Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Mmh we Mwanza iache hivyo hivyo, umesahau kwa Lowasa walideki hadi barabara, kwenye kura wakamtosa.

Halafu upinzani mnafeli kitu kimoja, nyie mna amini zaidi kampeni za majukwaani kujaza watu, mkiona nyomi mnadhani mmewini, CCM kampeni za jukwaani ni geresha tu.

Wana msemo wao wa nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, kitanda kwa kitanda na shuka kwa shuka.
Kusomeshwa namba ni kampeni tosha,mengine ni kukamilisha formality tu
 
Maskini. Hivi huko majimboni wagombea wa ubunge wananadi Sera gani. Maana huko vijijini hawajui flyover, sgr, bombadia wala striglers. Kazi ipo
 
Nimeona watu wamesimima hapo,

Mleta mada itakua sio mtu ndio maana hafahamu hata wenzake wanafanana vipi.
 
Angalia ukali wa maneno..Je maneno hayo angesema mwingine(vyama vya upinzani) wewe au watu wa mtazamo wako huwa munasema matusi!
Ukali wa maneno?!?! Ni namna wewe ulivyoipokea habari...ukiwa positive hakuna ukali wa maneno hapo...ila ukiwa negative na kutafuta makosa ya JPM ndipo utaona kuna ukali wa maneno...it is about perception ...
 
Kwa miaka mitano nimekuwa nikisikiliza hotuba za JPM hadi nikiwa nikimuona simfuatilii nikijua ni yale yale ya kila siku. Ndege zimekuwa ndege, mradi wa umeme, reli ya umeme, viwanda, mafisadi, barabara na kunuuunua kuku na mihindi njiani.

Nilishindwa kumfuatilia zaidi hasa pale alipoamua kwa nguvu zote mchana kweupeee kuwananga wapinzani na kuonyesha ubaguzi wa wazi. Alitamka wazi kuwa yeye hapeleki maendeleo kwenye majimbo ya wapinzani.

Kwa ubaguzi huu nikadhani alikuwa anaongea kisiasa kumbe alikuwa na dhamira ya kweli. Kuna siku, mama mmoja aliomba maji akaambiwa ana kiherehere na amuombe mumewe au mbunge na diwani wake aliyemchagua.

Leo yupo Ikungi anaomba ndugu wa Lissu na Lissu mwenyewe kura. Hakumbuki kwamba serikali yake ndiyo ilimunyima hela za matibabu, mshahara na kumfukuza kazi ya ubunge. Leo amejisahau.

Nilidhani atasema ni kwa nini hajatoa ajira, hajawajaongeza watumishi mishahara na kwa nini aliwaambia kuwa hakuchaguliwa ili aongeze mishahara? Mwisho niseme tu hakuna jipya ambayo nilisikia na leo ataongezea.

Jipya kasema atampa Lissu kazi. Mengine ile timu yetu FC kama kawaida.
 
Hayo ameyasema raisi Pombe, muda siyo mrefu kwenye kampeni zinazoendekea mkoani Singida, nanukuu.

"Elimu ni bure, wakinamama zaeni hakuna haja ya kupanga uzazi, matiti ya kunyonyesha mnayo, wanaume wa kuwapeni mimba wapo."

Toa maoni je ni kweli kupanga uzazi hakuna maana kama wataalamu wanavyo shauri, hii siyo mara ya kwanza Magufuli kuwaambia watanzania kuwa zaeni, msipange uzazi.
Mimi hata sijui,kwa sababu mbali na elimu bure ,yapo Mambo mengine, afya,makazi,chakula haha yanapatikana je,au ndio kutengeneza wanyonge wakutosha ili tufanikiwe.
 
Hujuma na Uhuni unaofanywa na ccm kwenye uchaguzi imewafanya watz wachukie siasa...
 
Magufuli lazima Mungu ampe Uraisi Ni Raisi pekee duniani ambaye anatamka wazi watu wamshangilie Mungu kwa kutushindia Corona Tanzania

Hafichi anasema Kama watu wanataka ushuhuda wa Mungu jinsi anavyoweza waje Tanzania waone ukuu wa Mungu

Hakuna Raisi popote duniani awe mfalme au Raisi aliyekiri uwezo wa Mungu mbele ya eating na ushahidi wa ushuhuda wa wazi wa ukweli Kama Magufuli

Kamtukuza Mungu na Mungu atamtukuza kwa kumpa uraisi.Sababu anataka Watu wote wamshukuru Mungu na kamtukuza kwa kazi kubwa aliyoifanya Tanzania na hampaki Mungu kwa sifa za uongo au za kutunga anampa sifa halisia sio fake au za kuandaa watu wamsifie

Uraisi Mungu atakupa Magufuli Hakuna nchi duniani hata Moja iliyoona God factor Ni muhimu kupambana na Corona umejipambanua pekee na Mungu .Wengine walifunga majumba ya ibada hata dini zilikotoka iwe Ulaya , Marekani , Uarabuni au Vatican nk ulikataa kuheshimu Mungu .

October 28 Mungu lazima atakupa uraisi kwa kumheshimu Mungu mikutano ya kampeni zako kwa kazi kubwa Mungu kalifanyia Taifa kuliokoa na janga la Corona

Wapinzani wako wao na Mungu kwenye Corona hawana muda wa kumsifu wanaponda tu!! Hawaoni kazi kubwa aliyofanya Mungu kwenye Hilo seals
Jiandae tu kuapishwa maana Mungu kakukubali sababu unakiri uwezo wake hadharani

Anza kushona suti ya siku ya kuapishwa
 
Tuliposema amejipitisha kwa nguvu kwenda kumsaidia Magu kwenye kampeni hatukukosea

Sasa ni aibu tupu mkutano wa waziri mkuu kukosa watu kiasi hiki

Kumbe bila wasanii hata Magufuli Hana watu.


Ni aibu mwaka huu hata mama Samia naye kakosa watu kisa kulikuwa hakuna malori ya kuwasomba

View attachment 1555613
Sawa...jidanganyeni hivyo hivyo...lakini isije ikawa mnajenga hapa hoja ya kinachodaiwa wizi wa kura ...mnaweza kuja kulalamika kuwa mikutano ya CCM ilikuwa Haina watu Sasa inakuaje wapate ushindi wa kishindo..
 
Kiki ya Corona ilishapita

Nasisi tutasema miujiza ya risasi 38 ndio itampeleka Lissu Ikulu.
 
Mwaka 2015 wagombea wa CCM maeneo mbalimbali wakati wa kampeni walipiga Sana pushap. Mwaka huu nafuatilia kampeni lakini sioni dalili za wagombea kupiga pushap?

Nini kimefanya pushap kupuuzwa awamu hii?
Ameshakuwa dictator mzoefu/dictator aliyekubuhu! He is agressive supreme of power!
 
Acha blah blah njoo na hoja za maana.
Kama kumtaja mungu, hata wauaji na wachawi humtaja mungu, tena kwa unyenyekevu na kutetemeka.
 
Kama Mungu aliagiza hivyo na kumaanisha, ilikuwaje Adam na Hawa wakazaa watoto wawili tu? Na Ibrahim ilikuwaje azae watoto wachache licha ya kuoa wanawake wawili? Uwe unairuhusu akili yako kuwa huru unaposoma maandiko ili uyalinganishe na mazingira uliyopo na sio unasoma kikasuku!
Au ccm Ina lengo la kuongeza idadi ya ombaomba barabarani? Haiyumkini karibu ombaomba wote wanatoka Kanda pendwa
hi
Kama Mungu aliagiza hivyo na kumaanisha, ilikuwaje Adam na Hawa wakazaa watoto wawili tu? Na Ibrahim ilikuwaje azae watoto wachache licha ya kuoa wanawake wawili? Uwe unairuhusu akili yako kuwa huru unaposoma maandiko ili uyalinganishe na mazingira uliyopo na sio unasoma kikasuku!
Au ccm Ina lengo la kuongeza idadi ya ombaomba barabarani? Haiyumkini karibu ombaomba wote wanatoka Kanda pendwa!

Mwanzo 25:1-2
Ibrahimu alioa mke mwingine jina lake akiitwa Ketura.
Akamzalia Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Sua.
baada ya kufa mkewe Sara, Ibrahim alioa na kupata watoto wengine 6
Muwe mnasoma vizuri Biblia
 
Kumtaja kumtaja Mungu kiholela ni ishara ya unafiki wa kiwango cha SGR.
 
Siku hizi kuna corona na wakati ule corona haikuwepo; hivyo wanaogopa yaliyompata Nkurunzinza!!
 
Jipya ni kwamba amesema anataka amuajiri TL kwa hiyo amwachie Urais
 
Kiki ya Corona ilishapita
Haihapita nchi zote zinazotuzunguka wanahaha nayo,Ulaya Wana haha nayo, Marekani wanahaha nayo sisi hao wazima wa afya tunadunda mitaani

Hata Ubelgiji Lisu alikotoka alitua na Libarakoa akadhangaa watu wako fit

Magufuli hiyo ya kumshukuru Mungu kea kutushindia corona Ni kick kwake kwa Mungu sio kwa watu ukiwemo wa Aina ya wewe

Mungu ndio huamua yupi anampa kick ya kumtukuza ampe utawala .Kick ya Magufuli Mungu kwake anaikubali atampa uraisi hata wewe usipompa kura sababu utawala hutoka kwa Mungu . Magufuli hahitaji kick yako mpagani wewe
 
Back
Top Bottom