Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Atapenyea wapi kaumiza Makundi yote ya wapiga kura, Askari ajawaongezea mishahara wanamsubiria wanyooshe acheki watakavyomgeuka utii wa kwenye gwanda sio utii wa ndani
 

Attachments

  • FB_IMG_1600852759286.jpg
    FB_IMG_1600852759286.jpg
    27.7 KB · Views: 1
CCM na wanaokifuasa ni laana kwa nchi.

Ni mikosi.

2020 tukatae ccm na wagombea wake kwa ngazi zote. chama kishazeeka wanaokishabikia nyakati hizi ni wana maslahi binafsi tu kwa kuwa wana ile imani ya kipuuzi kuwa ccm wanamiliki na kuvipelekesha vyombo ya ulinzi na usalama.

tarehe 28 piga spana kuanzia magufuli na vigaranga wake wote. hii nchi ni yetu sote tumeamua sasa hatutaki tena jinamizi linaloitwa ccm.
 
Walioko na wanaogombea CCM ni wasaka tonge tu wala hawana uchungu na WANANCHI na ndio maana wametuletea Sheria za ajabu sana za MAFAO wakati wenyewe washachukua chao ni UBINAFSI WA HALI YA JUU SANA. WOTE MBWA TUU.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
ccm na wanaokifuasa ni laana kwa nchi.

ni mikosi.

2020 tukatae ccm na wagombea wake kwa ngazi zote. chama kishazeeka wanaokishabikia nyakati hizi ni wana maslahi binafsi tu kwa kuwa wana ile imani ya kipuuzi kuwa ccm wanamiliki na kuvipelekesha vyombo ya ulinzi na usalama.

tarehe 28 piga spana kuanzia magufuli na vigaranga wake wote. hii nchi ni yetu sote tumeamua sasa hatutaki tena jinamizi linaloitwa ccm.
Nashauri wawachague Mawakala wa Waoiloni na wazee wa michango. Hivi nyie Chadema mnahielewa kweli
 
Muda huu ungetumia kujenga upendo kwenye familia yako badala ya kuwaza utopolo tu na kuilaumu serikali badala ya kupanga mipango ya kutoboa kimaisha.
 
Muda huu ungetumia kujenga upendo kwenye familia yako badala ya kuwaza utopolo tu na kuilaumu serikali badala ya kupanga mipango ya kutoboa kimaisha..
unapanga mipango chini ya serikali fulani fulani na in this case serikali yetu haieleweki.
 
TUWAAMBIE UKWELI WATANZANIA WENZETU JUU YA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO

_Anaandika Patrick Myovela_
_Mwandishi wa vitabu Tanzania._

Tukiwa tumebakiwa na siku 30 mkononi za kukamilisha kampeni za uchaguzi mkuu wa Tanzania, tumekwisha sikiliza kwa kiasi kikubwa sera za wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi kwa kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani. Baada ya hapo tuna siku moja tu ya kufanya maamuzi sahihi na ya msingi kwa mustakabali na ustawi wa Taifa letu la Tanzania kwa kuwachagua viongozi sahihi na wenye moyo wa kuliletea maendeleo makubwa Taifa hili.

Ni ukweli ulio wazi kuwa mbali na kuwepo kwa chaguzi nyingi kuu katika nchi mbalimbali duniani, macho mengi na masikio yameelekezwa kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania. Uchaguzi ambao umevuta hisia kubwa kwa watu wengi wa ndani na hata nje ya nchi.

Katika kuelekea uchaguzi huu mkuu wa mwaka 2020 wa Tanzania imekuwa bahati mbaya naweza kusema ama makusudi ya baadhi ya wagombea kusimama majukwaani na kufanya upotoshaji wa kimaelezo juu ya miradi ya maendeleo ambayo imefanyika na inayoendelea kufanyika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kile kijacho.

Makala hii leo hii inajikita kutoa maelezo ya manufaa ya baadhi ya miradi ya maendeleo ambayo Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikiitekeleza kwa lengo la kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakua kwa kasi na kufikia malengo yake ya kuingia katika uchumi wa kati.

Nchi zote duniani zimefanya kazi kubwa sana ya kuhakikisha kuwa zinakuwa na miundo mbinu imara na ya kisasa kwasababu hiyo ndiyo ni chanzo cha maendeleo ya kiuchumi na kwa upande mwingine ndiyo chanzo cha ukuaji wa kiuchumi.

Ni kwanini Tanzania tulihitaji kuwa na mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR? Kwa sasa tunahitaji kuwa na uchumi unganishi toka DSM kwenda Morogoro na kwingineko. Katika hili tunahitaji kuwa na usafiri rahisi, salama, uhakika na wa haraka. Hivyo basi bila kuwa na reli bora na ya kisasa hilo dhumuni litafikiwa kwa kusuasua sana. Na kama taifa hatuwezi kuendelea kujisifu kupata muunganiko huo kwa kutumia reli za kizamani zilizojengwa na mkoloni kwa ajili ya kutimiza malengo yake ya kinyonyaji.

Lazima ikumbukwe kuwa uwepo wa bandari ya DSM na uwezo wake wa upokeaji mizigo mingi inayokwenda mpaka mataifa jirani isingekuwa rahisi kubaki tukitumia reli ya mkoloni kwa karne hii. Tunahitaji uharaka na uhakika wa usafiri kwa ajili ya kusafirisha mizigo ya wateja toka bandarini mpaka kwenye maeneo yao ya biashara, soko na kwenye maeneo ya uzalishaji. Hivyo basi kazi ya reli ya kisasa (SGR) itakuwa ni kuunganisha lango la bidhaa la bandari ya DSM na maeneo mengine ya pembezoni mwa Tanzania kama ya nchi jirani na hata nje ya bara la Afrika. Hili lipo wazi kwasababu nchi nyingi za jirani zimekuwa zikitumia bandari ya Dar es Salaam kwa shighuli zao nyingi za kutoa ama kuingiza bidhaa zao.

Hakika kwa kuwepo kwa reli hii kutayapanua maeneo mengi kiuchumi, itakuza uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja, itachochea uwekezaji katika viwanda, itachocheana ushindani wa bandari, itapinguza gharama za usafirishaji na kuongeza wigo mpana wa usafirishaji wa bidhaa mbalimbali.

Zaidi ifahamike kuwa uwepo wa reli hii na uharaka wake itasaidia pia kufungua fursa za wawekezaji kwenda kwenye maeneo mbalimbali yatakayokuwa yakifikiwa na reli hii. Mathalani maeneo yatakayokuwa na vituo kama Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere na Morogoro yatatoa fursa kubwa kwa wawekezaji wadogo na wakubwa kuweza kufanya shughuli zao kwa uhakika. Watu wa benki, Maduka makubwa, hoteli, migahawa, zahanati nk watanufaika sana. Na kupitia wao ajira nyingi pia zitapatikana kwa Watanzania wenzetu. Hapo ukiachia faida ya jumla itakayopatikana kutokana na Serikali kukusanya kodi na kuboresha huduma nyingine za msingi kama elimu, afya, maji nk.

Tukiachana na reli ya kisasa ya SGR tutupie jicho suala la ununuzi wa ndege. Kwa miaka mingi Taifa lilikuwa kwenye sintofahamu ya kutegemea ndege moja kwa ajili ya kuendesha shirika lake la ndege. Hii ilikuwa ni aibu kwa Taifa lenye rasilimali nyingi na za kipekee ukilinganisha na mataifa mengine. Kwa kupitia mikakati kabambe ya Serikali ya awamu ya tano ndege 11 zimepatikana. Kati ya hizo ndege 8 zimekwisha wasili na kufanya safari zake mpaka nchi za India, Comoro, Afrika ya Kusini na China. Hii ni hatua kubwa na ya kusifika.

Kupitia kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu kumekuwa na upotoshaji mkubwa na wa wazi juu ya uwepo wa ndege hizi. Na hili linafanyika makusudi kwa kutokutaka kuwapa Watanzania wenzetu maarifa ya msingi juu ya ukweli na faida ya uwepo wa ndege hizi.

Kwa kuangalia kipengere kimoja tu cha faida ya biashara ya Utalii nadhani wale wote wanao potosha faida ya uwepo wa ndege hizi ilitosha kuwafunga midomo. Ni aibu kuwauliza Watanzania wenzako ndege zina faida gani kwenu wakati unajua wazi uwepo wa mnyororo wa thamani utokanao na safari za anga zilizo salama na za uhakika wa kuwaleta watalii.

Mtalii yeyote yule duniani mpaka akafikie maamuzi ya kutembelea vivutio vya utalii ni lazima kwanza ajihakikishie uhakika na usalama wa usafiri wa kumfikisha huko aendako. Na wengi huepuka masuala ya kuunganisha ndege ili kutokuwa na bajeti kubwa ya usafiri katika safari zao. Sasa katika hili Serikali ya awamu ya tano imelitibu kwa kuwapa uhakika watalii kupata usafiri ulio salama kutoka walipo hadi nchini Tanzania.

Inatia aibu sana kama Taifa kuwa na vivutio vikubwa vya utalii na vyenye kuliingizia taifa mapato makubwa huku mkiwa mnategemea usafiri wa kuwaleta watalii kupitia mataifa mengine. Zaidi uwepo wa watalii nchini hunufaisha wengi kuanzia wamiliki wa hoteli, wabeba mizigo, wauzaji wa bidhaa mbalimbali, kina mama lishe, watu wenye kampuni za magari nk. Hawa wote wanafurahia mnyororo huu wa thamani kwasababu ya Serikali kuweza kuwaleta watalii ambao wasingeweza kuwapa ushawishi wa kuja kwa wingi bila ya kuwepo kwa usafiri wa uhakika wa ndege.

Umeme wa uhakika kupitia mradi wa Stieglers Gorge ni moja ya hitaji kubwa sana tunalohitaji kama Taifa. Na hii ni kwa faida yetu kama wananchi na kwa wawekezaji. Uwepo wa umeme wa uhakika na wa bei nafuu ni wazi kabisa kuwa utachagiza na kuchochea kasi ya uwekezaji kuanzia viwanda vidogo, vya kati na vikubwa. Kwa kufungua fursa ya uwekezaji ndani ya nchi ni wazi kuwa watu wengi watakuwa kwenye nafasi ya kujiajili na kuajliwa. Watu wenye biashara za samaki, vinywaji baridi na moto, saloon, kuchomelea, viwanda vya mbao nk watanufaika sana na umeme wa bei ndogo na ulio wa uhakika.

Uwepo wa viwanda vikubwa na vidogo kadhalika vitatoa fursa kwa Watanzania kuuza bidhaa zao na hasa malighafi kama nyanya, mahindi, viazi, mihogo, korosho, mananasi nk. Hii itasaidia kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Bila kusahau ni lazima Watanzania wafahamu kuwa katika utekelezaji wa mradi huu wapo wenzetu wengi waliopata ajira zinazowasaidia kupata kipato cha kujikimu na maisha yao.

Mwisho kabisa nizingumzie suala la miradi ya flyovers za Ubungo na Tazara. Hii nayo ni hatua kubwa sana na kupongezwa kwa Serikali ya awamu ya tano. Haiingii kichwani hasa kwa kipindi hiki cha kampeni unapomsikia mgombea akiomba kura kwa wananchi walio nje ya jiji la DSM huku ukiwauliza ninyi mnafaidika nini na fly overs za Ubungo na Tazara? Kwanini Wasiulizwe wakazi wa jiji la DSM na hasa wa maeneo yanayolazimika kuvuka makutano hayo? Kimsingi nchi zilizopiga hatua kimaendeleo zimepambana sana kuondokana na suala la foleni za magari barabarani. Foleni hizi hupunguza muda wa watu wa kufanya kazi na kuzalisha kwa ajili yao na taifa.

Ni lazima ikumbukwe kuwa mapato ya jiji la DSM ni makubwa kuliko jiji lolote lile Tanzania. Na mapato yake huchangia kwa kiasi kikubwa Serikali katika uendeshaji wa shughuli zake. Hebu tuone mfano huu tu wa makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 kwa Ilala (44,505,151,623, Temeke 29,409,221,122 na Kinondoni 29,754,382,565) haya ni mapato kabla ya kukamilika kwa miradi ya ubungo na Tazara. Pia haya ni mapato ambayo yamepatikana huku foleni na msongamano ukiwa mkubwa. Je vipi baada ya kufunguka na kuondoka kwa msongamano?

Ni kosa kubwa kutokufahamu kuwa maeneo yanayo vuka maungano ya Ubungo na Tazara upeleka watu wengi kwenye maeneo yaliyo nyeti kwa shughuli za uzalishaji viwandani, bandari, biashara (kariakoo na posta nk)

Zaidi ni bahati mbaya kuwa hatutaki kufanya tathimini kwa kilichokuwa kikipotea kwa watu kukaa masaa zaidi ya matatu kwenye foleni na kuchelewa kufika maeneo yao ya kazi. Pia watu watambue kuwa kwa kuondoa msongamano maeneo ya makutano kutafungua fursa ya uwekezaji kwenye maeneo yanayofikika kirahisi na kufanya watu wapate ajira na kuinua pato la taifa na lile binafsi kiuchumi.

Nimalizie kwa kusema hivi; katika mbio za kutafuta uongozi wa nchi uongo na upotoshaji si silaha ya kufika kule tunakokutaka. Sera za wagombea zijikite kuonesha ni nini hasa mnachotaka kuwafanyia Watanzania kwa miaka mitano ijayo.

Niwatakie kampeni njema na zenye busara.
_____________________

_*Patrick Myovela*_
Mwandishi wa vitabu Tanzania.
+255 765 475 941
 
NANI ATAKUJA BAADA YA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI ITAKAPOTIMU MWAKA 2025?

Leo 13:15hrs 27/09/2020

Ni nani atakuja 2025 ili aweze kutupatia tokeo chanya la mradi wa ujenzi wa treni ya Umeme,reli ya kisasa SGR? Kwa sasa tunahitaji kuinua Uchumi wa Morogoro,Uchumi wa Tabora,Uchumi wa Kigoma,Uchumi wa Singida,Uchumi wa Shinyanga kwa kuwa na Uchumi unganishi toka Dar es Salaam kwenda Morogoro,kwenda Dodoma,kwenda Tabora,kwenda Kigoma,kwenda Singida,kwenda Shinyanga,katika hili tunahitaji kuwa na usafiri rahisi,salama,Uhakika,na wa haraka,hivyo basi bila kuwa na reli bora na ya kisasa hilo dhumuni halitafikiwa,sasa nani atakuja 2025 kutupatia tokeo chanya la treni ya Umeme kwa kutuletea Uchumi unganishi?

Nani atakuja Mwaka 2025 kutupatia tokeo chanya la Ujenzi wa meli kubwa tano katika ziwa Nyasa,Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika? Ujenzi wa meli hizo na upanuzi wa Bandari zetu,Bandari ya Dar es Salaam,Bandari ya Mtwara,Bandari ya Tanga,Bandari ya Kigoma,Uwepo wa Bandari hizi kubwa unavutia mizigo mingi itayokwenda katika nchi ya Malawi,Zambia,Zimbabwe,Rwanda,Burundi na Congo.Uwezo huu wa Bandari zetu kupokea mizigo mingi mikubwa inayokwenda katika nchi jirani isingekuwa rahisi kubaki tukitumia reli ya mkoloni kwa karne hii,Tunahitaji uharaka wa kufanya biashara na Uhakika wa usafiri kwa ajili ya kusafirisha mizigo ya wateja wetu toka bandarini hadi kwenye maeneo yao ya biashara.

Nani atakuja 2025 kutupatia tokeo chanya la Ujenzi wa bwawa kubwa la Umeme la mto Rufiji? Nani atakuja kutupatia tokeo chanya la Umeme wa uhakika utakaozalishwa na Bwawa la Julius Nyerere,Wilayani Rufiji? Uwepo wa Umeme wa uhakika na wa bei nafuu ni wazi kabisa utachochea kasi ya uwekezaji na ujenzi wa Viwanda,Umeme wa uhakika na wa bei nafuu ndio kichocheo kikuu cha Ujenzi wa Viwanda,Bwawa la Umeme la Julius Nyerere ,wilayani Rufiji litazalisha megawatt 2115, ni Mara mbili ya Umeme tunaotumia hivi sasa,Ni dhahiri kwa Umeme huu mwingi bei itapungua kwa maana Umeme wa ziada tutauuza nje ya nchi,Nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli atupe tokeo chanya la Ujenzi wa bwawa la Julius Nyerere?

Uwepo wa Umeme mwingi utafungua fursa kubwa ya uwekezaji ndani ya nchi yetu ya Tanzania,Ajira zitafunguka, Viwanda vitatengeneza ajira nyingi,watu wengi watakuwa kwenye nafasi ya kuajiriwa,ni muda sasa kila Mtanzania kufikiria wazo la kuanzisha kiwanda,watu wenye mashamba ya machungwa,machenza,korosho,matikitiki Maji,ni muda sasa kuanzisha Viwanda vya juice,watu wenye mashamba ya mahindi na mpunga ni muda sasa kuanzisha Viwanda vya unga na mchele na kuuza ndani na nje ya Tanzania,Umeme ni kila kitu katika uwekezaji,gharama za uwekezaji wa kitu chochote zinapungua kama Umeme ni wa uhakika na wa bei nafuu,

Watu wenye biashara za samaki,vinywaji baridi na moto,salooni,Viwanda vya magari,kuchomelea na kupaka rangi,Viwanda vya mbao,wote watanufaika sana na Umeme wa uhakika na bei nafuu, Morogoro kuna Mbuga ya Mikumi,Dar es Salaam hakuna Mbuga na Mbuga nzuri kwao na ya karibu ni Mikumi National Park iliyopo Morogoro,kwa hiyo fursa kwa wanamorogoro kupokea wageni pale Kihonda,wanaokuja na treni ya Umeme SGR na kuwapeleka Mikumi National Park, wanamorogoro mambo ya kuchukua mbwa wako kumpeleka Mikumi kumpandisha kwa cheetah au mbwa mwitu yaishe,ni muda wa kufanya biashara,anzisheni Tours,nunue Coaster chukueni watalii Morogoro Mjini,wapelekeni Mikumi National Park.

Nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli atujengee Viwanda baada ya Rais Magufuli kujenga bwawa la Umeme? Uwepo wa Viwanda vikubwa na vidogo kadhalika vitatoa fursa kwa Watanzania kuuza bidhaa zao na hasa malighafi kama nyanya,mahindi,viazi,mihogo,korosho,mananasi,machungwa,machenza,malimao,maaple,madaransi nk. Hii itasaidia kuinua Uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,tunatakiwa tuzalishe,tutengeneze na kula sisi wenyewe,kilimo kinatakiwa kitupatie ajira za aina tatu,kwanza kilimo kitupatie ajira ya kulima,zao la kilimo litupatie ajira viwandani, tutengeneze,juice,chakula,sukari na bidhaa hizo zitupe ajira nyingine ya biashara ndani na nje ya nchi,

Bila kusahau hata sasa miradi hii mikubwa inavyoendelea wapo watu wengi wameajiriwa, kuajiriwa kwao katika mradi wa treni ya Umeme na mradi wa Bwawa la Umeme unafanya pesa kuzunguka toka kwa mfanyakazi hadi kwa Mama ntilie anapokwenda kula hadi kwa mwenye duka anapokwenda kununua mchele na mwisho wa siku mwenye duka analipa kodi,kwa hiyo pesa ya mradi inarudi hata katika kipindi hiki wakati Ujenzi wa mradi ukiendelea kwa kukusanya kodi,kiuhasibu itaonekana tunatumia fedha nyingi kujenga miradi lakini kiuchumi tunapata faida kubwa kutokana na miradi hiyo,kwa maana miradi itatengeneza ajira,watu watalipwa watazungusha hela waliyolipwa katika mzunguko wa fedha na Serikali itapata kodi,

Nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli kulisimamia shirika letu la ndege la Atcl?Tangu mwaka 1977 baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki,nchi yetu ilikuwa na shirika la ndege linalosua sua na linalojiendesha kihasara kubwa,Mara baada ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kuingia, imefanikiwa kununua ndege mpya 11, Boeing,Airbus, Bomberdier,kufufuliwa kwa shirika letu la ndege kumetupatia heshima kama Taifa,tumewahi kukodi ndege mbovu,tumewahi kukodi ndege huku zikionekana zipo nchi nyingine zinapakwa rangi nyingine na kutumiwa na mtu mwingine,tumewahi kukatwa kodi na nchi tulizokodisha ndege badala ya kodi kuingia Tanzania,zilikwenda kwenye nchi hizo nyingine,

Wale baadhi wanaosema ndege si kipaumbele wala muhimu kwa Watanzania inabidi watambue Leo hii makusanyo ya mapato ndani ya Shirika la ndege ATCL ni zaidi ya sh Bilioni 4.5. na watalii wanaokuja na ndege hizo wameongeza mapato Tanapa na Mwaka uliopita Tanapa wametoa gawio la tsh Bilioni 650,ikiwa ni ongezeko la Watalii baada ya kununuliwa ndege kwa shirika letu la ndege la Atcl, kwa hiyo hii ndio faida ambayo watanzania tumeipata kwa Uwepo wa Rais John Pombe Magufuli,Je nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli ili aendeleze shirika hili la ndege la Atcl?

Nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli kutupatia tokeo chanya la Ujenzi wa bomba la Mafuta,Rais John Pombe Magufuli amefanikisha vilivyo kushirikiana na nchi ya Uganda kujenga Bomba la Mafuta linalotoka Hoima, nchini Uganda mpaka Chongoleani,mkoani Tanga nchini Tanzania, Ujenzi huo wa bomba la mafuta utazalisha ajira nchini na utaongeza pato la Taifa,Hayo yote yamefanikiwa kutokana na Serikali ya Rais John Pombe Magufuli kuzidi kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na nchi nyinginezo,miaka ya nyuma tulikuwa na shirika la Mafuta la tiper likafa lakini Rais John Pombe Magufuli ametuletea Mafuta kwenye bomba toka Uganda,Malori toka Rwanda,Burundi,Congo,Malawi,Zambia na Zimbabwe yatafunga safari kwenda Tanga kununua Mafuta,Je nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli atuletee tokeo chanya la Ujenzi wa bomba la Mafuta toka Uganda?

Nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli kutuletea tokeo chanya la uwazi wa taarifa na udhibiti wa rasilimali za nchi?Tumeshuhudia Serikali ikiweka uwazi kwenye mikataba ya madini na rasilimali zetu nyingine za taifa,Rais John Pombe Magufuli alifanikisha kuwekwa kwa makubaliano mapya yenye tija kwa Taifa la Tanzania,mathalani kwenye sekta ya madini ya Tanzanite,Almasi na dhahabu,tumeona tulivyokuwa tunaibiwa na wawekezaji,Sasa Serikali imeweka mikakati mipya ya kutokuibiwa tena,kama haitoshi tumeshuhudia wawekezaji wakibanwa vilivyo juu ya mikataba isiyokuwa na tija kwa Taifa,

Ni Serikali ya Rais Magufuli iliweka uthubutu wa kuwabana wawekezaji wa madini wa ACACIA iliyozaa Kampuni mpya ya Twiga na matunda yameonekana kwa Watanzania, Serikali ya Tanzania sasa inamiliki asilimia 16 ya hisa katika makampuni ya uchimbaji wa madini,na Sasa Serikali inapata gawio la faida ya madini ya asilimia 50 kwa 50,yote haya yamewezekana kwa sababu ya uzalendo wake Rais John Pombe Magufuli,Je nani atakuja baada ya Rais John Pombe Magufuli alinde rasilimali za Watanzania na kutupatia tokeo chanya la kutengeneza ajira kutokana na rasilimali zetu,ajira zitakazoinua kipato cha Mtanzania mmoja mmoja?

Nimalizie kwa kusema nani atakuja Mwaka 2025 baada ya Rais John Pombe Joseph Magufuli ambaye kwetu Watanzania,Rais John Pombe Magufuli ni mrithi wa kweli wa Mwalimu Julius Nyerere mwenye nia ya dhati ya kulikomboa kiuchumi,Taifa la Tanzania? Tulimuhitaji Mzalendo mfano wa Mwalimu Julius Nyerere na tukampata Rais John Magufuli ambaye ameondoa misheni town,ubadhirifu,dilidili,konakona,tumempata Rais John Pombe Joseph Magufuli kama mrithi wa dhati wa Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere,ambaye hakuwa mbinafsi,hakuwa wa kujilimbikizia mali,aliyeishi maisha ya kawaida licha ya kuwa Rais kwa miaka 23,Tunapompata mrithi huyu wa kweli wa Mwalimu Julius Nyerere, Watanzania tunapaswa kuomba tumpate John Pombe Magufuli mwingine baada ya muhula wa pili wa Rais John Pombe Magufuli kumalizika Mwaka 2025,Mungu mbariki Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Mungu mbariki Rais wetu Daktari John Pombe Magufuli,Mungu ibariki Tanzania.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research; Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Polepole yuko mubashara Channel ten!

Karibu.

Up dates;

Dkt. Magufuli kesho 28/9 atakuwa na mkubwa wa kampeni mkoani Iringa katika uwanja wa Samora.

Tarehe 29/9 Dkt. Magufuli atakuwa na mkutano wa kihistoria katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Katika mikutano hii Dkt. Magufuli atajikita kwenye kuelezea maono yake na hatajibishana na wanasiasa wengine majukwaani.

Ratiba kamili baada ya Mbeya itatangazwa baadaye.
 
Back
Top Bottom