Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Halafu kwa leo nadhani anasema uongo au amepewa takwimu ambazo si sahihi au ameamua kuupotosha umma kwa makusudi

amesema "alipoingia madarakani kulikua na vijiji 2,018 tu vyenye umeme, katika kipindi chake ameweka umeme vijiji 9,570
na Tanzania ina vijiji 12,284. Pia amesema ukijumlisha vijiji 9570 na vile vwa awali 2018, vijiji ambacvyo havina umeme ni 2000 na ushee"

hizi takwimu kazisema mara mbili leo Ikungi na Singida Mjini.

sasa hesabu zinakataa 9,570+2018 =11,588 Maana yake vijiji ambavyo havina umeme ni 696 tu (12284 - 11588). Hivyo tunaomba aseme takwimu sahihi au watu wake waje kurekebisha hizi number au mwenyewe arekebishe. Akiendelea kutosema takwimu sahihi hii itamuondolea credibility kwamba aidha yote semayo sio sahihi na kupoteza imani nae
 

..Mfumo wetu wa uendeshaji serikali lazima ubadilike.

..Wabunge [ Halmashauri ] wawe na sehemu yao ya kuleta maendeleo.

..Na Raisi [ serikali kuu] naye awe na sehemu yake ya kuleta maendeleo.

..Kwa hali ilivyo sasa hivi wananchi na wabunge wamekuwa OMBAOMBA mbele ya Raisi Magufuli.

..Hali imekuwa mbaya mpaka wakati wa mafuriko kuna mwananchi wamDsalaam aliamua kumlilia shida Raisi Magufuli kwa Kisukuma!!
 
Mbinu zake zote zimebainika kilichosalia ni kutafuta msaada wa kimataifa kuwadhibiti Tume ya uchaguzi wasifanye yale waliyopanga kuyafanya sasa kuwaibia kura vyama vya upinzani na kumjazia mgombea wa ccm.
 
Kwahiyo chadema mmeamua kumlipa chid benz laki moja na nusu au sio?
 
Nanyie wabongo acheni kulalamika mkiambiwa uzazi wa mpango mnasema Mara Freemason hao mara new world order! Mkiambiwa mzae napo mnalalamika sasa mnataka nini?
Tusiambiwe kila mtu ataamua mwenyewe.
 
Tumhurumie tu. Amejisahau. Anafikiri yeye ndiye kila kitu, na anaweza kufanya chochote. Bunge na mahakama vyote viko chini yake.
 

Magufuli hana uwezo na nafasi ya urais, ni mtu asiye sahihi kwenye nafasi ya urais. Hicho anachofanya sio sawa, ila kwakuwa katiba ina mapungufu ya kumfanya rais afanye chochote atakacho, ndio anadhani kupeleka maendeleo mahali ni mapenzi yake. Kwasababu ya hiyo tabia yake binafsi, hapo ndio watu wanajipendekeza ili haki yao awafanyie hisani.
 
Magufuli amekuwa mbunge kwa miaka mingi sana lakini ana uelewa mfupi kuhusu majukumu ya mbunge, sijui kama hata huo urais alionao aliupata kihalali.
 

Sasa wewe katafute data za ukweli uweke hadharani, tuone kitakachokukuta!
 
Magufuli anaamini fedha zote za serikali ni mali yake na ana uwezo wa kuzitumia bila kupitia bungeni, ndiyo sababu amekuwa akichota fedha hazina na kuzitumia bila idhini ya Bunge. Full kuvunja sheria!
Huyu jamaa kwa kifupi hajielewi na viatu vya uongozi vinampwaya.
 
Sijaona popote tangu CCM wamezindua kampeni zao wakisema chochote kuhusu wafanyakazi wa umma.

Mishahara, madaraja, nyongeza n.k

Ni kama hakuna kitu kama hicho kwenye ilani yao.

Sawa.
Noma ... Hatari tupu.
 
Ndiyo maana inahitajika katiba mpya inayompa Meya wajibu wa maendeleo kwa ngazi zote za chini huku mbunge akiwa na wajibu wa kuyatolea taarifa Bungeni, na pia kila wilaya itumie pesa zake inazokusanya kuleta maendeleo eneo husika huku wakipeleka kiwango fulani Serikali kuu, siyo kuchukua pesa za makusanyo ya Songea kwenda kujenga chato, katiba mpya ije na mfumo wa Tawala za majimbo zenye magavana kama kenya, America, South Africa na sehemu zingine Duniani itazuia hii mbinu ya Rais kuonekana ndiye hutoa pesa za maendeleo pekee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…