je nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli atuletee tokeo chanya la Ujenzi wa bomba la Mafuta toka Uganda?
Nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli kutuletea tokeo chanya la uwazi wa taarifa na udhibiti wa rasilimali za nchi?Tumeshuhudia Serikali ikiweka uwazi kwenye mikataba ya madini na rasilimali zetu nyingine za taifa,Rais John Pombe Magufuli alifanikisha kuwekwa kwa makubaliano mapya yenye tija kwa Taifa la Tanzania,mathalani kwenye sekta ya madini ya Tanzanite,Almasi na dhahabu,tumeona tulivyokuwa tunaibiwa na wawekezaji,Sasa Serikali imeweka mikakati mipya ya kutokuibiwa tena,kama haitoshi tumeshuhudia wawekezaji wakibanwa vilivyo juu ya mikataba isiyokuwa na tija kwa Taifa,
Ni Serikali ya Rais Magufuli iliweka uthubutu wa kuwabana wawekezaji wa madini wa ACACIA iliyozaa Kampuni mpya ya Twiga na matunda yameonekana kwa Watanzania, Serikali ya Tanzania sasa inamiliki asilimia 16 ya hisa katika makampuni ya uchimbaji wa madini,na Sasa Serikali inapata gawio la faida ya madini ya asilimia 50 kwa 50,yote haya yamewezekana kwa sababu ya uzalendo wake Rais John Pombe Magufuli,Je nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli alinde rasilimali za Watanzania na kutupatia tokeo chanya la kutengeneza ajira kutokana na rasilimali zetu,ajira zitakazoinua kipato cha Mtanzania mmoja mmoja?
Nimalizie kwa kusema nani atakuja Mwaka 2025 baada ya Rais John Pombe Joseph Magufuli ambaye kwetu Watanzania,Rais John Pombe Magufuli ni mrithi wa kweli wa Mwalimu Julius Nyerere mwenye nia ya dhati ya kulikomboa kiuchumi,Taifa la Tanzania? Tulimuhitaji Mzalendo mfano wa Mwalimu Julius Nyerere na tukampata Rais John Magufuli ambaye ameondoa misheni town,ubadhirifu,dilidili,konakona,tumempata Rais John Pombe Joseph Magufuli kama mrithi wa dhati wa Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere,ambaye hakuwa mbinafsi,hakuwa wa kujilimbikizia mali,aliyeishi maisha ya kawaida licha ya kuwa Rais kwa miaka 23,Tunapompata mrithi huyu wa kweli wa Mwalimu Julius Nyerere, Watanzania tunapaswa kuomba tumpate John Pombe Magufuli mwingine baada ya muhula wa pili wa Rais John Pombe Magufuli kumalizika Mwaka 2025,Mungu mbariki Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Mungu mbariki Rais wetu Daktari John Pombe Magufuli,Mungu ibariki Tanzania.
Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.
-Research; Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.