GE2025 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Samia Suluhu na Dkt. Emmanuel Nchimbi

GE2025 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Samia Suluhu na Dkt. Emmanuel Nchimbi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa tapeli Mwamposa wanakwenda wenyewe lakini hao wa CCM wanasombwa kama ng'ombe wanaopelekwa mnadani
JamiiForums1012362808.jpeg
Screenshot_20230918-210933.jpg
FB_IMG_1756473614429.jpg
 
inakuwaje wapiga picha hawana camera nzuri za kudakua kila mtu ukizoom waonekane,
wajiongeze picha zitoke bombaaaaaaa hakuna za kuwepo za kama enzi za kale
 
Ulikuwa chini ya uangalizi wa wazazi kipindi cha Mabadilikoo???!! Rowasaa!!!!! Rowasaaaa????? Mabadilikooo!!!!!hapo hujaona nyomi la Agustino Mrema ile ilikua funga kazi sasa sijapta kuona nyoma kama la Mrema
 
Ukishaona umati mkubwa hivyo na asilimia 90 wana jezi jua FIAT zimehusika.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
ndugu watanzania wenzangu kamwe usishidane na mtu aliyepewa libali na mungu, Ona nyomi la watanzania lilivyo kusanyika kumsikiliza Mhe.Samia Suluhu
WhatsApp Image 2025-08-31 at 7.31.14 AM.jpeg
 
View attachment 3461055
Sijawahi kuona katika miaka ya karibu watu wengi Kwa pamoja kama hawa wanaohudhuria mikutano ya Rais Samia,

JE, ni kupendwa?
Hapendwi mtu hapo, hao wameshurutishwa kuhudhuria ikabidi watii amri bila shuruti. Ukitaka kujua hilo angalia hata nyuso zao, hawana ile vibe ya mikutano ya siasa iliyozoeleka.

Wengi wa hao ni waalimu na watumishi wengine wa serikali.
 
DKT.NCHIMBI AWANADI WAGOMBEA UBUNGE,MADIWANI WA SIMIYU KWA WANANCHI

MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi amepokelewa kwa shangwe na wananchi alipokuwa akiwasili katika uwanja wa CCM,wilaya ya Bariadi Vijijini mkoani Simiyu kuendelea na mkutano wa Kampeni, leo Jumatatu Septemba 1,2025.

Dkt. Nchimbi aliyekuwa Mkoa wa Mara na sasa ameingia Mkoa wa Simiyu kuendelea na kampeni,akianzia jimbo la Busega na baadae kuelekea jimbo la Bariadi Vijijini na kufanya mikutano mikubwa ya hadhara.

Akiwahutubia wananchi wa Bariadi Vijijini mkoani Simiyu, Dkt.Nchimbi ambae ni Mgombea Mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, pia alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi Vijijini,Masanja Kungu Kadogosa sambamba na wagombea ubunge wengine pamoja na Madiwani wa mkoa huo.

Dkt. Nchimbi anaendelea na kampeni zake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania kuwaongoza katika awamu nyingine ya miaka mitano, katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025.
 

Attachments

  • 20250902_060429.jpg
    20250902_060429.jpg
    149.5 KB · Views: 34
  • 20250902_060432.jpg
    20250902_060432.jpg
    160.7 KB · Views: 25
  • 20250902_060440.jpg
    20250902_060440.jpg
    195.7 KB · Views: 25
  • 20250902_060442.jpg
    20250902_060442.jpg
    179.6 KB · Views: 25
Back
Top Bottom