Mikutano ya kisayansi ya kampeni za mgombea urais wa CCM Dr.Samia Suluhu Hassan kwa upande moja na mgombea mwenza Dr.Emmanuel John Nchimbi kwa upande mwingine, imepambwa kwa tsunami na mafuriko ya wananchi waliojawa shauku na hamasa ya kuwona kuwasikiliza, na hatimae kuwapigia kura nyingi sana za ushindi wa kishindo viongozi hao wa kitaifa pamoja na madiwani na wabunge wote wa CCM.
Hakuna dalili wala viashiria vya upinzani kuambulia kiti chochote, mahali popote uchaguzi mkuu wa October 29,2025.
Kumbuka,
miongoni mwa malengo ya kuanzishwa kwa chama cha Mapinduzi ni pamoja na kushiriki chaguzi, kushinda uchaguzi, kukamata dola, kuunda Serikali, kuongoza nchi, kuwatumikia wananchi na kuwaletea waTanzania wote maendeleo endelevu ya kijamii, kisiasa na kiuchumi na si vinginevyo.
Mungu Ibariki CCM
Mungu Ibariki Tanzania.
Kidumu chama cha Mapinduzi.