Kwa miaka mitano nimekuwa nikisikiliza hotuba za JPM hadi nikiwa nikimuona simfuatilii nikijua ni yale yale ya kila siku. Ndege zimekuwa ndege, mradi wa umeme, reli ya umeme, viwanda, mafisadi, barabara na kunuuunua kuku na mihindi njiani.
Nilishindwa kumfuatilia zaidi hasa pale alipoamua kwa nguvu zote mchana kweupeee kuwananga wapinzani na kuonyesha ubaguzi wa wazi. Alitamka wazi kuwa yeye hapeleki maendeleo kwenye majimbo ya wapinzani.
Kwa ubaguzi huu nikadhani alikuwa anaongea kisiasa kumbe alikuwa na dhamira ya kweli. Kuna siku, mama mmoja aliomba maji akaambiwa ana kiherehere na amuombe mumewe au mbunge na diwani wake aliyemchagua.
Leo yupo Ikungi anaomba ndugu wa Lissu na Lissu mwenyewe kura. Hakumbuki kwamba serikali yake ndiyo ilimunyima hela za matibabu, mshahara na kumfukuza kazi ya ubunge. Leo amejisahau.
Nilidhani atasema ni kwa nini hajatoa ajira, hajawajaongeza watumishi mishahara na kwa nini aliwaambia kuwa hakuchaguliwa ili aongeze mishahara? Mwisho niseme tu hakuna jipya ambayo nilisikia na leo ataongezea.