Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Nimeudhika sana; akiwa Singida kuna mpiga debe wake mmoja alisema yeye hawezi kulinganishwa na Kichuguu; nimekasirika sana na sasa nina mipango ya kwenda kumwuliza kwa nini hawezi kulinganishwa na mimi kujua kama ananiogopa au ananidharau.
 
Alisema lisu kibaraka, mara ghafla kabadilika sio kibaraka na anataka kumpa kazi ya kufanya, diiiiii
 
Kila anakoenda Magufuli kuna kundi kubwa la wasanii nyuma yake. Kundi hili hutumia muda mwingi zaidi kuburudisha kuliko wananchi kusikiliza Sera.

Hivyo nachelea kusema timu ya kampeni ya CCM iliona dalili ya mikutano yao kukosa kabisa watu hivyo wakaona njia ya pekee ni kushawishi kupitia wanamuziki.

Magufuli hajagusa maisha ya watu walio wengi kama wanavyoaminishwa, hakuna kundi lenye unafuu wa maisha. Bidhaa za chakula zimepanda maradufu, huduma za afya bado ni ghali, ajira zimedoda, maslahi ya watumishi hakuna, vifaa vya ujenzi ziko juu zaidi, ukilinganisha na kipindi cha Jakaya Kikwete, hakika ni aibu kubwa.

Bila wasanii ambao kimsingi ndiyo hujaza watu mikutano ingehudhuriwa na team yake ya kampeni.

Haki ya nyongeza ya mishahara ya watumishi ndiyo sasa wanatumia kulipa kundi kubwa la wasanii, zaidi ya 100.
 
Harufu ya upigaji tu, chama chakavu ndio kawaida kwao. Wakulima wanataka soko la uhakika wapate pesa sio silos za kuhifadhi mazao yao.
 
Wewe wacha kulewa umeme gani? mpaka leo miaka 60 ya utawala wa CCM kwenye bunge wanazungumzia matundu ya choo.
 
Harufu ya upigaji tu, chama chakavu ndio kawaida kwao. Wakulima wanataka soko la uhakika wapate pesa sio silos za kuhifadhi mazao yao.
mkuu ilo soko la uhakika si ndio serikali inayanunua wanayaweka humo then sudan wakikumbwa na njaa tunawauzia pamoja na kenya au iyo idea hujaipenda
 
Na watu wengine wanaenda kwenye viwanja kama hivyo kwa sababu hawana pa kwenda wanaona bora wakapoteze muda tu huko.
 
Naona unamtetea mpenda ngono mwenzio kwa nguvu kubwa sana
Ushauri wangu kwako ni kuwa: Anza Kwanza kumtamkia hivyo baba yako mzazi aliyekuzaa. Mwambie hivi: baba wewe ni mpenda ngono...jibu utakalopata kwa baba yako mzazi uje utueleze humu jf..
 
#MisigiriSingida

•Siwezi kuliacha
Taifa hili liangamie, likaingia mikononi mwa matapeli, watu waongo, nataka taifa hili niliache kwenye mikono salama•
 
Comment yako nimeipenda kwani imenionesha wewe ni mtu wa aina gani...awali ya yote jina lake la mwisho rais wetu ni Magufuli na siyo Magufuri...ni ajabu kwamba unashindwa hata kuandika kwa usahihi jina la kiongozi wetu mkuu wa nchi...halafu wakati unalalamika kuwa baadhi tuna obsession na JPM ni wazi wewe na wengine wachache mna 'negative obsession' na JPM...coming to the point...kufikiri kibeberu ni kuwaona viongozi wa Afrika kwamba ni wa hovyo, na kumuona mtu mweusi kuwa ni nothing..halafu pia kuwa na mawazo ya kibabe na arrogance kwa kujiona kuwa unajua Kila kitu na mwingine hajui na hasa ukiwa na chuki naye.. fikra za kibeberu ni fikra za supremacy na dharau...
Halafu Jambo jingine ni kuwa hakuna ukakasi wowote kwa kauli ya JPM. Alichosema Rais ni kuwa watu wazae...hakusema waende kufanya ngono...wanaosema hivyo ni wahuni na washenzi wachache wanaopotosha makusudi kauli ya JPM...Hakuna anayesema Rais au JPM hawezi kukosolewa...lakini kukosoa kwake kuwe kwa haki...Mimi binafsi yapo ninayoweza kumkosoa JPM..lakini nitafanya hivyo bila kupotosha kauli zake...
 
Ni wazi CCM imejipanga vyema ktk kampeni za uchaguzi wa mwaka huu 2020 kuliko 2015. Namuona Magufuli jinsi anavyo chanja mbuga Kanda ya Kati kuelekea Kanda ya Ziwa au magharibi, anapiga mikutano isiyo pungua 10 kwa siku!

Namuona Samia jinsi anavyo washa moto kanda ya Morogoro nadhani mwelekeo wa pwani.....boda tu boda

Namuona Majaliwa anakata mbuga Kanda ya Kaskazini, nadhani mwelekeo wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, kampeni ni kuwafikia wananchi walio wengi zaidi ktk maeneo yao na sio kuwakusanya ktk maeneo ya mijini.
 
Kampeni lazima afanye hasa ukitilia maani kuwa kuna watu kama wewe na akina Lissu ambao hamkubali kuwa wanayosema CCM wameyafanya. The strategy here ni kuyasema as many times as possible ili yawaingie na muamini kuwa waliyafanya kwani kwa macho hamtaki kuyaona, labda kwa masikio MTASIKIA. Pia ni kwa nia na lengo la kuwaeleza hawa DIASPORA NA WAKIMBIZI WA KISIASA kuwa kuna mambo yamefanyika na mengine mapya yanawekewa mikakati ya utekelezaji kama ilivyo kwenye CCM MANIFESTO or ILANI ambayo in your liking that is the Strategic Document from CCM Party Strategists.
 
Hahaha ukiangalia kampeni za ccm kutwa wanaimba, kuna clip iko kwenye main page ya JF kuna picha ya Magufuli, ukiifungua ni waimbaji mwanzo mwisho.

BASATA ikifanya kama TCRA iwazuie wasanii kushiriki siasa badala yake tuwasikie wagombea, ccm watatuambia hadi tausi wanavyotaga ikulu.
 
mimi sio mshabiki wa chama chochote ila nafuatilia tu kampeni za vyama vyote jinsi wanavyo pambana kutafuta kura....
kura ni kampeni na kampeni ni mipango ya kisayansi ya kutafuta kura nyingi
 
Zungukeni nchi nzima ila wananchi sisi hatuta wapigia kura Yani. Hatuwezi vumilia kufa njaa wakati nchi yetu ni tajiri, Kodi tunalipa, hafu mnaenda kununua ndege, kujenga barabara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…