Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Majimbo na mikoa vinatofautiana nini?
Sisi tunataka wote wanaoongoza wachaguliwe na wananchi. Siyo huu ujinga wa sasa!
... mambo ya teuzi kulipa fadhila hayo! Bila teuzi ata-exercise vipi mamlaka yake? Ataonesha vipi kwamba ndiye alpha na omega? Ikimpendeza humpa huyu na kumnyima yule bila yeyote kuhoji! Mfumo unatakiwa kufumuliwa na kusukwa upya vinginevyo kama nchi hatutoki kwa huu "uraisi wa kifalme" hata aje Jibril tutapiga maktaimu tu!
 
Akiwa Urambo JPM amewaonya watanzania kuwakataa wanaohubiri kuigawa nchi katika majimbo, sera hiyo ni hatari kwa mstakali wa umoja wa Taifa letu,amesema sera hiyo ni ubaguzi mtupu kwani majombo masikini yatabaki maskini.
Lakini yeye ndo anayewagawa waTanzania, kwamba hapeleki maendeleo kwenye majimbo ya wapinzani. Nadhani hiyo mianya ya kuwa na sera ya majimbo ni yeye mwenyewe anachochea.
 
Hana hoja huyo ,sisi sio wajinga wa kipindi chao kwamba hatujui uzuri na ubaya wake.Binafsi majimbo ndio kila kitu..Jimbo gani nchi hii ni maskini? Na Jimbo linaletaje ukabila?
Hii ni dalili ya hofu ya ccm kupokwa njia za kujinufaisha kwa pesa zetu kwa kutumia mgongo wa kihubu kimoja.
Swali je Leo hii chini ya mikoa,kuna maendeleo sawa baina ya mikoa? Kama jibu ni hapana Hana hoja
 
Kuna hela zitatoka central government kwa akili ya miradi ya maendeleo kama jimbo halijitoshelezi.
Ni kweli ila hutolewa kwa percentage ya contribution uliyotoa kuchangia uendeshaji wa serikali kuu kupitia makusanyo ya kodi ya serikali kuu kwako mfano ulikusanya kodi za serikali kuu kwenye eneo lako za milioni 100 e.g. kodi ya majengo au ardhi serikali kuu inakupa milioni 30

Sio kuwa kuna Pesa za bure toka serikali kuu kuja kwako toka migodi ya Dhahabu ya Geita ilipo Chato au gesi ya mtwara au pesa za utalii za Kilimanjaro au za bandari ya Dar es salaam zije kwako hakuna
 
Singida kwa Lisu wanakotegemea kuuza alizeti wataongoza kwa umaskini Tanzania
Unaposikia Sera ya majimbo unaelewaje kwani??? Unafikiri Mkoa ni jimbo au unafikiri ni majimbo haya ya uchaguzi ya wabunge????

Maana kama mnafikiri hayo mawili hapo juu wote mtakuwa mnakosea Kwa iyo ni vizuri kumwambia akili kubwa Tundu Lissu awaeleweshe!

Sera ya majimbo ya Tundu Lissu anaamaanisha kuunganisha mikoa na kuifanya Jimbo moja nyie vilaza wa Lumumba. Sasa kama Singida, Dodoma, Tabora na Morogoro ikiwa Jimbo moja la kati itakuwaje wakakosa maendeleo???

Alafu singida ipi unayosema haina rasilimali??? Hujui singida Kuna madini, na mapori ya akiba yenye wanyamapori wengi tu????
 
... hakuna eneo la Tanzania ambalo ni maskini kwa asili yake; ni sera mbovu ndizo zimepelekea umaskini wa kutisha kwa baadhi ya maeneo kama sio nchi nzima. Nchi hii ni tajiri kila mahali - watu wapo; ardhi ipo tele kila mahali! Changamoto iko kwenye SIASA SAFI na UONGOZI BORA - as simple as that!
Hakika umenena mkuu

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
Huyo babu yenu urais wenyewe alisokomezwa tu wala hakujiandaa kuwa rais, so sera ya majimbo hawezi kuielewa
 
Hao wapiga kura anaowadanganya ndo asilimia 75% ya Wadanganyika ambao pia ndo majority ya wapiga kura.Wengi wao hawana exposure na shule hawajaenda. Pia ni maskini wa kutupwa.
 
Unaposikia Sera ya majimbo unaelewaje kwani??? Unafikiri Mkoa ni jimbo au unafikiri ni majimbo haya ya uchaguzi ya wabunge????
Sera ya majimbo ya Tundu Lissu anaamaanisha kuunganisha mikoa na kuifanya Jimbo moja nyie vilaza wa Lumumba. Sasa kama Singida, Dodoma, Tabora na Morogoro ikiwa Jimbo moja la kati itakuwaje wakakosa maendeleo???
Sera za majimbo Lengo lake asiweko mnyonya mwingine .Hata uunge Singida na mtwara liwe Jimbo moja sio kuwa gesi ya mtwara mapato yake atayafaidi muuza alizeti lofa singida
Mtawala wa serikali ya Jimbo anaitwa gavana. SERIKALI yake huendeshwa kwa kila mikoa ndani ya Jimbo kuchangia gharama za uendeshaji na mapato ya mkoa mmoja kwenye Jimbo huwezi peleka mkoa mwingine
 
Tatizo ni akili yako??? China , Marekani na Ujerumani magavana wanafaidi nini???
 
Asituchagulie wa kutuongoza yeye hana hati miliki ya Tanzania.
Tutachagua mtanzania,
Hatutachagua mtu kwa kivuli cha huyu juha wenu hapa,
20200921_110910.jpg
 
Tatizo ni akili yako??? China , Marekani na Ujerumani magavana wanafaidi nini???
Ni maraisi wa majimbo kama sisi tunavyochagua raisi wa Zanzibar ndivyo ilivyo kule

Magavana ni maraisi wa majimbo na wana nguvu kama Raisi wa Zanzibar alivyo na nguvu
 
Back
Top Bottom