Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu. Na maendeleo ya watu, jambo la kwanza ni uhuru, haki na utu wake. Hivyo vitu vitatu visipokuwepo, chochote utakachokifanya hakina mantiki kwa ustawi wa mwanadamu.
Tangu enzi za kale, tangu enzi za wayahudi, watu wanaongelea uhuru. Wayahudi walimsubiri masiha kwa miaka elfu 40, wakiamini kuwa huyo masiha atawafanya wawe watu huru. Hawakumsubiria ili awajengee barabara, nyumba, reli au umeme, maana hayo waliamini hata mkoloni wao Mrumi alikuwa ana uwezo wa kuwafanyia. Alichowanyima Mrumi ni uhuru wao.
Magufuli kokote aliko, ajue kuwa hata angefanikiwa kutengeneza reli ya angani lakini akaendekeza siasa za kuwanyima watu uhuru, siasa za kuwadhalilisha watu, siasa za kuwabagua na kuwapendelea watu, siasa za kuwanyima watu haki, kamwe hatakumbukwa kwa mema bali kwa mabaya yake. Na atakuja kuwekwa kwenye historia kuwa ndiye alikuwa kiongozi wa kwanza mbaya kwa Taifa letu.
Rais Magufuli anatakiwa ajue kuwa katika ubinadamu wake, hakuna anachowazidi wanadamu wengine. Pamoja na kuwa kwamba yeye ni Rais lakini bado ni mwanadamu, tena mwenye mapungufu mengi, na wengi wanamzidi katika mengi, kuanzia akili, maarifa na uelewa wa mambo mengi. Asijione kama yeye ana mamlaka ya kuamua nani aishi na nani afe, nani awe huru na nani atekwe au kupotezwa. Mabaya aliyoyafanya ayajutie na atubu kwa dhamira na siyo kwa unafiki.
Sent using Jamii Forums mobile app