Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Angejua black Tax tunayolipa inavyotuumiza wengine. Baba ana watoto nane na ametangulia anaacha mama na watoto wote hao. Unakuta ni wa kwanza peke yake ametoboa. Anakuwa na kazi ya kuwatunza wadogo zake 7 pamoja na mama. Kweli leo unatuambia tuzae wakati hata chama chako kimeshindwa kutoa ajira. mwisho wa siku ni kulana sisi kwa sisi na kuzalisha majambazi na ukahaba kuongezeka.
"Black tax" is a term used to describe young black people who share their salary with immediate and extended family.
 
Tuliposema amejipitisha kwa nguvu kwenda kumsaidia Magu kwenye kampeni hatukukosea

Sasa ni aibu tupu mkutano wa waziri mkuu kukosa watu kiasi hiki

Kumbe bila wasanii hata Magufuli Hana watu.


Ni aibu mwaka huu hata mama Samia naye kakosa watu kisa kulikuwa hakuna malori ya kuwasomba

IMG_20200901_181359.jpg
 
Tuliposema amejipitisha kwa nguvu kwenda kumsaidia Magu kwenye kampeni hatukukosea

Sasa ni aibu tupu mkutano wa waziri mkuu kukosa watu kiasi hiki

Kumbe bira wasanii hata Magufuli Hana watu.View attachment 1555613
Na bado ! halafu inasemekana huyu hata kwao watu hawamtaki kabisa , ndio maana wagombea wa vyama vingine walitekwa
 
Hayo ameyasema raisi Pombe, muda siyo mrefu kwenye kampeni zinazoendekea mkoani Singida, nanukuu.

"Elimu ni bure, wakinamama zaeni hakuna haja ya kupanga uzazi, matiti ya kunyonyesha mnayo, wanaume wa kuwapeni mimba wapo."

Toa maoni je ni kweli kupanga uzazi hakuna maana kama wataalamu wanavyo shauri, hii siyo mara ya kwanza Magufuli kuwaambia watanzania kuwa zaeni, msipange uzazi.
Kupanga uzazi ni mbinu ya mabeberu kupunguza idadi ya watu weusi duniani...
 
Mheshimiwa Dr. Magufuli Rais wa Tanzania tunaomba majibu yako juu ya hoja za wapinzani kuwa umeminya Uhuru na haki za Watanzania kwa maslahi yako binafsi na chama chako CCM. Chaguzi zilizopita wapinzani waliomba kura kwa wananchi kwa kuwaahidi maendeleo na kuahidi kupigana na ufisadi uliofanywa na viongozi wa CCM, lakini mwaka huu wapinzani wanaahidi maendeleo na kuwaahidi Uhuru na haki .
Hata makaburu wa south Africa walileta maendeleo ya juu sana, Mimi binafsi nimesoma A- level shule iliyojengwa na Wazungu, na O-level pia nimesoma shule iliyojengwa na Wazungu pia. Wakoloni pia walileta maendeleo kwa kiasi chao. Lakini akina Nyerere walidai Uhuru.
Jibu la maendeleo hayana chama halitutoshi sisi tunaojua historia. Sisi ambao tumesoma historia na kufaulu vizuri A- level tunajua jinsi Waingereza walileta maendeleo America lakini Waamerika hawajaruhusu US. liwe koloni la kudumu la Uingereza.
Tunaomba majibu ili wananchi wajue kuwa Uhuru na haki vipo kila mahali na zile za wapinzani ni kelele mfu .
Ukipata majibu naomba unishirikishe na mimi
 
Kila apambane na hali yake, anayeuza haki ya ushoga kwa kuita haki ya faragha aendelee na anayeuza sera za kuboresha miundombinu aendelee, wananchi tutamchagua mzalenda, kibaraka wa mabeberu tutamuachia aende kugombea Kenya na Belgium.
 
Mmambo ya kusomba wasanii nchi nzima , na kuhamisha watu kutoka dodoma, kupita manyoni hadi singida mjini... Kinachotakiwa ni lori tu kutoishiwa mafuta...
Wakitoka huko mwisho wa siku wanadai kudhulumiwa au kutolipwa...
Baadhi wamejilipa kwa ubunge
 
Back
Top Bottom