abou
JF-Expert Member
- Mar 4, 2011
- 372
- 390
Unajua sera za vyama vya upinzani kuhusu muungano na muundo wake ? Huu ni mfano wa namna CCM tuna SERA ambazo hatuwezi kuzilingalisha na wengine, inashangaza kuwa unataka ulinganishe sera za CCM na vyama vingine.Kwanza wewe si mwanaCCM.
Pili lazima ukubali hakuna sera mbaya.. ikiweko hapa ilete niione.. tunachotofautiana ni uwezo was kuushawishi umma utuchague.. na Kama chama Cha Mapinduzi kinao msingi na mfumo Bora wenye ushawishi.
Tatu hakuna aliyetumia lugha ya asili mwanzo mpaka mwisho kufanya kampeni.. na maneno Kama Wasukuma wanasema..."insert Maneno hapa" hazijaanza kutumika leo kwenye siasa.
Tatizo ni kujiona hii Tanzania ni ya wasomi na Kiswahili kinaeleweka pote.. you are very mistaken"Mjuba" huifahamu Tanzania. Tembea Kisha urudi hapa useme Tena haya unayoyaandika.
Na hizi asili ndizo building blocks za Taifa Hili.. huwezi kupenda mchuzi (Uswahili) halafu ukachukia kitunguu na nyanya(makabila ya kibantu) utakuwa hayawani.
Siasa Duniani kote zinaendeshwa namna moja.. iwe Marekani iwe Uingereza iwe Urusi Japan kote... Ni jukumu la mwanasiasa kuconnect on individual level na wapiga kura..
Huko walikoendelea wasingesafiri na kufanya mikutano ya hadhara.. wangekaa kwenye tv wakazisoma sera na kuzidadavua kwa undani kabisa if that wa simple as you put it.
Running a country is one thing and getting elected is another.. Waacheni wenye ujuzi na hayo wafanye kazi yao.
Btw..sheria inaruhusu lugha hizi kitumika pale inapohitajika na mkalimani awepo.. Sasa Dr. JPM anahitaji mkalimani gani wakati yeye mwenyewe anaijua lugha ya kisukuma na Kiswahili!?
Bado ninangoja Kampeni iliyoendeshwa mwanzo mpaka mwisho kwa lugha ya kisukuma ..
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Pili, msingi wa hoja yangu ni kauli zako ulizozitoa kuwa mgombea wetu hana ushawishi wa kisera na anatumia kilugha kama njia ya kushawishi , na sisitiza tumekuwa tukishinda chaguzi sababu tuna ushawishi wa kisera kwa wapiga kura wetu nchi nzima bila kujali tofauti zao, na hata huyu JPM u ayedai hana ushawishi na hawezi kuuza sera zetu, hakuchaguliwa kwa sababu nyingine , ni kwakua aliweza kuuza sera zetu kwa ushawishi alionao kwa wapiga kura, si kwasababu ya kabila lake. Tatu si kweli kuwa kiswahili ni lugha ya wasomi, kiswahili ni lugha ya watanzania wote, na inazungumzwa nchini kote bila kujali kiwango cha elimu cha mzungumzaji.
Mwisho, narudia kusisitiza kuwa JPM hajahutubia kwa kilugha, alisalimia kwa kilugha, hajatoa AHADI MAALUM YA SIRI kwa wazungumzaji wa kisukuma,AMESALIMIA kwa kilugha. Kama unaushahidi wa JPM kuhutubia kwa kiligha wewe ndiyo uuweke, vinginevyo ni jitihada zenu za kukichafua chama huku mkijifanya wanachama
Ziada: Nilitegemea utasema mimi si mwana CCM kwakua ndiyo imekuwa kauli yenu mapandikizi, mnapo kizushia maneno chama (soma viongozi) tukiwasahihisha hilo ndilo jibu lenu. Lakini ukweli ni kuwa HAKUNA hotuba ya kilugha kama ipo, iweke. Na sera zetu ni bora kwa ustawi wa watu na taifa, kama hutaki, wafuate unaoona wana sera kutuzidi.