Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 04, 2025, ameendelea na mikutano yake ya kampeni katika Mkoa wa Songwe. Akiwa Mlowo, Jimbo la Mbozi, alilakiwa na wananchi waliokusanyika kwenye viwanja vya mkutano, wengi wao wakiwa wamebeba bendera na kuvaa nguo za kijani na njano rangi za chama chake.
Dkt. Samia alipowasili alilakiwa kwa shangwe, ngoma za asili na nyimbo za hamasa, kabla ya kupunga mkono kwa umati uliojaa shauku ya kumsikiliza. Katika hotuba yake, alizungumzia changamoto za wananchi wa Songwe, hususan upatikanaji wa maji safi, barabara za vijijini na huduma za afya, akiahidi kuwa masuala hayo yataendelea kushughulikiwa katika awamu ijayo ya uongozi wake endapo atachaguliwa.
Aidha, alitumia nafasi hiyo kuwasisitiza wananchi kudumisha mshikamano, akisema kuwa maendeleo hayataletwa kwa mtu mmoja bali kwa mshirikiano wa Serikali na wananchi.
Wananchi waliokuwepo walionekana kuguswa na hotuba yake, huku baadhi wakimshangilia kwa kauli mbiu na nyimbo za kuunga mkono CCM.
#haijapatakutoka
#kurayakwanzakwasamia