figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wakuu,

Nimeanzisha uzi huu ili tushikamane kama Watanzania kutafuta au kutoa taarifa ya watu waliopote. Kumeibuka wimbi la Watu wa kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Rais ndo Mwenyekiti wa kwanza wa usalama, kupitia thread hii ataweza kujua ni kiasi gani watu wanapotea bila hatua zozote kuchukuliwa.

Pili nashauri Polisi kama kuna mtu wamemkamata, watoe taarifa mapema kwa ndugu na jamii ili wajue yupo Mikono salama. Hapa chini naweka baadhi ya watu ambao wamepotea, post zao au Malalamiko ya ndugu zao.

Hivyo usikalie kimya hili tatizo la watu kupotea. Tujulishane ili Mamlaka zione tatizo lilivyo kubwa.

Karibuni.

Pia soma ===>>> Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati

=====

BAADHI YA MICHANGO YENYE TAARIFA ZA KINA KUHUSU ORODHA YA WATU WALIOPOTEA

PIA SOMA
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 

Kwa jina anaitwa Samuel John Mwita
Anafanyakazi Baobab secondary school. umri wake ni miaka 51 amepotea tangu jumatano tarehe 3/7/2024 Alfajiri.
Amepotea katika mazingira yasiyoeleweka RB number MPG/RB/980/2024. Ripoti ipo kituo Cha polisi Mapinga . Mwenye taarifa za kupatikana kwake atupigie kwa namba 0743812622 au 0712217762 au kituo Cha polisi kilicho karibu.

Sambaza kwa magroup mengi kwa ajili ya maombi na upatikanaji wa Mr. Samuel John Mwita.
 

Pichani ni Lenga Masunga Ng'hajabu, Muuguzi wa Hospitali ya KCMC -Idara ya Masikio, Pua na Koo(ENT). Amepotea katika mazingira ya utatanishi toka tarehe 04/07/2024. Mwenye taarifa yoyote kuhusu mtumishi huyu tunaomba ushirikiano wakumpata. piga namba 0658 450 667-0658 450 642
 
MAULIDI OMARY SONGAMBELE ni mfanyabiashara wa Kariakoo na mjukuu wa Mzee Alhaji Mustapha Songambele.

amepotea tangu tarehe 26 June 2024 alipokuwa anarejea nyumbani kwake baada ya shughuli zake Kariakoo.

Lakini nyumbani kwake hakufika na wala hajawahi kuonekana tangu tarehe 26 June 2024.

Ndugu zake wamejitaidi kumtafuta vituo vyote vya Polisi na Hospitali zote lakini hawajafanikiwa kumuona mpaka leo hii

Kwa mtu yoyote ataye fanikiwa kumuona anaombwa kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi au Kupiga simu kwa ndugu zake kwa namba za simu za 0626940955 au 0737107171.
 

Kada maarufu wa Chadema mkoani Tanga, Kombo Mbwana maarufu kama "Mzalendo" anadaiwa kutekwa Tarehe 16/06/2024 majira ya saa 2 mbili 2 asubuhi, akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Kwamatuku Wilaya Ya Handeni.Mke wa Kombo anasema siku ya tukio, walipata mgeni aliyejitambulisha kuwa ni "mtu wa serikali" akamtaka Kombo waongee, akieleza kwamba kuna eneo alinunua karibu na alipojenga Kombo. Baada ya kutoka Kombo hakurudi na hakupatikana tena kwenye simu hadi leo. Na huo ndio ulikua mwisho wa Kombo kuonekana hadharani.Hadi leo hajulikani alipo. Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Chadema mkoa wa Tanga, ndugu Michael Haule inaeleza kuwa wamemtafuta Kombo katika vituo vya Polisi na hospitalini lakini hawajamuona. Wametoa taarifa polisi lakini Kamanda wa Polisi amesema nao pia wanamtafuta. #JusticeForKombo #BringBackKombo
Your browser is not able to display this video.
 
"SADOCK JUMA MSUMI miaka yake 18,kabila lake ni MUHA mzaliwa wa BUKUBA -BUHIGWE-KIGOMA.

amepotea 05/07/2024 akiwa mkuranga pwani.

Aliamka asubuhi akielekea dukani, hata dukani hakufika na hadi Sasa hajulikani alipo.

UKIMUONA toa TAARIFA kwa kaka 0710859054 au kituo chochote Cha polisi kilichoko karibu.."
 
Mtoto huyu amepotea alitumwa kupeleka chakula Miyomboni Iringa mjini anaitwa Joshua iwapo unamtambua yupo Polisi Iringa Mjini
 
Anaitwa Furaha Augostino Lukosi ni mkazi wa Kinyerezi Kifuru,Dar es saalam.

Alipotea usiku wa tarehe 27 April 2024 kuamkia 28 April 2024 alfajiri saa kumi.

Alipakia abiria kijiweni kwake Kifuru toka hiyo siku hajaonekena tena.

Umri wake ni miaka 23, familia yake imezunguka vituo vyote vya polisi na hospital bila mafanikio.

Mtu yoyote akimuona au akipata taarifa apige simu namba 0718024723,+255 653 319 772,ni Dada yake..."
 
Wana x huyu mnayemuona.hapa alikuja kuchukuliwa na maaskari buza saa tisa mchana anaitwa Bakari Issa kambona alichukuliwa tarehe 26 mwezi wa kwanza hadi leo hajaonekana ndugu wametafuta kila kona wamemkosa
 
ANAITWA JANETH MGOO AMEPOTEA TOKA JUMATATU ILIYOPITA TAREHE 24 JIONI MAENEO YA TABATA BARAKUDA MTAA WA SAIBABA ALIAGA ANAENDA DUKANI KUNUNUA VOCHA ALIVOTOKA HAKURUDI TENA MPAKA LEO KAMA UTAFANIKIWA KUMUONA POPOTE TUWASILIANE KWA 0716766355/0684519497 MUNGU AWABARIKI ASANTENI
 
Bismilah rahamanirahiym.
Asalam aleykum ndugu zangu huyu mtoto hapo pichani amepotea ameokotwa na mwendesha pikipiki huko mbezi kibanda cha mkaa jina lake ilham makoye hivyo kwa yeyote anaemfahamu aende kituo cha polisi mbezi kwa magufuli
 
Sasa naanza kuogopa jamani mbona watu wanapotea sana kuna nn jamani🥱😭😭😭😭😭
 
Anaitwa ABDALA MAKUKA ana miaka 31 UR ni FT 5.8 mwenyeji wa Iringa tangu apotee ana siku ya tatu Leo hajulikani alipo msaada familia inalia kumtafuta kijana wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…