Salaam Wana JF.
Rais Magufuli ni kiongozi mwenye maono na aliyeonyesha uthubutu wa hali ya juu katika ya viongozi wa bara hili la Afrika, Uthubutu wake ni wa kimapinduzi na unaolenga kuwakomboa wananchi, Magufuli amethubutu kisiasa, kiuchumi na kijamii, ni kiongozi wa pekee kwa sasa anayeweza kusimama na kukemea "Ukoloni Mambo leo" Kwa maana ya unyonyaji wa mabeberu, Aidha Magufuli ni mjamaa na kiongozi anayeishi katika falsafa za kuwatumikia watu walio "Wanyonge" na Wanyonge ndio wengi, Maono ya Magufuli yapo wazi kwenye "COVID-19", "Mikataba ya Madini" na "Falsafa ya ufufuaji wa viwanda"
Kwa Mantiki hiyo Wananchi wana Kiburi cha kumchagua tena Dkt. Magufuli kwa miaka mingine mitano, kwa sababu nia na hoja za kufanya hivyo zipo wazi kulingana na matendo yake, Myonge myongeni lakini haki yake mpeni, tumpe mitano tena Dkt. Magufuli atende yaliyo mema zaidi kwa ustawi wa nchi na kizazi cha sasa na hapo badae.