Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Huo siyo ukweli ni ujinga na ulimbukeni wa madaraka .najuta kumpa kura yangu mwaka 2015
kikubwa umejua anakuwazia nini.

maana wagombea wa viti vya ubunge wana akili mbovu sana, yaani mtu unatukana serikali ambayo ukishapewa ridhaa na wananchi wako unatakiwa ukaiombe pesa za maendeleo jimboni kwako tena[emoji3][emoji3][emoji3].

kuna haja ya kubadiri namna ya kuangalia mambo. isiwe kisiasa zaidi bali lengo liwe kwenda mbele zaidi.
 
Ulichotaka kumaanisha katika aya yako ya mwisho ni kuwa kimetumika kisukuma kwakuwa kuna ahadi ambazo watu wasiojua kisukuma hawakutakiwa kujua au kusikia sababu watapata wivu ? Kwamba sera zetu haziuzi ila kushawishi kwa kuongea kilugha !? Kuwa kuna watanzania ambao leo 2020 hawajui kiswahili inabidi waambiwe kwa lugha zao, mgombea wetu akienda Mtwara, Tanga, Mbeya na maeneo mengine tutegemee atazungumza kwa lugha hizo ndiyo atakuwa na ushawishi, vinginevyo mgombea wetu hana ushawishi ?
Absurd! kuyasikia haya leo kutoka kwetu sisi wana CCM, kuwa kuna mwana CCM anaaminisha umma kuwa mgombea wetu hana ushawishi na hawezi kuuza ilani na sera zetu?! Anaweza kuuza lugha yake tu? Tena unaaminisha watu wakati wa campaign? Jambo la ajabu kabisa. CCM imeshinda kila chaguzi katika historia ya nchi yetu, sababu wagombea wetu wa urais ni watu wanaoweza kunadi na kuuza sera zetu na ilani yetu kwa wananchi, wameweza kueleza haya katika lugha rahisi kwa kila mpiga kura, bila kujali chama chake, dini, elimu, kabila, umri au kipato chake. Umeshindwa hata kueleza kuwa mh. Alikuwa akitoa salamu tuu kwa lugha mbalimbali na sera zote zilinadiwa kwa kiswahili!??
Ajabu kabisa ! Unasema bila uwoga, soni wala haya kuwa tunazungumza kilugha eti kwasabu hatuwezi kushinda kwa sera. Si kweli, ni uwongo, uliojaa chuki na wenye lengo la kusambaza chuki hii kwa wapiga kura. Ni matumaini yangu utajifikiria ulichokiandika dhidi ya chama cha mapinduzi na tuhuma ambazo umekipa chama kisirisiri na utarekebisha mara moja tuhuma hizo na uwongo, unafiki na uzandiki dhidi ya chama.
Kimsingi, Mh. Alisalimia tuu kwa kilugha na hakuna jipya wala si jambo geni, ni kama wanasiasa wanavyosalimia kwa salamu za dini.
 
Nakuhakikishia kuna wasukuma na wamasai Hawajui kuswahili

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Swala siyo nguvu ya ukawa. Hata rungwe anaishinda CCM.
Nguvu ya CCM iko kwenye tume yao ikisaidiana na vyombo vya usalama na mahakama. Nje ya hapo tarehe 28 mngeaga ikulu.
Hata mwaka 2015 hamkshinda ila CCM mlijitangaza washindi.
 
Kwa
Wivu tu. TZ ongea lugha yoyote. Utanaka tuwe tunaongea viingeleza Kama Ubelgiji?

Kusukuma ni Kanda ya Ziwa..

Mkikosa kabsa Sera mnataka Hadi watu waache kuwasiliana kwa ukaribu?

Mtu anaongea na watu wa Mwanza unataka hadi wewe uelewe?
kwani sheria za uchaguzi zinasemaje? tusinajsi akili zetu. ebu leteni sheria ya uchaguzi kuhusu lugha
 
Anaongea na wapiga kura wake na wanaelewa hiyo lugha, akija mkoani kwako ataongea kiswahili wala usiwaze, kikubwa naamini umeliona nyomi la watu
 
Mnakumbuka kale kakabila alikopewa john 2015 kwa kumficha kuwa sio msukuma!

Amesahau tz sio ya wasukuma
Jiwe bin Mwamba alizaliwa Bujumbura, akakulia Busubi (Biharamuro), lakini akapata bahati ya kujipachika Usukuma - ambao unaona anacheza nao kupitiliza. Muulize akuoneshe kaburi la babu yake!!!
 
Nyerere, mwinyi, mkapa, kikwete sijasikiaga lugha zao wala sijui ni makabila yao lakn huyu bwana huyu... Sijui tulimtoa wapi...
 
Hivi kila mgombea akianza kupiga kampeni kilugha, kikabila sielewi tutafika wap..
Hivi kinachowachanganya ni lugha aliyoitumia leo baada ya kuingia Mwanza au ni lile nyomi lililokuwa linazuia njia ili kipenzi chetu aseme nao japo neno japo moja
 
Kwanza wewe si mwanaCCM.

Pili lazima ukubali hakuna sera mbaya.. ikiweko hapa ilete niione.. tunachotofautiana ni uwezo was kuushawishi umma utuchague.. na Kama chama Cha Mapinduzi kinao msingi na mfumo Bora wenye ushawishi.

Tatu hakuna aliyetumia lugha ya asili mwanzo mpaka mwisho kufanya kampeni.. na maneno Kama Wasukuma wanasema..."insert Maneno hapa" hazijaanza kutumika leo kwenye siasa.

Tatizo ni kujiona hii Tanzania ni ya wasomi na Kiswahili kinaeleweka pote.. you are very mistaken"Mjuba" huifahamu Tanzania. Tembea Kisha urudi hapa useme Tena haya unayoyaandika.

Na hizi asili ndizo building blocks za Taifa Hili.. huwezi kupenda mchuzi (Uswahili) halafu ukachukia kitunguu na nyanya(makabila ya kibantu) utakuwa hayawani.

Siasa Duniani kote zinaendeshwa namna moja.. iwe Marekani iwe Uingereza iwe Urusi Japan kote... Ni jukumu la mwanasiasa kuconnect on individual level na wapiga kura..

Huko walikoendelea wasingesafiri na kufanya mikutano ya hadhara.. wangekaa kwenye tv wakazisoma sera na kuzidadavua kwa undani kabisa if that wa simple as you put it.

Running a country is one thing and getting elected is another.. Waacheni wenye ujuzi na hayo wafanye kazi yao.

Btw..sheria inaruhusu lugha hizi kitumika pale inapohitajika na mkalimani awepo.. Sasa Dr. JPM anahitaji mkalimani gani wakati yeye mwenyewe anaijua lugha ya kisukuma na Kiswahili!?

Bado ninangoja Kampeni iliyoendeshwa mwanzo mpaka mwisho kwa lugha ya kisukuma ..

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Umeeleza vizuri sana, sasa tungoje tuone mrejesho
 
Ukiona hivyo ujue hazikuhusu
 
Hili lijamaa,linaona kete iliyobaki ili liludi Ikulu ni ukabila kwenda mbele,kila sehemu linaandamana na boss wa TRL,Kadogosa,ambaye ni Msukuma,ili kumtumia Kama chambo ya kupata kura.
Nyerere aliyaona zamani,kitu likikosa sera,lazima litajipambanua kwa ukabila au dini.
Kikwete alijipambanua kwa udini alipoona mambo mazuri,huyu karata yake ya mwisho ni ukabila tu.
Hili jitu hili,lina "PHD"lakini haliwezi kuongea kiswahili vzr,lugha ya malikia,ndio kabisa,linazidiwa hata na mtoto wa Darasa la nne,wa English medium.
 
Anajariu kuwa please wana mwanza kuonesha yeye ni wakwao. Walichomfanyia juzi sio kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…