Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Amepuuza vilio vya watanzania kuhusu biashara zao kudorora, vijana kukosa ajira na kutoyakemea matukio ya utekaji, mauaji, matusi ya Musiba kwa wazee wastaafu na mengine mengi.

Alifanya maamuzi mengi kibabe. Mfano kukataza mikutano ya siasa, kukataza bunge kuwa live, n.k kwa kisingizio kuwa watanzania wachape kazi. Lakini yeye kutwa kucha yuko mubashara hata kwa mambo yasiyo na umuhimu.

Laiti kama Magufuli angekuwa msikivu, mnyenyekevu na mpenda watu, uchaguzi huu ungekuwa rahisi kwake.
 
Kusema kampeni za Ccm ni ngumu ni vichekesho
Rais Magufuli hata asipopiga kampeni kuanzia leo ushindi ni 90%

Rafiki zetu wa Chadema mtaula wa chuya huu mwaka hampati hata mbunge
Ndo mana anaambatana na bongo movies, bongo flaver na kina maria nyerere kuongeza vichwa hahaha hizi degree za kudesa hizi mbaya sana
 
Tatizo watu wanakuwa na maana zao za usikivu na unyenyekevu ambazo ni za kumtaka kiongozi aendeshe nchi kwa matakwa yao.

Tupo milioni 59 ikiwa rais atamsikilza kila mtu hip haitakuwa nchi bali itakuwa Bar.

Kampeni hazijadorora tena zimeboreshwa kwani mashambulizi yanatokea kila upande.

Mama Samia, Pinda, Kikwete, JPM na Majaliwa wanashambulia jukwaa katika mikoa tofauti huwezi kulinganisha na Lissu anayetembea mkoa mmoja hadi mwingine na akipitisha michango kwa wanaomsikiliza.
 
Kusema kampeni za Ccm ni ngumu ni vichekesho
Rais Magufuli hata asipopiga kampeni kuanzia leo ushindi ni 90%

Rafiki zetu wa Chadema mtaula wa chuya huu mwaka hampati hata mbunge
Ingekuwa nikweli CCM wasingejichosha kubeba watu kwenye malori Kama mifugo
 
Anatia aibu huyu mgombea. Miaka 5 ikulu lkn watanzania wanamkataa kama wote.
Mbishi anahisi anachofikiria yye ni sahihi kwenye kila jambo. Hivi unamtoza mmachinga kodiak ya 20 kwa mwaka wakati wewe mshahara wako hulipi kodi . Unapora KOROSHO za watu na kuwalipa kwa mafungu ili uonekane una maamuzi yasiyoyumbaa kisha kesho unaenda kuomba kura siyo ujinga nn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…