Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Sijaona popote tangu CCM wamezindua kampeni zao wakisema chochote kuhusu wafanyakazi wa umma.

Mishahara, madaraja, nyongeza n.k

Ni kama hakuna kitu kama hicho kwenye ilani yao.

Sawa.
Na kwa kiburi hiki wafanyakazi wenye ndugu wanaowategemea wawahamasishe wafanye maamuzi sahihi maana wao ndio wanaumia
 
Wasanii kwetu ndiyo watu wa muhimu
Wengine subirini kwanza [emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
 
Kwa miaka mitano nimekuwa nikisikiliza hotuba za JPM hadi nikiwa nikimuona simfuatilii nikijua ni yale yale ya kila siku. Ndege zimekuwa ndege, mradi wa umeme, reli ya umeme, viwanda, mafisadi, barabara na kunuuunua kuku na mihindi njiani.

Nilishindwa kumfuatilia zaidi hasa pale alipoamua kwa nguvu zote mchana kweupeee kuwananga wapinzani na kuonyesha ubaguzi wa wazi. Alitamka wazi kuwa yeye hapeleki maendeleo kwenye majimbo ya wapinzani.

Kwa ubaguzi huu nikadhani alikuwa anaongea kisiasa kumbe alikuwa na dhamira ya kweli. Kuna siku, mama mmoja aliomba maji akaambiwa ana kiherehere na amuombe mumewe au mbunge na diwani wake aliyemchagua.

Leo yupo Ikungi anaomba ndugu wa Lissu na Lissu mwenyewe kura. Hakumbuki kwamba serikali yake ndiyo ilimunyima hela za matibabu, mshahara na kumfukuza kazi ya ubunge. Leo amejisahau.

Nilidhani atasema ni kwa nini hajatoa ajira, hajawajaongeza watumishi mishahara na kwa nini aliwaambia kuwa hakuchaguliwa ili aongeze mishahara? Mwisho niseme tu hakuna jipya ambayo nilisikia na leo ataongezea.
 
Ulimbukeni wa ajabu, uzuri Watanzania wajinga wanapungua.
Leo Ikungi kasema ... Mtaturu miezi michache kaniomba maji..... wengine walikuwa hawaombi..( Lissu) ..
Aibu na fedheha kwa wananchi toka kwa mtawala.
Aibu kwa kweli.
 
..huu ndio mtizamo ambao Magufuli ameujenga kwa muda mrefu, na amekuwa akipita kila mahali kusisitiza hilo.

..kwamba eneo husika kupata maendeleo raisi/magufuli ndiye muamuzi. Na asipojisikia, au asipokuwa na mahusiano mazuri na mbunge wa eneo hilo, basi hakuna maendeleo.

..kama anakusanya kodi kila mahali ktk nchi hii, basi miradi ya maendeleo igawanywe kulingana na mahitaji, na siyo raisi anajisikia vipi, au mbunge ana mahusiano gani na watawala.
Nasikia ukiwa mbunge wa upinzani maendeleo hawapati kwenye jimbo lako ili wananchi waone huna lolote
 
Mheshimiwa Dr. Magufuli Rais wa Tanzania tunaomba majibu yako juu ya hoja za wapinzani kuwa umeminya Uhuru na haki za Watanzania kwa maslahi yako binafsi na chama chako CCM. Chaguzi zilizopita wapinzani waliomba kura kwa wananchi kwa kuwaahidi maendeleo na kuahidi kupigana na ufisadi uliofanywa na viongozi wa CCM, lakini mwaka huu wapinzani wanaahidi maendeleo na kuwaahidi Uhuru na haki .
Hata makaburu wa south Africa walileta maendeleo ya juu sana, Mimi binafsi nimesoma A- level shule iliyojengwa na Wazungu, na O-level pia nimesoma shule iliyojengwa na Wazungu pia. Wakoloni pia walileta maendeleo kwa kiasi chao. Lakini akina Nyerere walidai Uhuru.
Jibu la maendeleo hayana chama halitutoshi sisi tunaojua historia. Sisi ambao tumesoma historia na kufaulu vizuri A- level tunajua jinsi Waingereza walileta maendeleo America lakini Waamerika hawajaruhusu US. liwe koloni la kudumu la Uingereza.
Tunaomba majibu ili wananchi wajue kuwa Uhuru na haki vipo kila mahali na zile za wapinzani ni kelele mfu .
 
Back
Top Bottom