Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Rekodi ya kazi nzuri aliyoifanya JPM inajieleza na Wazalendo wote tunajukumu moja tuu October 28th ni kumpatia kura nyingi JPM na kumpatia wabunge na madiwani wengi.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Tangu ameingia kwenye ngome ya upinzani ni hatari tupu....anatumia silaha za maangamizi...anaingamaza kabisa upinzani kasikazini, leo hii trh anachakaza ngome ya mwenyekiti wa chadema ndg. Mbowe.

dakika hizi za majeruhi ni silaha za maangamiza tu...ukizinduka Rais na wabunge wameshatangazwa. Hii hatari...nilisha sema ccm wanatumia sayansi ya hali ya juu.. na utashangaa

Mbowe anafutwa rasmi ktk raamani ya siasa ktk jimbo la hai
 
MAGUFULI ni kiongozi mwenye uthubutu na uwezo mkubwa katika kujenga mifumo inayojenga msingi imara wa uchumi wa kisasa, uchumi shindani, uchumi jumuishi, uchumi wa kitaifa unaolenga kunufaisha wa Tanzania. Huyu ndie atakaetufikisha kwenye nchi ya asali na maziwa.#kaziendelee #28MAGUFULIDAY
 
Mheshimiwa Rais ninakuandkia waraka huu kwanza kwa kukupongeza kuhusu kazi kubwa uliyoifanya katika kampeni hii ya uchaguzi wa 2020. Kwa kweli umeendesha kampeni ya kisayansi kwa kutumia mbinu mbalimbali kuwafikia wapiga kura. Pamoja na hilo umetekeleza mambo yafuatayo:

1. Kuendesha kampeni kwa ustaarabu
2. Kupeleka ujumbe wa mambo uliyoyatekeleza kwa ufasaha
3. Kuendelea kutekeleza majukumu yako na hapo hapo ukielekeza utekelezaji wa miradi
4. Kuendelea kuahidi utakayoyafanya awamu ijayo
5 kwa uungwana na unyenyekevu kabisa ulipokosea umeomba radhi na kuahidi kurekebisha ie suala la kuongeza mishahara
5. Umetumia lugha ya staha wakati wote kama kiongozi wa nchi
6. Umeelezea vizuri maendeleo uliyofanya na yanaonekana kwa macho kwa wapiga kura.

Kwa haya machache mimi binafsi ninakutakia ushindi mnono kesho ili uweze kuendelea na uongozi wa nchi kwa ulipotufikisha tayari tunayo matumaini makubwa mno.MUNGU AKUBARIKI.

Donald Ndagula
 
Katika siku za mwisho za utawala wa mfalme Sauli, licha ya utisho wake mbele za anaowatala, haikuwa salama yake ya kubaki ktk kiti chake cha ufalme. Jambo hili lilikuwa ni bayana kwa kuwa Mungu alimkataa.

Magufuli licha ya kuzungukwa na washauri wengi waliokuwa wanafiki kupitiliza, lkn kuna jambo kubwa sana wanalitambua juu yako. Ndiyo! Wanatambua kwa dhati kuwa hukubaliki wala Watanzania hawakupendi.

Magufuli linahitaji kubaki kuwa jina lako, pengine kidogo na "attribute" ya Rais mstaafu na kiongozi wa kiimla. Hilo la shahada yako ya uzamivu itakupasa ujitetee wewe mwenyewe, mimi wala sina ugomvi na wewe.

Naiona Tanzania mpya chini ya Tundu Lissu na Maalim Seif. Magufuli nenda, Magufuli nenda kwenu Chato. RIP CCM.
 
Back
Top Bottom